UCL: MABINGWA REAL KUWABONDA NAPOLI HUKO SANTIAGO BERNABEU?

UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Ratiba/Matokeo:
Mechi za Kwanza
Jumanne 14 Februari 2017
Benfica 1 Borussia Dortmund 0      
Paris Saint Germain 4 Barcelona 0          
Jumatano 15 Februari 2017
Bayern Munich v Arsenal                 
Real Madrid v Napoli              
+++++++++++++++++++++++++
IMG-20170215-WA0001SANTIAGO BERNABEU huko Madrid, Spain itakuwa na Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya Mabongwa Watetezi Real Madrid na Timu toka Italy Napoli.
Habari njema kwa Real ni kupona kwa Staa wao na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo ambae alikuwa na maumivu toka Mechi yao ya La Liga ya Jumamosi walipocheza na Osasuna na kumfanya akose Mazoezi ya Juzi Jumatatu.
Lakini Real watamkosa Fowadi wao Gareth Bale licha ya Mchezaji huyo kurejea Mazoezini baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akijiuguza Enka yake.
Mechi hii italuwa ya kwanza kati ya Real na Napoli kwani hazijawahi kukutana kwenye Mashindano yeyote.
Wakati Mabingwa Real wakisaka kutinga Robo Fainali ya UCL kwa mara ya 7 mfululizo, hii ni mara ya pili tu kwa Napoli kufika hatua hii.
Mechi hii inawakutanisha Real ambao wamefungwa Mechi 2 tu Msimu huu na Napoli ambao hawajafungwa tangu Oktoba wakiwa kwenye mbio za Mechi 18 bila kipigo.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
REAL MADRID: Navas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo, Toni Kroos, Casemiro, James Rodriguez, Lucas, Ronaldo, Benzema.
NAPOLI: Reina, Hysaj, Albiol, Koulibaly, Allan, Diawara, Hamsik, Callejon, Insigne, Mertens
REFA: Damir Skomina (Slovenia)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo
Mechi za Kwanza
Jumanne 21 Februari 2017
Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid            
Manchester City v Monaco               
Jumatano 22 Februari 2017
FC Porto v Juventus               
Sevilla v Leicester City           
Mechi za Pili
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
Jumanne 7 Machi 2017
Arsenal v Bayern Munich                 
Napoli v Real Madrid              
Jumatano 8 Machi 2017
Barcelona v Paris Saint Germain (0-4)           
Borussia Dortmund v Benfica (0-1)      
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto               
Leicester City v Sevilla           
Jumatano 15 Machi 2017 
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen            
Monaco v Manchester City