LEO USIKU BARCA KUFUNGA MWAKA BILA MSN, MESSI, SUAREZ, NEYMAR WAPO LIKIZO!

BARCA-MESSI-SUAMABINGWA wa Spain FC Barcelona Leo watatinga Uwanjani kwao Nou Camp kucheza Mechi yao ya mwisho kwa Mwaka 2016 bila ya Nyota wao Watatu, maarufu kama MSN, ambao wamepewa Likizo ya Mapema.
Baada ya Mechi hizi za Leo Soka la Spain linakwenda mapumziko ya Krismas na Mwaka Mpya na kurejea baada ya Wiki ya Kwanza ya Januari.
Lakini Kocha wa Barca Luis Enrique ameamua Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, ambao ndio hao MSN, pamoja na Gerrard Pique hawahitajiki kwa Mechi yao ya Leo na kuwaruhusu kwenda tangu walipomaliza Mechi yao ya Wikiendi walipoinyuka Espanyol 4-1.
Leo Barca wanarudiana na Timu ya Daraja la chini Hercules CF katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya Copa del Rey ambalo ni Kombe la Mfalme wa Spain.
Katika Mechi ya kwanza Timu hizi zilitoka 1-1.
COPA DEL REY
Raundi ya Mtoano ya Timu 32 - Mechi za Marudiano
Ratiba
**Saa za Bongo
(Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza)
21:00Sevilla FC v Formentera (5:1) 
21:00SD Eibar v Sporting Gijon (2:1)
23:00Osasuna v Granada CF (0:1)
23:00Valencia C.F v CD Leganes (3:1) 
23:00Deportivo La Coruna v Real Betis (0:1)   0:00FC Barcelona v Hercules CF (1-1)

LA LIGA: ‘UCHAWI’ WA MESSI WAIPA BARCA USHINDI DABI YAO NA ESPANYOL!

MESSI-ESPANYOLLuis Suarez alipiga Bao 2 wakati Barcelona ikiwachapa Mahasimu wao Espanyol 4-1 katika Dabi yao na kupanda hadi Nafasi ya Pili kwenye La Liga.

Suarez ndie aliefunga Bao za Kwanza Dakika za 18 na 67 na kisha Jordi Alba kufunga Bao la 3 Dakika ya 68 wakatiDavid Lopez akiipa Espanyol Bao lao pekee Dakika ya 79.

Messi, ambae aling’ara mno, alionyesha miujiza pale alipowatambuka Mabeki Wanne wa Espanyol na kumpasia Suarez aliefunga Bao la Pili na kisha Dakika 1 baadae kurudia uchawi huo huo kwa kuwapita Mabeki Wanne na kumpa Jordi Alba aliepiga Bao la 3.

Messi ndie aliefunga Bao la 4 la Barca katika Dakika ya 90.

Matokeo haya yamewaacha Barca Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Real Madrid ambao wamecheza Mechi 1 pungufu kwa vile walikuwa huko Japan ambako Jana walitwaa Kombe la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.

Baada ya Mechi ya Leo Usiku, La Liga itaenda Mapumzikoni hadi Januari 6.

VIKOSI:

BARCELONA (Mfumo 4-3-3): Ter Stegen; Sergi Roberto, Pique, Mascherano, Alba; Denis Suarez, Iniesta, Busquets; Messi, Suarez, Neymar

Akiba: Rakitic, Turan, Rafinha, Cillessen, Alcacer, Digne, Umtiti.

ESPANYOL (Mfumo 4-4-2): Diego Lopez; Javi Lopez, David Lopez, Reyes, Martin; Piatti, Fuego, Diop, Jurado; Caicedo, Moreno

Akiba: Jimenez, Ruben, Duarte, Reyes, Vazquez, Roca, Melendo

REFA: Antonio Miguel Mateu Lahoz

LA LIGA

Ratiba:

Jumatatu Desemba 19

2245 Athletic Bilbao v Celta Vigo

Januari 6

Espanyol v Deportivo La Curuna

Januari 7

Real Madrid v Granada

SD Eibar v Atletico Madrid

Celta Vigo v Malaga

Real Sociedad v Sevilla

Januari 8

Athletic Bilbao v Alaves

Real Betis v Leganes

Las Palmas v Sporting Gijon

Villarreal v FC Barcelona

HATIMAE MESSI AKUTANA NA MTOTO WA AFGHANISTAN ALIEPATA UMAARUFU DUNIANI KWA KUVAA JEZI YA MFUKO WA PLASTIKI WA STAA HUYO!

MESSI-MTOTO-AFGHAN-MEETMWEZI Januari, mwanzoni mwa Mwaka huu, Dunia ilipata mtikisiko pale Mtoto mdogo toka Nchi yenye shida kubwa na balaa kubwa ya Vita, Afghanistan, aliponaswa kwenye Picha akiwa amevaa Jezi iliyotengenezwa kwa Mfuko wa Plastiki na kuandikwa kwa Mkono Mgongoni Namba 10 na Jina la Messi.

Picha hiyo ikarindima Mitandaoni na kila Gazeti Duniani kote ikimuonyesha Murtaza Ahmadi, mwenye Miaka 6, akiwa na Jezi hiyo ambayo mwenyewe alikiri Lionel Messi, Staa wa FC Barcelona kutoka Argentina, ni kipenzi chake.

Baada ya hapo Mtoto huyo alipelekewa Jezi halisi na Zawadi nyingine toka kwa Messi.

Lakini umaarufu huo wa Murtaza Ahmadi ukaibua hatari kubwa kwa Mtoto huyo na Familia yake na wakalazimika kuikimbia Nchi yao Afghanistan ambako walikuwa wakiishi Jimbo la Ghazni, Wilaya ya Jaghori na kukimbilia Pakistan.

Hii Leo, Mjini Doha, Qatar, Mtoto Murtaza amekutana uso kwa uso na kipenzi chake Lionel Messi na Staa huyo kumbeba Mtoto huyo kwa furaha.

Messi ametua Qatar na Timu yake Barcelona kucheza Mechi ya Kirafiki na Klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia baadae Leo.

Kukutana kwa Messi na Murtaza kumetangazwa na Kamati ya Matayarisho ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2022 za Qatar ambao ndio waliandaa safari ya Mtoto huyo kwenda Doha.

LA LIGA: SERGIO RAMOS AIPA USHINDI REAL DAKIKA ZA MAJERUHI!

REAL-RAMOS-KADI21SERGIO RAMOS Jana tena alifunga Bao muhimu katika Dakika za lala salama na kuipa ushindi Real Madrid wa Bao 3-2 walipocheza na Deportivo La Coruna ambao umewafanya wawe juuu kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 6 mbele ya Barcelona.

Mapema Jana, Barca waliichapa Osasuna 3-0.

Jana, Real, wakicheza kwao Santiago Bernabeu bila Cristiana Ronaldo, walikuwa 2-1 nyuma na kusawazisha na kushinda katika Dakika 6 za mwisho kwa Bao za Morata, Dakika ya 50, Mariano, Dakika ya 84 na Ramos Dakika ya 92.

Bao za Deportivo zilifungwa na Joselu Dakika za 63 na 65.   

Ushindi huo pia umeweka Rekodi mpya kwa Klabu ya Real ya kutofungwa katika Mechi 35.

Sasa Real wanaruka kwenda Japan kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Desemba 9

Malaga CF 1 Granada CF 1

Jumamosi Desemba 10

Osasuna 0 FC Barcelona 3

Real Sociedad 3 Valencia C.F 2

Las Palmas 1 CD Leganes 1

Real Madrid CF 3 Deportivo La Coruna 2

Jumapili Desemba 11

1400 SD Eibar v Deportivo Alaves

1815 Celta de Vigo v Sevilla FC

2030 RCD Espanyol v Sporting Gijon

2245 Real Betis v Athletic de Bilbao

Jumatatu Desemba 12

2245 Villarreal CF v Atletico de Madrid

LA LIGA: BARCA WAICHAPA TIMU YA MKIANI OSASUNA NA KUWAKARIBIA VINARA REAL!

MESSI-SHANGILIA-BARCAWAKICHEZA Ugenini huko Estadio El Sadar, Mjini Pamplona huko Nchini Spain. Mabingwa Watetezi wa La Liga FC Barcelona walibanwa 0-0 hadi Haftaimu lakini Kipindi cha Pili kuibuka kidedea kwa kuitwanga Osasuna Bao 3-0.

Matokeo haya yamewaweka Barca wawe Pointi 3 tu nyuma ya Vinara Real Madrid ambao baadae Leo wako kwao Santiago Bernabeu kucheza na Deportivo La Coruna.
Bao la kwanza la Barca lilifungwa Dakika ya 59 na Luis Suarez kufuatia ushirikiano wa Lionel Messi, Jordi Alba na kisha kupasiwa Mfungaji.

Bao la Pili alifunga Messi Dakika ya 72 kupitia Messi ambaye pia alipiga Bao la 3 kwenye Dakika ya 92.

Matokeo haya yamezidi kuwachimbia Osasuna mkiani mwa Msimamo wa La Liga.

VIKOSI:

Osasuna (Mfumo 4-4-2): Nauzet; Oier, Miguel Flano, Ivan Marquez, Clerc; Berenguer, De Las Cuevas, Causic, Torres; Sergio Leon, Riera

Osasuna substitutes: Mario, Bonnin, D. Garcia, Riviere, U. Garcia, Fuentes, Kenan.

Barcelona (Mfumo 4-3-3): Ter Stegen; Sergi Roberto, Pique, Umtiti, Alba; Andre Gomes, Busquets, Iniesta; Messi, Suarez, Arda

Barcelona substitutes: Rakitic, Denis, Rafinha, Cillessen, Mascherano, Alcacer, Digne.

REFA: Juan Martínez Munuera

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Desemba 9

Malaga CF 1 Granada CF 1

Jumamosi Desemba 10

Osasuna 0 FC Barcelona 3

1815 Real Sociedad v Valencia C.F

2030 Las Palmas v CD Leganes

2245 Real Madrid CF v Deportivo La Coruna

Jumapili Desemba 11

1400 SD Eibar v Deportivo Alaves

1815 Celta de Vigo v Sevilla FC

2030 RCD Espanyol v Sporting Gijon

2245 Real Betis v Athletic de Bilbao

Jumatatu Desemba 12

2245 Villarreal CF v Atletico de Madrid