LA LIGA: BARCA WAISOGELEA KILELENI REAL AMBAO MECHI YAO YA LEO IMEFUTWA!

LALIGA-2016-17JANA huko Nou Camp, Barcelona waliitandika Athletic Bilbao 3-0 na kuwasogelea Vinara Real Madrid na kuwa Pointi 1 nyuma yao kwenye La Liga.

Leo Real Madrid walitakiwa kucheza Ugenini na Celta Vigo lakini Mechi hiyo imefutwa baada ya Uwanja wa Balaidos kupigwa na Dhoruba na kuharibu Paa ambalo linasemekana si salama kwa Washabiki.

Kufutwa kumeifanya Real iwe imecheza Mechi 2 pungufu ya Barca lakini bado wanaongoza La Liga.

Hapo Jana Bao za Barca zilifungwa na Paco Alcacer, Dakika ya 18, Lionel Messi, Dakika ya 40, na Aleix Vidal, Dakika ya 67.

LA LIGA

Ratiba/Matokeo:

Jumamosi Februari 4

Atletico de Madrid 2 CD Leganes 0

Valencia C.F 0 SD Eibar 4

Malaga 0 RCD Espanyol 1

Barcelona 3 Athletic Bilbao 0

Jumapili Februari 5

1400 Sevilla FC v Villarreal CF

1815 Sporting Gijon v Deportivo Alaves

2030 Real Sociedad v Osasuna

2245 Celta de Vigo v Real Madrid CF [IMEAHIRISHWA]

Jumatatu Februari 6

2245 Granada CF v Las Palmas