COPA DEL REY: BARCA YAFUNGA MWAKA BILA MSN - MESSI, SUAREZ, NEYMAR KWA KUTWANGA 7, TURAN HETITRIKI!

BARCA-TRIO-MSNArda Turan alipiga Bao 3 wakati Barcelona wakiichapa Timu ya Daraja la 3 Hercules 7-0 na kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey kwenye Mechi iliyochezwa Nou Camp Jana Usiku.

Licha ya Barca kutoka 1-1 na Hercules katika Mechi ya Kwanza, Kocha Mkuu wa Barca, Luis Enrique, mara baada ya Barca kuitwanga Espanyol 4-1 katika Mechi ya La Liga Juzi Jumapili, aliamua kuwapa likizo ya mapema Mastaa wake Lionel Messi, Luis Suarez, Neymar na Pique likizo kwa vile Soka la Spain litasimama hadi baada ya Wiki ya Pili ya Januari kupisha Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Nila ya hao Nyota, Barca waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Digne, Dakika ya 37, na Rakitic, ikiwa ni Penati ya Dakika ya 45.

Kipindi cha Pili, Barca waliongeza Bao nyingine kupitia Rafinha, Dakika ya 50, Turan, 55, 86 na 89, na Alcácer, 73        

Wakati Timu nyingine Spain zikihenya kufunga Mwaka kwa Mechi hizi za Copa del Rey, Real Madrid wao walicheza mapema Mechi zao za Kombe hili na kufuzu kwa vile walikwenda Japan ambako Juzi walitwaa Kombe la Ubingwa wa Kombe la Dunia kwa Klabu.

COPA DEL REY

Mechi za Marudiano – Raundi ya Mtoano Timu 32

Jumanne Desemba 20

Villarreal CF 1 CD Toledo1 [4-1]

Real Sociedad 1 Real Valladolid 1 [4-2]  

Atletico de Madrid 4 Guijuelo 1 [10-1]     

Malaga CF 3 Cordoba CF 4 [3-6] 

Las Palmas 2 Huesca 1 [4-3]        

Jumatano Desemba 21

Sevilla FC 9 Formentera 1 [14-2] 

SD Eibar 3 Sporting Gijon 1 [5-2]

Deportivo La Coruna 3 Real Betis 1 [3-2]           

Osasuna 2 Granada CF 0 [2-1]    

Valencia C.F 2 CD Leganes 1 [5-2]         

FC Barcelona 7 Hercules CF 0 [8-1]        

Alhamisi Desemba 22

22:00  Deportivo Alaves v Gimnastica    

22:00  Celta de Vigo v UCAM Murcia      

23:00  Athletic de Bilbao v Real Racing Santander      

23:00  RCD Espanyol v Alcorcon 

**Real Madrid ilikamilisha Mechi zake na kusonga kwa kuitwanga Cultural Leobesa Jumla ya Mabao 13-2 kwa Mechi 2

Habari MotoMotoZ