BARCA KUMPA NEYMAR MKATABA NA DAU JIPYA AMKARIBIE MESSI!

NEYMAR-SHANGILIAvPSGRais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu, ambae ametangaza nia ya kugombea tena wadhifa huo Klabuni hapo Mwezi ujao katika Uchaguzi wao, ameahidi kuwa endapo atashinda ataongeza na kuuboresha Mkataba wa Nahodha wa Brazil Neymar.

Bartomeu amesema atamwongezea Neymar Miaka Miwili kwenye Mkataba ili abakie Nou Camp hadi 2020 na pia ataongezewa kipato ili amkaribie Lionel Messi na pia awe sawa na Nahodha wa Klabu hiyo Andres Iniesta.

Pato la Neymar linatarajiwa kufikia Pauni Milioni 8.5 sawa na Iniesta wakati Messi anazoa Pauni Milioni 14.5 kwa Mwaka.

Pia Bartomeu ameahidi kuwa Mkataba mpya wa Neymar utakuwa na Kipengele kinachotaka Klabu yeyote ya inayotaka kumchukua wakati hajamaliza Mkataba na Barca ilipe Pauni Milioni 180 ndio aachiwe kuhama.

Hivi sasa Rais huyo na Klabu hiyo wameshitakiwa Mahakamani huko Spain kwa kukwepa kulipa Kodi stahiki ya Pauni Milioni 9.5 walipomnunua Neymar kutoka Klabu ya Brazil Santos.

Msimu uliopita Neymar aliifungia Barca Bao 39 na Juzi Neymar alipachika Bao lake la 44 kwa Nchi yake Brazil akifunga tela nyuma ya Wafungaji Bora wa Nchi hiyo Pele mwenye Bao 77, Romario 62, Ronaldo 55 na Zico 48.

UTATA WA KOCHA LUIS ENRIQU BARCA!

LUISENRIQUEUle utata wa hatima ya Kocha Luis Enrique kubakia FC Barcelona sasa umekwisha baada ya kusaini nyongeza kwenye Mkataba wake.

Katika Msimu wake wa kwanza tu na Barca, Enrique alimudu kutwaa Trebo baada kubeba Ubingwa wa Spain La Liga, Copa del Rey na juzi kuzoa Kombe la Ubingwa Ulaya, UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Lakini licha ya mafanikio hayo ilizigaa imani kubwa ataondolewa.

Lakini kwa kusaini nyongeza ya Mkataba itakayomweka Barca hadi mwishoni mwa Msimu wa 2016/17,  utata huo sasa umekwisha.

Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, ndie alietangaza kuongezewa Mkataba Enrique.

Enrique, ambae aliwahi kuzichezea Barca na Real Madrid, aliteuliwa Mwaka jana kumbadili Tata Martino ambae sasa ni Kocha wa Argentina.

KAZOA TREBO LAKINI LUIS ENRIQUE HAJIJUI BARCA!

LUISENRIQUEKocha wa Barcelona Luis Enrique Jana alifanikiwa kutwaa Kombe la 3 katika Msimu wake wa kwanza tu baada ya kuichapa Juventus Bao 3-1 katika Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Berlin, Germany.

Lakini, kwa muda mwingi Nou Camp inekuwa ikigubikwa na uvumi mzito wa kufukuzwa kwa Luis Enrique ambae ni Mchezaji wa zamani wa Barca na pia Kocha wa zamani wa Timu B.

Na Jana, mara baada ya Barca kuzoa Ubingwa wa Ulaya, Luis Enrique, mwenye Miaka 45, alibanwa ili afafanue nini hatima yake kufuatia minong'ono hiyo mikubwa.

Enrique alisema: "Sijui. Lakini nafurahia wakati huu. Changamoto yangu wakati huu ni kufurahi na kupata mapumziko mazuri ya wakati wa Kiangazi!"

Enrique pia alitoboa kuwa wakati wa uamuzi utafika tu.

Alizungumza: "Sijali wanaoniponda. Tumefungwa Mechi 6 na Sare 4 katika Mechi 60 na huu ni moja ya Misimu bora kwa Barca! Bila shaka Barca ndio Klabu bora Ulaya katika Miaka 10 iliyopita!"

Nae Kiungo mkongwe wa Barca, Andrea Iniesta, alipohojiwa kuhusu hatima ya Enrique alijibu: "Yeye ni Kocha na Kiongozi wetu na tunatumai atakuwepo Mwakani. Hajasema lolote kama sivyo!"

CHICHARITO AJIPIGIA 'NDOGONDOGO' KWA MENEJA MPYA REAL!!

maxresdefaultStraika wa Manchester United Javier Hernandez 'Chicharito' amekiri kuwa hajui kama atarejea tena Real Madrid Msimu ujao lakini amesifu uteuzi wa Vigogo hao wa Spain wa kumchukua Rafa Benitez kama Meneja wao mpya.
Benitez aliteuliwa Majuzi kushika nafasi ya Carlo Ancelotti ambae alitimuliwa mara baada ya Msimu wa La Liga kumalizika na Timu hiyo kushika Nafasi ya Pili.
Chicharito, mwenye Miaka 27, alionekana hahitajika huko Old Trafford mara baada ya kuanza kazi kwa Meneja mpya Louis van Gaal mwanzoni mwa Msimu uliopita na kuruhusiwa kwenda kwa Mkopo Real. 
Akiwa huko Santiago Bernabeu, Chicharito alianza kwa kusuasua lakini mwishoni mwa Msimu alianza kung'ara na kupiga Bao mfululizo, Bao 6 katika Mechi zake 6 za mwisho.
Lakini kutimuliwa kwa Kocha Carlo Ancelotti kumemuacha Chicharito njia panda na mwenyewe hajui wapi atacheza Msimu ujao kama ni kurudi Old Trafford, kubakia Bernabeu, kwa Mkopo au kudumu, au kwenda kwingineko.
Amesema: "Sijui nitakuwa wapi, United, Madrid au kwingineko, nipo vakesheni sasa. Sasa yupo Benitez na hawezi kuongea na mimi kwa vile nilikuwa kwa Mkopo. Lakini nadhani Rafa ananijua. Ni Kocha mzuri na nadhani atafanya kazi njema Real!"
 
 
 

OLYMPIASTADION-BERLIN: LEO NI JUKWAA MURUA KWA LIONEL MESSI!

MESSIMwaka 2014 haukuwa mwema kwa Nahodha wa Argentina na Staa wa FC Barcelona, Lionel Messi.
Kwa mara ya kwanza katika Miaka 6 Messi alitoka bila Kombe lolote na Klabu yake Barcelona na lile tegemeo kwamba ataiwezesha Argentina kutwaa Kombe la Dunia huko Brazil kupotea bila mafanikio.
Matokeo hayo yaliwafanya wengi kuamini kuwa Messi, ambae alikuwa ndie Mtu wa Kwanza kuzoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa mara 4 mfululizo kuanzia 2008 hadi 2012, sasa amekwisha.
Lakini Mwaka mmoja baadae, baada ya kuanza kwa kusuasua na hata kuzozana na Kocha wa Barca, Luis Enrique, Messi, katika Miezi 6 iliyopita amekuwa moto.
Messi ameiinua Barca na kuibebesha Mataji Mawili, yale ya La Liga na Copa del Rey, na Leo ana nafasi kubwa kuwapa Kombe la 3 la UEFA CHAMPIONZ LIGI ikiwa wataifunga Juventus huko Olympiastadion Jijini Berlin Nchini Germany.
Hata mwenyewe Messi amekiri kuhusu 2014 kwa kusema: "Ni Mwaka ambao nataka kuusahau. Nilikuwa nje kwa maumivu na kukosa Mechi nyingi. Niliporejea sikujisikia vyema." 
Inaaminika moja ya sababu ya kubadilika kwa Messi, mwenye Miaka 27, ni kumpata Mtaalam wa Lishe, Giuliano Poser, kutoka Italy ambae   alimfanya apunguze uzito kwa Kilo 3.5 tangu wawe pamoja na kumfanya awe fiti zaidi na mwepesi zaidi.
Hivi sasa Messi ameonyesha tena ule umahiri wake wa kulipuka kwa kasi na kutambuka Mabeki kwa spidi kali kama alivyoonyesha kwenye Fainali ya Copa del Rey alipowachomoka Mabeki Wanne na kufunga Bao safi sana ambalo litabaki katika historia.
Je Usiku huu huko Germany, Lionel Messi ataonyesha maajabu?