CAS YAIPIGA MSUMARI ATLETICO, KIFUNGO CHA FIFA KUSAJILI CHABAKI!

ATLETICO-BARCACAS(Court of Arbitration for Sport), Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, imeitupa Rufaa ya Klabu ya Spain Atletico Madrid iliyopinga kufungiwa na FIFA kusajili Wachezaji Wapya.
Atletico, na wenzao wa Spain Real Madrid, waliadhibiwa na FIFA kutosajili Wachezaji Wapya kwa kukiuka Kanuni za Kusajili Wachezaji Chipukizi.
Hatua hii ya CAS inamaanisha Atletico hairuhusiwi kusajili Mchezaji Mpya hadi Dirisha la Uhamisho la Januari 2018.
FIFA iliwaadhibu Atletico na Real Mwaka Jana kutosajili kwa Madirisha ya Uhamisho Mawili na pia kutwangwa Faini za Pauni 622,000.
CAS iliipunguzia Real Adhabu yao kwa Mwaka Mmoja lakini kwa Atletico hawakupata afueni.
Hivyo Atletico hawawezi kusajili Mchezaji Mpya hadi Januari 2018 lakini wako huru kumuuza yeyote.
Hatua hii inamaanisha Atletico haiwezi hivi sasa kumchukua Alexandre Lacazette kutoka Lyon ya France licha ya kuwepo makubaliano kwa Klabu hizo mbili.

Habari MotoMotoZ