FLORENTINO PEREZ KUBAKIA RAIS WA REAL MADRID HADI 2021

>FLORENTINO PEREZ ‘AMPA 5’ ZIDANE!

REAL PEREZ ZIDANEMABINGWA wa Spain na Ulaya Real Madrid wataongozwa na Florentino Perez kwa Miaka mingine Minne kama Rais baada ya kutojitokeza kwa Mgombea mwingine kwenye Uchaguzi wa Rais wa Klabu hiyo.

Siku ya mwisho ya Wagombea kujitokeza ilikuwa Jana Jumapili Saa 6 Usiku na hakuna yeyote aliejitokeza kuchuana na Rais wa sasa wa Mabingwa hao.

Hali hiyo inamfanya Rais Perez awe amepita mara 3 sasa bila kupingwa.

Perez aliwahi kuwa Rais wa Real kuanzia Mwaka 2000 na kisha kurejea tena wadhifa huo Mwaka 2009 na kuushika hadi sasa.

Perez, mwenye Miaka 70, bado ana ari kubwa kuiongoza Real Madrid na kushusha Mataji mengine mengi hasa katika kipindi hiki ambacho Real imepanda Chati mno katika Historia yao iliyotukuka.

Perez, ambae amempongeza mno Zinadine Zidane, hivi sasa ana mpango kabambe wa kuboresha na kumwongezea Mkataba Kocha Mkuu Zinedine Zidane ambae amewapa Mataji mawili mfululizo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Msimu huu ulioisha Juzi pia kubeba Ubingwa wa La Liga.

REAL PEREZ

Habari MotoMotoZ