RONALDO, BENZEMA & MODRIC KUPUMZIKA MADRID v DEPORTIVO

REAL-ZIZOUCristiano Ronaldo na Karim Benzema hawamo kwenye Kikosi cha Real Madrid ambacho Jumamosi kinacheza Mechi ya La Liga na Deportivo La Coruna Uwanjani Santiago Bernabeu Jijini Madrid huko Nchini Spain.
Kwa vile nae Gareth Bale ni Majeruhi, basi Real, ambao wanaongoza La Liga wakiwa Pointi 6 mbele ya Mabingwa FC Barcelona, itakuwa imekosa Fowadi yake yote kamili ya Timu ya Kwanza.

Pia, Kocha Zinedine Zidane ameamua kumpumzisha Kiungo mahiri Luka Modric kwa ajili ya Mechi hii.

++++++++++++++++

JE WAJUA?

-Real haijafungwa katika Mechi 34 mfululizo na hii wameifikia Rekodi ya Klabu hiyo iliyowekwa huko nyuma!
++++++++++++++++

Zidane ameamua kumchukua Fowadi wa Timu yao ya Rizevu, Mariano, ili aungane na Alvaro Morata na Lucas Vazquez kwenye Mashambulizi kwa ajili ya Mechi hii na Deportivo ambao wako Nafasi ya 16 kwenye La Liga wakiwa Pointi 21 nyuma ya Vinara Real.
Zidane hakusema kwa nini Mastaa wake wako nje lakini Real, baada ya Mechi hii, wanasafiri kwenda Japan kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu wao wakiwa ndio Wawakilishi wa Bara la Ulaya baada ya kutwaa Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu uliopita.

LA LIGA

Ratiba

**Saa za Bongo

Ijumaa Desemba 9

2245 Malaga CF v Granada CF

Jumamosi Desemba 10

1500 Osasuna v FC Barcelona

1815 Real Sociedad v Valencia C.F

2030 Las Palmas v CD Leganes

2245 Real Madrid CF v Deportivo La Coruna

Jumapili Desemba 11

1400 SD Eibar v Deportivo Alaves

1815 Celta de Vigo v Sevilla FC

2030 RCD Espanyol v Sporting Gijon

2245 Real Betis v Athletic de Bilbao

Jumatatu Desemba 12

2245 Villarreal CF v Atletico de Madrid

Habari MotoMotoZ