LA LIGA: LEO REAL KUTINGA EL SADAR ‘DIMBA NUKSI’ KWA ZIDANE!

ZIDANE-RONALDO-SITLEO Usiku, Vinara wa La Liga Real Madrid wako Ugenini Estadio El Sadar kucheza na Timu ya mkiani Osasuna lakini Uwanja huo ni ‘nuksi’ kwa Meneja wao Zinedine Zidane.

Uwanja huo una mlolongo wa matokeo na historia mbaya kwa Kocha wa Real Zinedine Zidane tangu enzi za Uchezaje wake ambako walifungwa katika Mechi zake za kwanza, 3-1 na 1-0, Misimu ya 2001/02 na 2002/03.

Mechi ya 3 kwenda huko kama Mchezaji hakuchezi kwani alikuwa Majeruhi na Real kutoka 1-1 wakati Mechi ya 4 walitoka Droo na ya 5 na ya mwisho kama Mchezaji aliikosa kwa kuwa Kifungoni.

Kama Kocha, akiwa Msaidizi wa Carlo Ancelotti, Real waliambua Sare ya taabu.

Leo Usiku Zinedine Zidane anatinga tena Estadio El Sadar akiiongoza Real ambao wanaongoza La Liga wakiwa Pointi 1 na Mechi 2 mkononi dhidi ya Mahasimu wao Barcelona ambao nao Leo wapo Ugenini kucheza na Deportivo Alaves Timu ambayo imepanda Daraja Msimu huu na ndio Mpinzani wake kwenye Fainali ya Copa del Rey na ambayo Mwezi Septemba iliichapa Barca 2-1 huko Nou Camp.

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Februari 10

RCD Espanyol 1 Real Sociedad 2

Jumamosi Februari 11

1500 Real Betis v Valencia C.F

1815 Deportivo Alaves v FC Barcelona

2030 Athletic de Bilbao v Deportivo La Coruna

2245 Osasuna v Real Madrid CF

Jumapili Februari 12

1400 Villarreal CF v Malaga CF

1815 CD Leganes v Sporting Gijon

2030 Las Palmas v Sevilla FC

2245 Atletico de Madrid v Celta de Vigo

Jumatatu Februari 13

2245 SD Eibar v Granada CF