HATIMAE MESSI AKUTANA NA MTOTO WA AFGHANISTAN ALIEPATA UMAARUFU DUNIANI KWA KUVAA JEZI YA MFUKO WA PLASTIKI WA STAA HUYO!

MESSI-MTOTO-AFGHAN-MEETMWEZI Januari, mwanzoni mwa Mwaka huu, Dunia ilipata mtikisiko pale Mtoto mdogo toka Nchi yenye shida kubwa na balaa kubwa ya Vita, Afghanistan, aliponaswa kwenye Picha akiwa amevaa Jezi iliyotengenezwa kwa Mfuko wa Plastiki na kuandikwa kwa Mkono Mgongoni Namba 10 na Jina la Messi.

Picha hiyo ikarindima Mitandaoni na kila Gazeti Duniani kote ikimuonyesha Murtaza Ahmadi, mwenye Miaka 6, akiwa na Jezi hiyo ambayo mwenyewe alikiri Lionel Messi, Staa wa FC Barcelona kutoka Argentina, ni kipenzi chake.

Baada ya hapo Mtoto huyo alipelekewa Jezi halisi na Zawadi nyingine toka kwa Messi.

Lakini umaarufu huo wa Murtaza Ahmadi ukaibua hatari kubwa kwa Mtoto huyo na Familia yake na wakalazimika kuikimbia Nchi yao Afghanistan ambako walikuwa wakiishi Jimbo la Ghazni, Wilaya ya Jaghori na kukimbilia Pakistan.

Hii Leo, Mjini Doha, Qatar, Mtoto Murtaza amekutana uso kwa uso na kipenzi chake Lionel Messi na Staa huyo kumbeba Mtoto huyo kwa furaha.

Messi ametua Qatar na Timu yake Barcelona kucheza Mechi ya Kirafiki na Klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia baadae Leo.

Kukutana kwa Messi na Murtaza kumetangazwa na Kamati ya Matayarisho ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2022 za Qatar ambao ndio waliandaa safari ya Mtoto huyo kwenda Doha.

Habari MotoMotoZ