LIONEL MESSI AMSIFIA CRISTIANO RONALDO - AMTAJA ANA 'KIPAJI CHA AJABU'!

NI NADRA sana kwa Wachezaji wa Barcelona na Real Madrid kusifiana lakini Lionel Messi ameibuka na kumpongeza Cristiano Ronaldo.

CR7-MESSIMessi amemsifia Ronaldo kwamba ana kipaji cha pekee kwa kuisaidia Real Madrid kubeba UEFA CHAMPIONZ LIGI walipoibamiza Juventus 4-1 Wiki iliyopita huku Ronaldo akipiga Bao 2.
Mara nyingi Messi na Ronaldo hupambana kuzoa Mataji na hata safari hii wanachuana tena kugombea Ballon d'Or huku Ronaldo akionekana na uhakika kuitwaa Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora Duniani kwa mara ya 5 na kumfikia Messi kwa idadi.
Lakini Messi amesisitiza upinzani kati yake na Ronaldo ni kitu kinachokuzwa na kushabikiwa na Vyombo vya Habari.
Huku akimtaja Ronaldo kama mmoja wa Wachezaji Bora Duniani, Messi ametamka: "Huo upinzani kati yetu umebuniwa na Wanahabari na si sisi!"
Aliongeza: "Sisi tunachotaka ni kufanya vyema kila Mwaka kwa Timu zetu na kinachosemwa nje sikipi umuhimu!"
Kuhusu Ronaldo, Messi amesisitiza: "Yeye. Ni Mchezaji wa Kipaji cha ajabu mno ana uwezo wa aina yaje na Mwaka hadi Mwaka anakuwa Bora zaidi na ndio maana yeye ni mmoja wa wale Bora Duniani!"

Habari MotoMotoZ