MTU 9 BARCA YATINGA KWA MBINDE FAINALI, YIONDOA MTU10 ATLETI!

==RED 3 ZATEMBEA!

MESSI-ESPANYOLMABINGWA Watetezi Barcelona wametinga Fainali ya Kombe la Mfalme wa Spain Copa del Rey baada Jana kutoka Sare 1-1 na Atletico Madrid huko Nou Camp na kusonga kwa Jumla ya Bao 3-2 kwa vile walishinda Mechi ya Kwnza 2-1.Barca walifunga Bao lao Dakika ya 43 na Atleti kusawazisha Dakika ya 83 kupitia Kevin Gameiro ambae kabla ya hapo alikosa Penati.Mechi hii ilishuhudia Kadi Nyekundu 3 ambazo walipewa Wawili wa Barca Luis Suarez, Dakika y 90, na Sergi Roberto, Dakika ya 57, na mwingine Mchezaji wa Atleti Yannick Carrasco katika Dakika ya 69.Mbali ya matukio hayo pia Antoine Griezmann wa Atleti 'alidhulumiwa' Bao la wazi kwa madai ni Ofsaidi huku Lionel Messi wa Barca akipiga Posti.Sasa Barcelona watacheza Fainali na Mshindi kati ya Alaves au Celta Vigo ambao Leo wanacheza Mechi ya Pili ya Nusu Fainali .Timu hizo zilitoka 0-0 katika Mechi yao ya Kwanza.