LA LIGA: VINARA REAL WAPIGWA UGENINI NA VALENCIA!

LALIGA-2016-17-2-3VINARA wa La Liga Real Madrid Jana walipokea kipigo chao cha Pili Msimu huu kwenye Ligi hiyo ya Spain walipochapwa 2-1 Ugenini na Valencia katika moja ya Mechi zao 2 za Viporo.

Valencia waliongoza 2-0 baada ya kufunga katika Dakika za 4 na ya 9 kwa Goli za Zaza na Orellana lakini Cristiano Ronaldo akaleta matumaini alipoachika Bao kwa Kichwa Dakika ya 44.

Goli hizo zilidumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili, Ronaldo alikosa nafasi ya kuisawazishia Real alipopaisha Kichwa chake.

Licha ya kufungwa, Real bado wapo kileleni mwa La Liga wakiwa na Pointi 52 kwa Mechi 22 wakifuata Mabingwa Watetezi FC Barcelona wenye Pointi 51 kwa Mechi 23 na Timu ya 3 ni Sevilla yenye Pointi 49 kwa Mechi 23.

VIKOSI:

Valencia:

1 Diego Alves

2 Cavaco Cancelo

24 Garay

5 Mangala

14 Gayá

8 Pérez

10 Parejo

9 El Haddadi

15 Orellana [Soler, 56']

17 Nani [Siqueir, 39']

12Zaza [Suárez, 74']

Akiba:

6 Siqueira

7 Suárez

11 Bakkali

13 Domenech

18 Soler

20 Medrán

23 Abdennour

Real Madrid:

1 Navas

2 Carvajal

5 Varane [Nacho, 73']

4 Ramos

12 Marcelo

19 Modric [Vázquez, 76']

14 Casemiro

8 Kroos

10 Rodríguez [Bale, 62']

9 Benzema

7 Ronaldo

Akiba:

6 Nacho

11 Bale

13 Casilla

16  Kovacic

17  Vázquez

21 Morata

22 Isco

REFA: Ricardo de Burgos Bengoetxea

LA LIGA

Ratiba

Ijumaa Februari 24

Las Palmas v Real Sociedad

Jumamosi Februari 25

Deportivo Alaves v Valencia C.F

Real Betis v Sevilla FC

CD Leganes v Deportivo La Coruna

SD Eibar v Malaga CF

Jumapili Februari 26

RCD Espanyol v Osasuna

Atletico de Madrid v FC Barcelona

Athletic de Bilbao v Granada CF

Sporting Gijon v Celta de Vigo

Villarreal CF v Real Madrid CF

NEYMAR APOTEZA RUFAA, SASA KIZIMBANI KUJIBU MASHITAKA YA RUSHWA KUHUSU UHAMISHO TOKA SANTOS KWENDA BARCA!

NEYMAR-RUSHWASUPASTAA wa Brazil Neymar ameshindwa Rufaa yake huko Spain na sasa itabidi atinge Kizimbani Mahakamani kujibu Mashitaka ya Rushwa yanayohusiana na Uhamisho wake wa Miaka Minne iliyopita kutoka Santos ya Brazil kwenda Barcelona.

Pamoja na Neymar, Rufaa za Klabu za Santos, Barcelona na Kampuni inayoendeshwa na Wazazi wa Neymar nazo zimeshindwa kwenye tuhuma hizo hizo na sasa kwa pamoja watatinga Kizimbani kujibu Mashitaka yanayotokana na malalamiko ya Kampuni ya Uwekezaji ya Brazil, DIS.

DIS imedai ilipaswa kulipwa Asilimia 40 ya Ada ya Uhamisho wa Neymar waliyolipa Barca kwa Santos lakini wakapewa Dau dogo huku gharama halisi zikifichwa.

+++++++++++++++++++++++

Undani wa Uhamisho wa Neymar:

-DIS ililipa Euro Milioni 1.4 Mwaka 2009 kwa Hisa zao za Umiliki wa Neymar wa Asilimia 40.

-Barcelona ilidai ililipa Euro Milioni 57.1 kwa Uhamisho wa Neymar na Santos kupata Euro Milioni 17.1.

-Waendesha Mashitaka huko Spain wanadai Santos ililipwa Euro Milioni 25.1 na hivyo DIS ilipaswa kulipa ziada ya Euro Milioni 3.2

+++++++++++++++++++++++

Waendesha Mashitaka huko Spain wanataka Neymar ahukumiwe Kifungo cha Miaka Miwili na Faini ya Dola Milioni 10 kwa lakini, kwa taratibu za Spain, kwa vile Kifungo hicho hakizidi Miaka Miwili na pia Neymar ni Mkosaji wa mara ya kwanza hatasekwa lupango na badala yake anaweza kupewa Kifungo cha Nje akipatikana na hatia.

Kwa upande wa Klabu, Waendesha Mashitaka wanataka Barca itozwe Faini ya Dola Milioni 9 na Santos Dola Milioni 7.

Mwaka Jana Mwezi Juni, Barcelona ililipa Faini ya Euro Milioni 5.5 Mahakamani baada ya kukiri kwa Mamlaka ya Kodi ya Spain ilikosea Mahesabu kuhusiana na Uhamisho wa Neymar na hivyo haikulipa Kodi stahiki.

Mwezi Julai Mwaka Jana, Mchezaji mwingine wa Barcelona Lionel Messi na Baba yake Mzazi walihukumiwa Miezi 21 Jela kwa udanganyifu kwenye ulipaji Kodi huko Spain lakini hawakutumikia Kifungo Jela kwa vile walikuwa Wakosaji wa mara ya kwanza na Kifungo chao kilikuwa cha chini ya Miaka Miwili.

PENATI YA DAKIKA 90 YA MESSI YAIPA BARCA USHINDI!

LALIGA-2016-17-2-3-1JANA Barcelona walihitaji Penati ya Dakika ya 90 iliyofungwa na Lionel Messi ili kuifunga Timu ya chini Leganes 2-1 katika Mechi ya La Liga iliyochezwa Nou Camp.
Barca walikuwa wa kwanza kufunga katika Dakika ya 4 kupitia Messi lakini Leganes wakasawazisha Dakika ya 71 kwa Bao la Unai Lopez.
Lakini Barca wakapata ushindi kwa hiyo Penati iliyotolewa baada Neymar kuangushwa ndani ya Boksi.
Wiki hii iliyopita haikuwa njema kwa Barca kwani Jumanne iliyopita walicharazwa 4-0 na Paris Saint-Germain katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Paris, France.
Kwenye Mechi hiyo baadhi ya Washabiki wa Barca Uwanja huo wa kwao Nou Camp waliamua kuizomea Timu yao.
Ushindi huu wa Barca dhidi ya Leganes umewaweka Nafasi ya Pili Pointi 1 nyuma ya Real Madrid wenye Mechi 2 mkononi.

 

LA LIGA: BALE AREJEA UWANJANI NA KUPIGA BAO REAL IKIPAA KILELENI!

BALE-AREJEABAO za Dakika za 33 na 83 za Alvaro Morata na Gareth Bale zimewapa Real Madrid ushindi wa 2-0 walipocheza na RCD Espanyol katika Mechi ya La Liga Uwanjani Santiago Bernabeu.

Ushindi huu umezidi kuwapaisha Real kileleni mwa La Liga wakiwa na Pointi 52 kwa Mechi 21 wakifuata Mabingwa Watetezi Barcelona wenye Pointi 48 kwa Mechi 22.

Raha kubwa kwa Real ilikuwa kumwona tena Fowadi wao kutoka Wales Gareth Bale akirejea Uwanjani baada kuwa nje akiuguza Enka kwa Siku 88 na kuingizwa Dakika ya 71 na kupata Bao baada ya muvu iliyoanzishwa na Cristiano Ronaldo na kumpasia Marcelo aliempenyezea Bale na kufunga.

Jumapili Barca wako kwao Nou Camp kucheza na CD Leganes.

VIKOSI:

REAL MADRID (Mfumo 4-3-3): Kiko Casilla; Carvajal, Varane, Pepe, Nacho [Marcelo 81']; Kovacic [Casemiro, 61'], Kroos, Isco; Vazquez, Morata [Bale, 71'], Ronaldo

Akiba: Rodriguez, Bale, Marcelo, Casemiro, Diaz, Asensio, Yanez

ESPANYOL (Mfumo 4-2-3-1): Lopez; D.Reyes, Lopez, O.Duarte, Martin; Fuego, Diop; J.Reyes [Pérez, 45'], Jurado [Alvaro, 82'], Piatti; Moreno

Akiba: Jimenez, R.Duarte, Alvarez, Caicedo, Perez, Vazquez, Roca

REFA: Alberto Undiano Mallenco

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Jumamosi Februari 18

Sporting Gijon 1 Atletico de Madrid 4

Real Madrid CF 2 RCD Espanyol 0

2030 Deportivo La Coruna v Deportivo Alaves

2245 Sevilla FC v SD Eibar

Jumapili Februari 19

1400 Real Sociedad v Villarreal CF

1815 Valencia C.F v Athletic de Bilbao

2030 Celta de Vigo v Osasuna

2245 FC Barcelona v CD Leganes

Jumatatu Februari 20

2245 Malaga CF v Las Palmas

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: REAL YAITWANGA NAPOLI!

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Mechi za Kwanza

Jumanne 14 Februari 2017

Benfica 1 Borussia Dortmund 0                 

Paris Saint Germain 4 Barcelona 0                

Jumatano 15 Februari 2017

Bayern Munich 5 Arsenal 1                 

Real Madrid 3 Napoli 1              

+++++++++++++++++++++++++

REAL3NAPOLI1MABINGWA WATETEZI Real Madrid wametoka nyuma kwa Bao 1 na kuitandika Napoli 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, iliyochezwa huko Santiago Bernabeu.

Napoli walitangulia kufunga kwa kombora la Lorenzo Insigne na Real kusawazisha kwa Bao la Karim Benzema.

Bao hizo zilidumu hadi Mapumziko.

Kipindi cha Pili Real walikwenda mbele 2-1 baada ya kazi njema ya Cristiano Ronaldo na kumlisha Toni Kroos aliefunga.

Bao la 3 la Real lilifungwa kwa kigongo cha Carlos Casemiro.

++++++++++++

MAGOLI:

Real Madrid 3

Karim Benzema 19

Toni Kroos 49

Carlos Casemiro 54

Napoli 1

Lorenzo Insigne 8

++++++++++++

Timu hizi zitacheza Marudiano yao hapo Machi 7 huko Italy na Mshindi kutinga Robo Fainali.

VIKOSI:

Real Madrid: Navas, Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo, Modric, Casemiro, Kroos, Rodriguez, Benzema, Ronaldo.
Akiba: Casilla, Pepe, Nacho, Kovacic, Vazquez, Morata, Isco.

Napoli: Reina, Hysaj, Albiol, Koulibaly, Ghoulam, Zielinski, Diawara, Hamsik, Callejon, Mertens, Insigne.
Akiba: Cabral, Giaccherini, Allan, Jorginho, Maggio, Maksimovic, Milik.

REFA: Damir Skomina (Slovenia).

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

Mechi za Kwanza

Jumanne 21 Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid              

Manchester City v Monaco               

Jumatano 22 Februari 2017

FC Porto v Juventus               

Sevilla v Leicester City           

Mechi za Pili

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza

Jumanne 7 Machi 2017

Arsenal v Bayern Munich [1-5]         

Napoli v Real Madrid [1-3]               

Jumatano 8 Machi 2017

Barcelona v Paris Saint Germain [0-4]                

Borussia Dortmund v Benfica [0-1]           

Jumanne 14 Machi 2017

Juventus v FC Porto               

Leicester City v Sevilla           

Jumatano 15 Machi 2017

Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen              

Monaco v Manchester City              

++++++++++++++++++++++++++++

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza

7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili

11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza

18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)