LA LIGA: KIPORO CHA REAL CHAPANGWA!

COPA DEL REY: LEO BARCA AU ATLETI NANI FAINALI?

LALIGA-2016-17-2-3-1WAKATI Mechi ya kiporo cha La Liga cha Real Madrid kikipangwa Tarehe mpya, Leo ni Marudiano ya Nusu Fainali ya Copa del Rey huko Nou Camp kati ya Barcelona na Atletico Madrid.

LA LIGA: KIPORO CHA REAL CHAPANGWA!

Mechi ya La Liga kati ya Vinara wake Real Madrid na Valencia sasa itachezwa Februari 22 Nyumbani kwa Valencia.

Awali Mechi hii ilikuwa ichezwe Desemba lakini ikifutwa kutokana na ushiriki wa Real huko Japan kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.

Upangwaji upya wa Mechi hii unazidi kuwashushia Real mzigo mkubwa kwani sasa sasa watakuwa na Mechi 8 ndani ya Siku 25 zikiwemo Mechi 2 za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Napoli ya Italy.

Juzi Jumapili, Mechi nyingine ya Real ya La Liga Ugenini na Celta Vigo ilifutwa kutokana na Dhoruba iliyoharibu Paa la Uwanja wa Balaidos na hadi sasa Mechi hiyo haijapangiwa Tarehe mpya.

COPA DEL REY: LEO BARCA AU ATLETI NANI FAINALI?

Mabingwa Watetezi Barcelona wanachungulia Fainali ya 4 mfululizo ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, wakati Leo wakicheza Mechi ya Pili ya Nusu Fainali na Atletico Madrid huko Nou Camp huku wao wakiwa mbele baada kushinda Mechi ya Kwanza 2-1.

Kwenye Mechi hii, Barca watamkosa Staa wao wa Brazil Neymar ambae yupo Kifungoni Mechi 1 na pia Nyota wao Lionel Messi anapaswa kujichunga hii Leo kwani akilambwa Kadi ya Njano tu hatacheza Fainali.

Copa del Rey

Nusu Fainali

Ratiba – Mechi za Pili

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Jumanne Februari 7

Barcelona v Atletico Madrid [2-1]

Jumatano Februari 8

Alaves v Celta Vigo [0-0]