BARCELONA: ERNESTO VALVERDE KOCHA MKUU MPYA KUMBADILI LUIS ENRIQUE!

BARCA-VALVERDEBarcelona imemteua Ernesto Valverde kuwa Kocha Mkuu wao Mpya kwa Mkataba wa Miaka Miwili wenye Nyongeza ya Mwaka Mmoja juu yake.

Valverde, mwenye Miaka 53, alikuwa Fowadi wa zamani wa Barca aliechezea Klabu hiyo kwa Misimu Miwili kuanzia 1988 na kufunga Bao 8 katika Mwchi 22 akiandamwa na Majeruhi.

Kocha huyo ametokea Athletic Bilbao alikokuwa Kocha Mkuu na kujiuzulu Wiki iliyopita na sasa anambadili Luis Enrique ambae amemaliza Mkataba wake wa Miaka Mitatu na kuiweka Barca Nafasi ya Pili kwenye La Liga wakiwa nyuma ya Mabingwa Real Madrid.

Kwenye Msimu wake wa kwanza, Enrique alitwaa Trebo, wa pili akibeba Dabo na huu wa mwisho Copa del Rey tu.

Akitangaza ujio wa Ernesto Valverde ambae atatambulishwa rasmi Alhamisi, Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, alimsifia Valverded na kudai anakuza Vijana na anacheza staili ya Barcelona.

Wachambuzi wamedai kazi kubwa kwa Valverde hivi sasa ni kuiweka Timu icheze Kitimu badala ya kumtegenea Lionel Messi na pia kuimarisha Difensi yao ambayo Msimu huu kwenye Tripu zao za Ugenini kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Juventus, PSG na Manchester City ilibamizwa Bao 10.

ERNESTO VALVERDE - Historia ya Ukocha

BAADA kustaafu Uchezaji Mwaka 1997, alijiunga na Athletic Bilbao kama Kocha wa Timu ya Vijana na Msimu wa 2003/04 kuwa Kocha wa Timu ya Kwanza ambako aliiongoza Timu kushika Nafasi za 5 na 5 kwenye La Liga.

Mwaka Mmoja baadae akatua Espanyol na kuifikisha Fainali ya UEFA CUP na kisha kwenda Ugiriki kuiongoza Olympiacos na kuiwezesha kutwaa Ubingwa na Kombe la FA.

Baada Mwaka Mmoja, Valcerde akatua Valencia na kisha kurudi tena Olympiacos na kukaa Miaka Miwili na kutwaa Ubingwa mara 2 na Kombe la FA na kisha kurudi Valencia Mwaka 2013 ambayo aliiweka Nafasi ya 4 kwenye La Liga huku akitinga 7 za juu mara 3 kwa Misimu iliyofuatia na Msimu huu kumaliza Nafasi ya 7.

Msimu wa 2014/15 walimudu kufika Fainali ya Copa del Rey na kuibwaga Barcelona Jumla ya Mabao 5-1 kwa Mechi 2 za kugombea 2015 Spanish Super Cup.

COPA DEL REY: MESSI, NEYMAR, ALCACER WAIPA KOMBE BARCA!

COPAREY17BARCELONA Jana waliipiga Alaves Bao 3-1 kwenye Fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey na kujipa ahueni baada Wiki iliyopita kushindwa kuutetea Ubingwa wao wa La Liga ulioenda kwa Mahasimu wao Real Madrid.
Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa Barca kutwaa Kombe hili.
Fainali hii ilichezwa huko Vicente Calderon Jijini Madrid na ndio Mechi ya mwisho kabisa kwa Kocha wa Barca Luis Enrique ambae anaondoka Klabuni hapo.
Bao zote za Mechi hiyo zilifungwa Kipindi cha Kwanza.
Barca walitangulia kufunga Dakika ya 30 kupitia Lionel Messi na Alaves kusawazisha kwa Frikiki ya Theo Hernandez Dakika ya 33.
Barca walipiga Bao 2 za chapchap Dakika za 45 na 48 kupitia Neymar na Alcarer na kwenda Haftaimu 3-1 mbele.

 
 

MESSI: RUFAA YATUPWA, JELA MIEZI 21 PALE PALE!

BARCA-MESSI-SITADHABU ya Kifungo cha Jela cha Miezi 21 alichoshushiwa Mchezaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi itabaki pale pale baada kuthibitishwa na Mahakama ya Rufaa ya Spain.
Hata hivyo, huko Spain, Vifungo vya chini ya Miezi 24 si lazima ukae lupango na badala yake unaweza kupewa Kifungo cha Nje.
Mwaka Jana, Messi na Baba yake Mzazi aitwae Jorge walihukumiwa Jela kwa Kosa la Ukwepaji Kodi wa Euro Milioni 4.1.
Kosa hilo linahusiana na kuanzisha Kampuni feki huko Belize na Uruguay kusimamia Mauzo ya Hatimiliki za Picha na Matangazo yanayomhusu Messi ili kukwepa kulipa Kodi huko Spain.
Kifungo cha Babae Messi, ambae alihukumiwa Miezi 24 Jela, kilipunguzwa hadi Miezi 15 baada ya kulipa Kodi zilizokwepwa.
Kesi hii sasa imerejeshwa Mahajama ya Mjini Barcelona ili kuamua aina ya Adhabu ikiwa ni Jela au Kifungo cha Nje.

REAL MADRID YAMSAINI KINDA MBRAZIL MIAKA16 KWA £39.6 MILIONI!

VINICIUSMABINGWA WAPYA wa Spain Real Madrid wamemsaini Vinícius Júnior kutoka Flamengo ya Brazil kwa Dau la Pauni Milioni 39.6.
Tineja huyo amekichezea Kikosi cha Kwanza cha Flamengo Mechi 1 tu.
Inadaiwa Klabu za Barcelona na Manchester United zilitoa Ofa za Euro Milioni 30 lakini ile ya Euro Milioni 46 ya Real ndio imewini.
Vinícius Júnior alisaini Mkataba Mpya na Flamengo Wiki iliyopita na ndani yake kubadilishwa Kipengele cha Kuuzwa kwake wakati Mkataba ukiwa hai kutoka Euro Milioni 30 hadi 46 ambazo ndizo Real wamelipa.
Dili hii imemfanya Kinda huyu kuwa Mchezaji wa Bei mbaya wa Pili kununuliwa katika Historia ya Brazil baada Neymar kununuliwa na Barcelona kutoka Santos Mwaka 2013 kwa Dau la Euro Milioni 86.
Mara baada Dili ya Kijana huyu kukamilika, Real imetangaza kuwa wataanza kummiliki Mchezaji huyu kuanzia Julai 2018 akitimiza Miaka 18 lakini atabaki Flamengo hadi Julai 2019.
Vinicius ameichezea Timu ya Taifa ya Brazil ya U-17 mara 22 akipachika Bao 19.
Kwenye Ubingwa wa Nchi za Marekani ya Kusini w U-17, Vinicius ndie aliibuka Mchezaji Bora na Mfungaji Bora akipiga Bao 7.

LA LIGA: REAL MADRID MABINGWA, RONALDO AWASETIA UBINGWA WA KWANZA TANGU WA JOSE MOURINHO 2012!!

>ZAMA ZA BARCA KWISHNEI!

JANA, La Liga, ilifikia tamati na Real Madrid kuutwaa Ubingwa baada ya kuichapa Ugenini Malaga 2-0.

Huo na Ubingwa wa Kwanza wa La Liga kwa Real tangu wautwae Mwaka 2012 chini ya Meneja wa sasa wa Manchester United Jose Mourinho.

Pia Real sasa wako njiani kutwaa Dabo, Ubingwa wa Spain na UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa mara ya kwanza katika Miaka 59.

Juni 3, Real wapo huko Cardiff, Wales kucheza na Juventus katika Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Jana, Real walikwenda mbele 1-0 Dakika ya Pili tu baada Krosi tamu ya Isco kumkuta Cristiano Ronaldo aliefunga.

Dakika ya 55 Real walikwenda 2-0 mbele kufuatia Kona ya Toni Kroos kuunganishwa na Sergio Ramos na Kipa Kameni kuokoa na Mpira kumgonga Varane na kudondokea kwa Karim Benzema aliekwamisha Wavuni.

Mara baada ya Mechi hiyo kwisha Jiji la Madrid huko Spain lilizima kwa Shangwe na Mashabiki wa Real kusongana katikati ya Mji kwenye Chemchem ya Cebeles kusheherekea kama ilivyo desturi yao huku Uwanja wa Malaga ukiwa hoihoi.

VIKOSI:

MALAGA: Kameni, Torres, Hernandez, Mikel, Ricca, Camacho, Keko, Recio, Fornals, Jony, Sandro.

REAL MADRID: Navas, Danilo, Varane, Ramos, Marcelo, Casemiro, Modric, Kroos, Isco, Ronaldo, Benzema.

BARCA 4 EIBAR 2

Barcelona Jana walivuliwa Ubingwa na kutwaa Nafasi ya Pili ya La Liga na kuwa Pointi 3 nyuma ya Mabingwa Real Madrid baada ya wao kutoka nyuma 2-0 na kuilaza Eibar 4-2.

Eibar walifunga Bao zao Dakika 7 na 61 kupitia Takashi Inui na Barca kujibu Dakika za 63, 73, 75 na 92 Wafungaji wakiwa Junca, aliejifunga mwenyewe, Luis Suarez na 2 za Lionel Messi ambae pia alikosa Penati na ufunga nyingine.

Bao za Messi zimemfanya azoe Buti ya Dhahabu ya La Liga kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2012/13.

VIKOSI:

BARCELONA: Ter Stegen, Roberto, Umtiti, Marlon, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Messi, Suarez, Neymar.

EIBAR: Yoel, Capa, Lejuene, Arbilla, Junca, Pena, Dani Garcia, Escalante, Inui, Enrich, Kike.

LA LIGA 

Matokeo:

Raundi ya 38 – Mechi za Mwisho
Ijumaa Mei 19
Granada 1 Espanyol 2 

Jumamosi Mei 20
Deportivo 3 Las Palmas 0 
Sporting Gijon 2 Real Betis 2 
Leganes 1 Alaves 1 

Sevilla 5 Osasuna 0
Jumapili Mei 21
Atletico Madrid 3 Athletic Club 1 
Celta Vigo 2 Real Sociedad 2
Valencia 1 Villarreal 4
Barcelona 4 Eibar 2 
Malaga 0 Real Madrid 2 

Habari MotoMotoZ