LA LIGA: BARCA SARE, ATLETI KIDEDEA, REAL KILELENI POINTI 6 MBELE YA BARCA!

Lionel-Messi-161127-Scores-G-300UKAME wa Barcelona kukosa ushindi huko Estadio Anoeta umeendelea na kuwa Mechi 8 baada ya Jana kunusurika kipigo na kutoka 1-1 na Real Sociedad kwenye Mechi ya La Liga.
Matokeo haya yamewaacha Barca Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Real Madrid ambao Jumamosi waliifunga Sporting Gijon 2-1 na Bao zao zote kufungwa na Cristiano Ronaldo.
Mapema Jana Atletico Madrid wakicheza Ugenini waliibamiza Osasuna 3-0 kwa Bao za Diego Godin, Kevin Gameiro na Yannick Carrasco.
Jana Barca walinusurika baada ya Willian Jose kuipa Real Sociedad Bao Dakika ya 53 na Lionel Messi kuwapa Sare kwa Bao la Dakika ya 59.
Barca, ambao hawajashinda huko Estadio Anoeta maarufu kama San Sebastian tangu 2007, nusura waonje kipigo cha 5 mfululizo  Uwanjani hapo pale Carlos Vela kupiga Posti mara 2 na Bao 'halali' la Juanmi kukataliwa kwa Ofsaidi.
Sasa kazi kubwa ipo kwa Barca kuwasimamisha na Ronaldo na Timu yake kwenye El Clasico hapo Jumamosi huko Nou Camp wakati Real Madrid wakitua hapo kucheza na Barcelona.
Hadi sasa baada Mechi 13 Real wapo Nambari Wakiwa na Pointi 33 wakifuata Barca wenye 27 pamoja nacSevilla na Timu ya 4 ni Atletico Madrid wenye Pointi 24.
LA LIGA
Matokeo 
Jumapili Novemba 28
Villareal 0 Deportivo Alaves 2
Osasuna 0 Atletico Madrid 3
Celta Vigo 3 Granada 1
Real Sociedad 1 Barcelona 1

LA LIGA: BAO ZA RONALDO ZAIPELEKA REAL JUU ZAIDI KILELENI POINTI 7 MBELE YA TIMU YA PILI BARCA!

RONALDO-HETITRIKI-ESPANYOLBAO 2 za Cristiano Ronaldo Leo zimewaweka Rela Madrid kuwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili Barcelona walipoifunga Sporting Gijon 2-1 kwenye Mechi ya La Liga iliyochezwa huku Mvua kubwa ikimwagika Uwanjani Santiago Bernabeu.

Ronaldo alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 5 tu kwa Penati iliyotolewa baada Lucas Vazquez kukatwa na Sergio Alvarez.

Dakika ya 18 Ronaldo akaipa Real Bao la Pili na kuongoza 2-0 lakini Sporting Gijon wakapata Bao lao 1 Dakika ya 35 Mfungaji akiwa ni Carlos Carmona.

Gijon walikosa nafasi ya wazi kuifanya Mechi iwe suluhu walipopewa Penati kwenye Dakika ya 76 na Duje Cop kuipaisha juu.

Kwa Real Mechi yao inayofuata ni ya La Liga Wikiendi ijayo huko Nou Camp kuivaa Barcelona lakini Barcelona Kesho Jumapili wako Ugenini kucheza na Real Sociedad.

VIKOSI:

Real Madrid: Navas, Danilo, Pepe, Ramos, Nacho, Kovacic, Modric, Rodriguez, Vazquez, Benzema, Ronaldo

Akiba: Casilla, Carvajal, Marcelo, Casemiro, Asensio, Isco, Mariano 

Sporting Gijon: Marino, Douglas, Lillo, Mere, Amorebieta, Isma Lopez, Carmona, Sergio, Rachid, Moi Gomez, Cop

Akiba: Whalley, Babin, Victor Rodriguez, Cases, Canella, Xavi Torres, Viguera

REFA: Alejandro José Hernández Hernández

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Novemba 25

SD Eibar 3 Real Betis 1

Jumamosi Novemba 26

Malaga CF 4 Deportivo La Coruna 3

Real Madrid CF 2 Sporting Gijon 1

2030 RCD Espanyol v CD Leganes

2245 Sevilla FC v Valencia C.F

Jumapili Novemba 27

1400 Villarreal CF v Deportivo Alaves

1815 Osasuna v Atletico de Madrid

2030 Celta de Vigo v Granada CF

2245 Real Sociedad v FC Barcelona

Jumatatu Novemba 28

2245 Las Palmas v   Athletic de Bilbao

LA LIGA: ZIDANE ‘KUTOMLINDA’ SERGIO RAMOS MWENYE ‘SMAKU’ YA KADI ILI ASIIKOSE EL CLASICO WIKIENDI IJAYO!

REAL-RAMOS-KADI21NI SIRI ya wazi kuwa Beki wa Real Madrid Sergio Ramos akimaliza Mechi bila Kadi yeyote basi hilo ni tukio adimu na linaweza hata kubeba Vichwa vya Habari huko Spain lakini safari hii anaombewa Wikiendi hii asipewe Kadi ili asiikose El Clasico Wikiendi ijayo.

Jumamosi hii, Vinara wa La Liga, Real Madrid, wako kwao Santiago Bernabeu kucheza na Sporting Gijon na Kocha wa Real Zinedine Zidane amesema Ramos atakuwemo Kikosini licha ya Kichwani mwake kuwa na Kadi za Njano 4 na akipata nyingine 1 yuko Kifungoni Mechi 1 LALIGA-NOV25na hivyo ataikosa Mechi ya Jumamosi ijayo Desemba 3 dhidi ya Mahasimu wao FC Barcelona huko Nou Camp.  

Akiongea na Wanahabari, Zidane amesema Ramos atacheza na Sporting Gijon kwani ni Mechi muhimu.

Pengine uamuzi huo wa Zidane unatokana na ukweli kuwa Real wana upungufu kwa safu ya Mabeki kufuatia kuumia Raphael Varane Juzi walipocheza Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Sporting Lisbon na pia Pepe kuwa ndio kwanza amerejea Kikosini kutoka kuwa Majeruhi.

Habari njema kwa Real ni kurejea Mazoezini kwa Kiungo wao Mbrazil Casemiro ambae alikuwa nje tangu Septemba kufuatia kuvunjika Mfupa wa Mguu.

Lakini pigo kubwa ni kuumia kwa Fowadi wao kutoka Wales Gareth Bale ambae aliumia Enka kwenye Mechi ya Juzi na Sporting Gijon na yupo hatarini kuukosa Msimu wote uliobakia.

Hivi sasa, baada ya Mechi 12, Real ndio wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 30 wakifuata Barca wenye 26 na Sevilla 24.

LA LIGA

Ratiba

**Saa za Bongo

Ijumaa Novemba 25

2245 SD Eibar v Real Betis

Jumamosi Novemba 26

1500 Malaga CF v Deportivo La Coruna

1815 Real Madrid CF v Sporting Gijon

2030 RCD Espanyol v CD Leganes

2245 Sevilla FC v Valencia C.F

Jumapili Novemba 27

1400 Villarreal CF v Deportivo Alaves

1815 Osasuna v Atletico de Madrid

2030 Celta de Vigo v Granada CF

2245 Real Sociedad v FC Barcelona

Jumatatu Novemba 28

2245 Las Palmas v   Athletic de Bilbao

SASA WAHISPANIA WAMSHUKIA SAMUEL ETO’O, WATAKA ASWEKWE JELA MIAKA 10!

ETOOWAENDESHA MASHITAKA wamependekeza Mahakamani huko Spain kuwa Samuel Eto'oafungwe Jela Miaka 10 na kulipa Faini ya Pauni Milioni 12 kwa Udanganyifu wa Kukwepa Kodi.

Eto’o anatuhumiwa kukwepa kulipa Kodi huko Spain inayokaribia Pauni Milioni 3.2 wakati akiichezea Barcelona kati ya Mwaka 2006 na 2009.

Pamoja na Eto’o, Waendesha Mashitaka hao pia wanataka Adhabu kama hiyo ya Eto’o apewe aliekuwa Wakala wake wakati huo Jose Maria Mesalles Mata.

Hivi sasa Eto’o, Mwenye Miaka 35, anaichezea Klabuya Uturuki Antalyaspor.

Mchezaji huyo kutoka Cameroun alianza Soka lake kwenye Chuo cha Real Madrid na kisha kujiunga na Real Mallorca Mwaka 2000 na Barcelona kumchota Miaka Minne baadae ambako aliisaidia kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 3 na UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 2 na kisha kuondoka Mwaka 2009 kwenda Inter Milan.

Akiwa na Inter Milan, Eto’o alitwaa Ubingwa wa Ulaya Msimu wa 2009/10 chini ya Jose Mourinho.

Taarifa hizi za kutaka kusulubiwa Eto’o zimekuja Siku 1 tu baada ya Mahakama huko Spain kupendekeza Mchezaji wa Barcelona kutoka Brazil Neymar afungwe Miaka Miwili pamoja na kudungwa Faini ya Dola Milioni 10.6 kuhusiana na Kesi ya Udanganyifu wakati wa Uhamisho wake kutoka Santos ya Brazil kwenda Barcelona Mwaka 2013.

Mapema Mwaka huu, Mchezaji mwingine wa Barcelona, Lionel Messi, alishitakiwa kwa Udanganyifu na Ukwepaji Kodi huko Spain na kuhukumiwa Kufungwa Jela Miezi 21 na kulipa Faini ya Euro Milioni 1.7 lakini Kifungo hicho kikasitishwa.

Mchezaji mwingine wa Barcelona aliekumbwa na balaa kama hilo ni Javier Mascherano ambae nae alihukumiwa Jela Miezi 12 na Kifungo hicho kusitishwa.

Lakini inahofiwa kuwa kutokana na Adhabu kali ambayo Waendesha Mashitaka wanayotaka kwa Eto’o, ipo hatari kubwa Mwafrika huyo akatupwa Jela akipatikana na Hatia tofauti na yaliyowakuta Waargentina Messi na Mascherano au ambayo yatamkuta Mbrazil Neymar.

 

WAENDESHA MASHITAKA SPAIN WATAKA NEYMAR AFUNGWE MIAKA 2!

BARCA-NEYMAR-NEW-CONTRACTWAENDESHA MASHITAKA huko Spain wanataka Fowadi wa Barcelona afungwe Miaka Miwili Jela kuhusiana na Kesi inayodai kulikuwepo na udanganyifu wakati wa Uhamisho wake kutoka Santos ya Brazil kuhamia Barcelona.

Mbali ya Kifungo hicho, Waendesha Mashitaka hao wanataka pia Neymar apigwe Faini ya Euro Milioni 10.

Awali Mahakama huko Spain chini ya Jaji Jose de la Mata iliitupa Kesi hiyo ikidai ni ya Madai na si Uhalifu lakini mapema Mwezi huu ilifufuliwa tena baada ya Waendesha Mashitaka kukata Rufaa na kushinda.

Jaji wa Mahakama huko Nchini Spain, aliamua Neymar inabidi atinge Mahakamani kujibu tuhuma za udanganyifu ikiwa ni Miezi kadhaa baada ya Kesi hiyo kutupwa nje ya Mahakama.

Kesi hii ilifunguliwa tena kwa shinikizo la Kampuni ya Brazil, DIS, wakidai kudhulumiwa katika Uhamisho wa Mchezaji huyo Mwaka 2013 wa kutoka Santos kwenda Barcelona.

Mbali ya Neymar, wengine ambao waliokabiliwa na Mashitaka hayo ni Baba yake Mzazi pamoja na Rais wa Barcelona, Sandro Rosell, na Rais wa Klabu ya Santos, Odilo Rodrigues.

Mashitaka hayo yanahusishwa na Udanganyifu na Rushwa kwa madai kuwa Fedha halisi za Uhamisho wa Neymar zilifichwa ili kuidhulumu Kampuni ya Brazil, DIS, ambayo pia ilikuwa ikimiliki Haki za Kibiashara za Neymar kwa pamoja na Familia ya Neymar na Klabu ya Brazil Santos.

Hivi sasa Waendesha Mashitaka wametaka Baba Mzazi wa Neymar apate Adhabu kama Mwanawe pamoja na Sandro Rosell ambae wametaka afungwe Miaka Mitatu zaidi lakini wameiomba Mahakama imwachie huru Rais wa sasa wa Barca Josep Maria Bartomeu.

+++++++++++++++++++++

CHIMBUKO:

-Mwaka 2013, Barcelona walitangaza kuwa Ada ya Uhamisho ya Neymar kutoka Santos ya Brazil kwenda Barcelona ilikuwa Euro Milioni 57.1 huku Euro Milioni 40 akilipwa Neymar na Familia yake na Santos kupokea Euro Milioni 17.1 ambapo kati ya hizo Euro Milioni 6.8 zililipwa kwa Kampuni ya DIS iliyomiliki Asilimia 40 ya Haki za Kibiashara za Neymar

-Madai yakaibuka kuwa Ada halisi ni Euro Milioni 83.

+++++++++++++++++++++

Tayari Barcelona ilishahukumiwa kulipa Euro Milioni 5.5 ikiwa ni Ukwepaji Kodi kwenye Uhamisho huo wa Mwaka 2013 wa Neymar.

Tangu atue Nou Camp Mwaka 2013, Neymar ametwaa Ubingwa wa La Liga mara 2, Copa del Rey 2, UEFA CHAMPIONZ LIGI, UEFA Super Cup, Spain Super Cup na FIFA Kombe la Dunia kwa Klabu.

Mwezi Oktoba, Neymar alisaini Mkataba Mpya wa Miaka Mitano na Barcelona.

Waendesha Mashitaka wa Kesi hii ya sasa wamepewa Siku 10 na Mahakama kukamilisha taratibu za Kesi kuanza kusikilizwa.