LA LIGA MBIO TAKATIFU KUELEKEA UBINGWA: REAL MADRID & BARCELONA VITANI!

LALIGA-2017-MBIOReal Madrid na Barcelona wapo kwenye 'Mbio Takatifu' wakishindana kuwa Mabingwa wa La Liga Msimu huu.

Timu zote 2 zipo kileleni zikifungana kwa Pointi 84 kila mmoja lakini Real wana faida ya Mechi 1 mkononi.

Katika Wiki 2 zijazo Bingwa wa Spain na Timu zitakazoshushwa Daraja kutoka La Liga zitapatikana.

Gemu ambayo ipo mkononi mwa Real ni.ile ya Ugenini na Celta Vigo ambayo wataicheza Jumatano Mei 17.
Mechi walizobakisha Barca ni ile ya Ugenini na Las Palmas na kisha Nyumbani na Eibar.

Real bado kucheza na Celta Vigo Ugenini na kisha Nyumbani na Sevilla na kumalizia Ugenini na Malaga.
Washiriki wa UEFA CHAMPIONZ LIGI tayari Watatu washapatikana ambao ni Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid wakati Sevilla wakihitaji Pointi 1 tu kuungana nao na kuwakata maini Villareal.LALIGA-MEI10

Timu 2 ambazo zitaiwakilisha Spain kwenye UEFA EUROPA LIGI zitatoka kati ya Villareal, Athletic Bilbao na Real Sociedad.

Lakini huenda Timu zote hizo zikacheza Mashindano hayo ikiwa Barcelona wataifunga Alaves kwenye Fainali ya Copa del Rey.

Vita ya Kushuka Daraja
Tayari Osasuna na Granada zishateremka Daraja wakati Sporting Gijon wako mashakani.

Sporting wanaweza kujinusuru wakishinda Mechi zao 2 zilizobaki na kuacha balaa kwa Deportivo La Coruna na Leganes.

LA LIGA 

Ratiba

Raundi ya 37

 **Saa za Bongo

Jumamosi Mei 13

17:00 Espanyol v Valencia 

17:30 Osasuna v Granada 

Jumapili Mei 14
17:00 Alaves v Celta Vigo 

21:00 Athletic Club v Leganes 
21:00 Real Betis v Atletico Madrid 
21:00 Eibar v Sporting Gijon 
21:00 Las Palmas v Barcelona 
21:00 Real Madrid v Sevilla 
21:00 Real Sociedad v Malaga 
21:00 Villarreal v Deportivo 

Jumatano Mei 17
22:00 Celta Vigo v Real Madrid 

Raundi ya 38 – Mechi za Mwisho
Ijumaa Mei 19
21:45 Granada v Espanyol 

Jumamosi Mei 20
18:00 Deportivo v Las Palmas 

18:00 Sporting Gijon v Real Betis 
18:00 Leganes v Alaves 

Jumapili Mei 21
17:45 Atletico Madrid v Athletic Club 

17:45 Celta Vigo v Real Sociedad 
17:45 Sevilla v Osasuna 
17:45 Valencia v Villarreal 
21:00 Barcelona v Eibar 
21:00 Malaga v Real Madrid 

LA LIGA: REAL BILA RONALDO, MASTAA KIBAO YAWASHA 4 NA KUISHIKA BARCA KILELENI!

LALIGA-2017-MBIOBAO mbili mbili za Alvaro Morata na James Rodriguez zimewapa Real Madrid ushindi wa 4-0 walipocheza na Granada Ugenini huko Estadio Los Carmenes na kuifikia kwa Barcelona wanaoongoza La Liga.
Hata hivyo, Real wanayo Mechi 1 mkononi wakibakiza Mechi 23 na Barca 2.
Bao zote za Real zilifungwa Kipindi cha Kwanza na James Rodriguez Dakika za 3 na 11 na Alvaro Morata Dakika za 30 na 35.
Kikosi cha Real chini ya Kocha Zinedine Zidane kilikuwa bila ya Cristiano Ronaldo na wengine wakibakizwa Sergio Ramos na Casemiro toka kile Kikosi ambacho Majuzi kiliibandika Atletico Madrid 3-0 kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Real watarudiana na Atletico huko Vicente Calderon Jumatano ijayo.
Mapema Jana Barca iliichapa Villareal 4-1 kwa Bao za Neymar, Lionel Messi, Bao 2 moja la Penati, na Luis Suarez.
Bao la Villareal lilifungwa na Cedric Bukambu.

 

WAJUE CELTA VIGO - KIZINGITI CHA LEO CHA MAN UNITED KUTUA FAINALI ULAYA!

Celta Vigo v Manchester United
UWANJA: Estadio Balaidos 
TAREHE: Alhamisi, 4 Mei Kuanza: 22:05 Saa za Bongo
×××××××××××××××××××××××
celta-vigoChini ya Meneja Jose Mourinho, Manchester United wamesonga vizuri kwenye Mashindano ya UEFA EUROPA LIGI Msimu huu, Kombe pekee ambalo hawajawahi kulitwaa Ulaya,  na sasa kizuizi kikubwa kwao kutinga Fainali ni Klabu ya Spain Celta Vigo.
Licha Klabu za Spain, wakiwemo Sevilla waliotwaa Kombe hili mfululizo mara 3 kwa Misimu Mitatu iliyopita, kulitwaa Kombe hili mara 10, Celta Vigo hawajawahi kutinga Nusu Fainali ya Mashindano haya.
CELTA VIGO NI NANI?
Celta Vigo ipo Mji mdogo uitwao Vigo wenye Wakazi 200,000 ambao upo Kaskazini Magharibi ya Spain ukipakana na Nchi ya Portugal.
Klabu hii imekuwa ikiranda kwenye Madaraja Mawili ya juu huko Spain na kuanzia Miaka ya 2000 kupata mafanikio na kutua La Liga wakati walipokuwa na Wachezaji kama vile Alexander Mostovoi, Valery Karpin na Staa wa baadae wa Chelsea Claude Makelele na kumudu kushika Nafasi ya 4 ya La Liga Mwaka 2003.
Lakini wakaporomoka tena na kushuka Daraja la Pili na kukaa huko kwa Miaka Mitano kabla kurejea La Liga Mwaka 2012.
Celta Vigo hawajawahi kutwaa Taji lolite licha kufika Nusu Fainali za Copa del Rey mara 2 katika Misimu Miwili iliyopita.
Celta wapo chini ya Kocha kutoka Argentina Eduardo Berizzo na Msimu huu wapo Nafasi ya 11 kwenye La Liga ambayo waliichapa Barcelona 4-3 Mwezi Oktoba.
Celta hutumia Mfumo wa 4-2-3-1 ambao huongozwa na Mafowadi Iago Aspas, Miaka 29 kutoka Spain, na John Guidetti, Miaka 25 kutoka Sweden.
Aspas ni Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Guidetti aliwahi kuichezea Man City huku wote wakipwaya kwenye Timu hizo.
Mastaa wengine wa Celta ni Winga kutoka Denmark Pione Sisto ambae aliifungia Timu yake Midtjylland walipicheza na Man United kwenye Mashindano haya Msimu uliopita.
Mwingine Nyota wa Celta ni Mbelgiji wa Miaka 21 Theo Bongonda lakini msukaji mkubwa wa Timu hii ni Mchezaji mwingine toka Denmark Daniel Wass ambae ni Kiungo Mshambuliaji.
Nguvu kubwa ya Celta Vigo pembezoni mwa Uwanja ni Mafulbeki wao wanaopanda na kushuka Jonny Castro na Hugo Mallo.
Man United lazima wachukue tahadhari kwani Timu hii imeilaza Barcelona mara 3 ikiwemo vipigo vya 4-1 na 4-3 kwenye Uwanja wa Leo Estadio Balaidos.
Pia Msimu huu Celta wameitupa nje ya Copa del Rey Real Madrid baada ya kuichapa 2-1 huko Bernabeu na kutoka Sare 2-2 hapo Estadio Balaidos.

MAN UNITED - KIKOSI KILICHOENDA SPAIN:

David de Gea, Joel Pereira, Sergio Romero

Antonio Valencia, Matteo Darmian, Axel Tuanzebe, Eric Bailly, Chris Smalling, Phil Jones, Daley Blind

Michael Carrick, Jesse Lingard, Marouane Fellaini, Paul Pogba, Ander Herrera, Ashley Young, Juan Mata, Henrikh Mkhitaryan

Wayne Rooney, Anthony Martial, Marcus Rashford

REFA: Sergei Karasev (Russia)

UEFA EUROPA LIGI

Nusu Fainali – Mechi za Marudiano

**Saa za Bongo

Alhamisi Mei 11

2205 Manchester United v Celta Vigo

2205 Olympique Lyonnais v Ajax Amsterdam [1-4]

Tarehe Muhimu:

04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

FAINALI

24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden

UEFA CHAMPIONZ LIGI: JUMANNE NI DABI EL MADRILENO SANTIAGO BERNABEU, REALMADRID v ATLETICO MADRID!

>PATA UNDANI!

UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI

UCL-SF-REAL-ATLETINusu Fainali – Mechi za Kwanza

**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo

Jumanne Mei 2

Real Madrid v Atletico Madrid

Jumatano Mei 3

AS Monaco v Juventus

++++++++++++++++

Jumanne Usiku Estadio Santiago Bernabéu Jijini Madrid Nchini ndio dimba la Nusu Fainali ya Kwanza ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kati ya Mahasimu wakuu wa Mji huo Real Madrid na Atletico Madrid, Mechi ambayo ikikutanisha Timu hizi hubatizwa El Derbi Madrileno.

Hii ni mara ya 5 kwa Timu hizi kupambana katika Mechi za Ulaya na Real Madrid walimaliza ndoto za Atlético Madrid kwenye UCL katika Misimu Mitatu iliyopita, ikiwa ni pamoja wa Fainali za Mwaka 2014 na 2016.

+++++++

JE WAJUA?

-Real na Atletico zimekutana Mechi 204 za La Liga na Makombe ya Spain na Real kushinda 103, Atletico 51 na Sare 50.

-Lakini tangu 2014 walipofungwa Fainali ya UCL, Atletico wamefungwa Mechi 1 tu kati ya 10 za Mashindano ya kwao Spain dhidi ya Real wakishinda 5 na Sare 4.

-Mechi pekee waliyofungwa na Real ni ya Msimu huu wa La Liga walipopigwa 3-0 walipokuwa kwao Vicente Calderon kwa Hetitriki ya Cristiano Ronaldo hapo 19 Novemba 2016.

-Marudiano ya La Liga hapo 8 Aprili 2017, Real na Atletico zilitoka 1-1 kwa Bao za Pepe na Griezmann.

+++++++
Mwaka Jana Vigogo hawa wa Spain walikutana kwenye Fainali ya UCL huko Milan, Italy na Sergio Ramos kuipa Bao Real Dakika ya 15 na Atletico kusawazisha Dakika ya 89 kupitia Yannick Carrasco baada ya Antoine Griezmann kukosa Penati Dakika ya 48.

Fainali hiyo ikabaki Sare ya 1-1 hadi Dakika za Nyongeza 30 kumalizika na Penati Tano Tano kupigwa.

Real walifunga Penati zao kupitia Lucas Vázquez, Marcelo, Bale na Ramos wakati Atletico kufunga kupitia Griezmann, Gabi na Saúl Ñíguez huku Juanfran akipiga Posti Penati yao ya 4 na kumwacha Cristiano Ronaldo akiipigia Real Penati ya 5 na kufunga na kuwapa Kombe Real.

KWENYE MECHI HIYO ILIYOCHEZWA SAN SIRO HAPO 28 MEI 2016, VIKOSI VILIKUWA:
REAL MADRID:
Navas, Carvajal (Danilo 52), Ramos, Pepe, Marcelo, Casemiro, Kroos (Isco 72), Modrić, Bale, Benzema (Lucas Vázquez 77), Ronaldo.
ATLÉTICO MADRID: Oblak, Juanfran, Godín, Savić, Filipe Luís (Lucas Hernández 109), Gabi, Augusto Fernández (Carrasco 46), Koke (Partey 116), Saúl, Griezmann, F Torres.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

TAREHE MUHIMU:

MECHI ZA MTOANO:

02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

LA LIGA: BARCA, REAL ZAKABANA KILELENI!

LALIGA-2017-MBIO-1BARCELONA na Real Madrid zimeendelea kushinda na kufungana kwa Pointi kileleni mwa La Liga lakini Real wana lulu ya Mechi 1 mkononi.
Mapema Jana Real Madrid walizoa ushindi mwishoni walipoibwaga Valencia huko Santiago Bernabeu wakati Bao 2 za Luis Suarez zikiisaidia Barcelona kuibwaga Espanyol katika Dabi ya Catalunya huko Mjini Barcelona.
Huko Bernabeu, Cristiano Ronaldo aliipati Real Bao Dakika ya 27 alipounganisha kwa Kichwa Krosi ya Dani Carvajal lakini Kipindi cha Pili alikosa kufunga Bao la Pili wakati Penati yake ilipookolewa na Kipa Diego Alves.
Dani Parejo akaisawazishia Valencia Dakika ya 82 kwa Frikiki lakini Dakika 4 baadae Marcelo akafunga Bao la Pili na kuipa Real ushindi wa 2-1.
Nao Barca wametwaa uongozi wa La Liga mbele ya Real baada kuichapa Espanyol 3-0 kwa Bao 2 za Luis Suarez na 1 la Ivan Rakitic.
Atletico Madrid wameichapa Las Palmas 5-0 na kujichimbia Nafasi ya 3 kwenye La Liga.
Bao za Atletico zilifungwa na Kevin Gameiro, Bao 2, Saul, Thomas Parteyna Fernando Torres.
Tony Adams, Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Jana alishuhudia Timu yake Granada ambayo yeye ndie Kocha wa muda ikiungana na Osasuna kuwa Timu ya Pili kushuka Daraja walipifungwa 2-1 na Real Sociedad.

Habari MotoMotoZ