LA LIGA: REAL WAITOA BARCA KILELENI, RONALDO AKIONGOZA!

LALIGA-2016-17-2REAL MADRID wamerejea tena kileleni mwa La Liga baada ya Jana kuifunga Osasuna 3-1 huko Estadio El Sadar Uwanja ambao Kocha wa Real Zinedine Zidane hajawahi kupata ushindi tangu akiichezea Timu hiyo.

Mapema Jana, wakicheza Ugenini, Mabingwa Watetezi wa La Liga Barcelona waliinyuka Deportivo Alaves 6-0 na kutwaa uongozi wa La Liga.

Bao za Barca kwenye Mechi hiyo zilifungwa na Luis Suarez, Bao 2, Neymar, Messi, Ruano, alijifunga mwenyewe na Ivan Rakitic.

Kwenye Mechi ya Real, Bao zao 3 zilifungwa na Cristiano Ronaldo, Isco na Vazquez wakati lile la Osasuna likipigwa na Leon Limones.

Ushindi huu umewaweka Real kileleni wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 20 wakifuata Barca wenye Pointi 48 kwa Mechi 22.

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Februari 10

RCD Espanyol 1 Real Sociedad 2

Jumamosi Februari 11

Real Betis 0 Valencia C.F 0

Deportivo Alaves 0 FC Barcelona 6

Athletic de Bilbao 2 Deportivo La Coruna 1

Osasuna 1 Real Madrid CF 3

Jumapili Februari 12

1400 Villarreal CF v Malaga CF

1815 CD Leganes v Sporting Gijon

2030 Las Palmas v Sevilla FC

2245 Atletico de Madrid v Celta de Vigo

Jumatatu Februari 13

2245 SD Eibar v Granada CF