SPAIN KODI BALAA: DI MARIA AKIRI KOSA, HUKUMU JELA MWAKA, FAINI £1.76M!

ANGELDIMARIAWINGA wa Paris Saint-Germain kutoka Argentina Angel Di Maria amehukumiwa Kifungo cha Jela Mwaka Mmoja na kutwangwa Faini ya Pauni Milioni 1.76.

Hukumu hiyo imetokana na Ukwepaji Kodi huko Spain wakati akiwa Mchezaji wa Real Madrid na yeye mwenyewe kukiri Makosa Mawili.

Di Maria alidumu Real Miaka Minne na kuihama kwenda Man United Mwaka 2014 ambako nako alihamia PSG Mwaka 2015.

Ingawa amehukumiwa Kifungo cha Jela lakini hatatumikia Kifungo hicho ambacho kitakuwa Kifungo cha Nje kwa sababu huko Spain Kifungo cha chini ya Miaka Miwili hutumikiwa nje ili mradi tu uwe hujawahi kuwa na Rekodi ya Uhalifu.

Hukumu hii imekuja Siku Moja tu baada ya Meneja wa zamani wa Real, Jose Mourinho, ambae sasa yupo Man United kuburuzwa Mahakamani nae pia akituhumiwa na Ukwepaji Kulipa Kodi.

Wiki iliyopita, nae Mchezaji mwingine wa Real, Cristiano Ronaldo, ameburuzwa Mahakamani akituhumiwa pia kukwepa kulipa Kodi.

Mwaka Mmoja uliopita, Lionel Messi wa Barcelona alihukumiwa Jela Miezi 21 na Faini juu kwa Makosa hayo hayo ambayo pia yalimkumba Mchezaji mwingine wa Barca Javier Mascherano.

RAIS WA REAL PEREZ ‘KUMBEMBELEZA’ RONALDO KUBAKI BERNABEU BAADA FIFA KOMBE LA MABARA KWISHA!

REAL PEREZ RONALDORAIS wa Klabu ya Real Madrid Florentino Perez amesema kuwa bado hajaongea na Cristiano Ronaldo kuhusu hatima yake lakini atafanya hivyo baada ya kumalizika kwa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayoendelea hivi sasa huko Nchini Russia.

Ronaldo, mwenye Miaka 32, Wiki iliyopita alitamka ataondoka Spain na kuiacha Real Madrid mara baada ya kuburuzwa Mahakamani alikofunguliwa Mashitaka ya Ukwepaji Kulipa Kodi ya Thamani ya Euro Milioni 14.7 kati ya Miaka 2011 na 2014 kitu ambacho mwenyewe na wasaidizi wake wamekipinga katakata.

Hivi sasa Ronaldo, ambae alisaini Mkataba Mpya na Real wa Miaka Mitano Novemba 2016, yupo Russia na Timu ya Taifa ya Portugal kwenye Kombe la Mabara.

Mara baada ya Jana kupita bila kupingwa katika Uchaguzi wa Real Madrid na kuthibitishwa kama Rais wa Klabu hiyo kwa Miaka Minne mingine ijayo wadhifa ambao ameushika tangu 2009, Perez alieleza: “Kitu pekee naweza kusema ni kuwa Cristiano Ronaldo ni Mchezaji wa Real Madrid.”

+++++++++++++

RONALDO, PEREZ NA REAL!

-Mwaka 2009, Perez, akishika wadhifa wa Rais wa Real kwa kipindi cha pili, alimsaini Ronaldo kutoka Manchester United kwa Dau la Rekodi ya Dunia la Pauni Milioni 80.

-Ronaldo, ambae aliisaidia Man United kutwaa Ubingwa mara 3 na UEFA CHAMPIONZ LIGI katika Miaka yake 6, alitwaa Ballon d'Or mara tu baada ya kutua Bernabeu na pia kuwapa UEFA CHAMPIONZ LIGI, La Liga na Kombe la Dunia kwa Klabu.

-Baada kuichezea Real Miaka 8, yote chini ya Rais Perez, Ronaldo ameweka Rekodi ya Magoli kwa Klabu kwa kuifungia Bao 406 katika Mechi 394.

-Wiki 2 zilizopita, Ronaldo aliisaidia Real kutwaa Ubingwa wa Ulaya wao wa 12 huku yeye akipiga Bao 2 walipoichaka Juventus 4-1 kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Cardiff, Wales.

+++++++++++++

Pereza, akiongea na Stesheni ya Radio ya Onda Cero, aliendelea: "Ni wazi kuna kitu kimetokea, kitu ambacho kimemkera, kinamtesa. Nina hakika atatuambia na tutaona!”

Perez alisema: “Yupo kwenye Mashindano muhimu, Kombe la Mabara. Hayajaisha na sitaki kuisumbua Timu ya Portugal!”

Pia Perez amedai Ronaldo, ambae sasa anahusishwa na kurudi Manchester United au kuhamia Paris St-Germain, hahangaishwi na Fedha.

Perez amenena: “Yeye anataka kuwa Mchezaji Bora Duniani tu. Ikiwa anataka kuihama Real, basi si sababu ya Fedha!”

Vile vile Perez amethibitisha kuwa hawajapokea Ofa yeyote ya kumnunua Ronaldo, Alvaro Morata na James Rodriguez kama inavyovumishwa sasa.

Ameeleza: “Tunataka kubakisha Wachezaji wetu wote kwa ajili ya Msimu ujao!”

FLORENTINO PEREZ KUBAKIA RAIS WA REAL MADRID HADI 2021

>FLORENTINO PEREZ ‘AMPA 5’ ZIDANE!

REAL PEREZ ZIDANEMABINGWA wa Spain na Ulaya Real Madrid wataongozwa na Florentino Perez kwa Miaka mingine Minne kama Rais baada ya kutojitokeza kwa Mgombea mwingine kwenye Uchaguzi wa Rais wa Klabu hiyo.

Siku ya mwisho ya Wagombea kujitokeza ilikuwa Jana Jumapili Saa 6 Usiku na hakuna yeyote aliejitokeza kuchuana na Rais wa sasa wa Mabingwa hao.

Hali hiyo inamfanya Rais Perez awe amepita mara 3 sasa bila kupingwa.

Perez aliwahi kuwa Rais wa Real kuanzia Mwaka 2000 na kisha kurejea tena wadhifa huo Mwaka 2009 na kuushika hadi sasa.

Perez, mwenye Miaka 70, bado ana ari kubwa kuiongoza Real Madrid na kushusha Mataji mengine mengi hasa katika kipindi hiki ambacho Real imepanda Chati mno katika Historia yao iliyotukuka.

Perez, ambae amempongeza mno Zinadine Zidane, hivi sasa ana mpango kabambe wa kuboresha na kumwongezea Mkataba Kocha Mkuu Zinedine Zidane ambae amewapa Mataji mawili mfululizo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Msimu huu ulioisha Juzi pia kubeba Ubingwa wa La Liga.

REAL PEREZ

MSTUKO: CRISTIANO RONALDO ATAKA KUNG’OKA REAL SASA!

Cristiano Ronaldo amewaambia Real Madrid anataka kuondoka Real Madrid Dirisha hili la Uhamisho.

RONALDO-BALLONDORImeripotiwa kuwa Supastaa huyo kutoka Ureno amempasha Rais wa Real, Florentino Perez, anataka kuondoka Spain mara tu baada ya kuburuzwa Mahakamani akishitakiwa kwa Ukwepaji Kulipa Kodi.

Ronaldo ameshitakiwa Mahakamani kwa kukwepa kulipa Kodi ya Spain ya Euro Milioni 14.7 kitu ambacho amepinga vikali.

Kwa mujibu wa Gazeti la Ureno A Bola, Ronaldo mwenye Miaka 32, amekasirishwa mno na jinsi alivyotendewa na sasa anataka kuihama Nchi ya Spain.

Hadi sasa Klabu ya Real haijatamka lolote kuhusun ripoti hizi lakini ni wazi Rais Perez hatataka Mchezaji Bora Duniani ambae amewabebesha Ubingwa wa La Liga na UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu uliokwisha hivi karibuni ang’oke hapo.

Ronaldo, ambae ametwaa Ballon d’Or mara 4, ameifungia Real Mabao 406 katika Mechi zake 394 tangu atue hapo kutoka Manchester United Mwaka 2009.

Akiwa na Real amevunja Rekodi kadhaa na kutwaa Mataji makubwa yakiwemo UEFA CHAMPIONZ LIGI 3, La Liga 2 na FIFA Kombe la Dunia kwa Klabu 2.

Hivi sasa Ronaldo ana Mkataba na Real hadi 2021 na Uhamisho wowote utakaomhusu yeye ni lazima utakuwa wa Dau la Rekodi ya Dunia.

 

RONALDO-KESI UKWEPAJI KODI: WAKILI WAKE ADAI 'KESI SI YA HAKI'!!

Antonio Lobo Xavier, mmoja wa Mawakili wa Cristiano Ronaldo, amejibu tuhuma za Waendesha Mashitaka wa Mahakama za Spain wanazodai Staa huyo alikwepa kulipa Kodi yenye thamani ya Euro Milioni 14.7 kati ya Miaka ya 2011 na 2014.
REAL-RONALDO-BAOJana Ronaldo, Mchezaji Bora Duniani anaechezea Klabu ya Spain Real Madrid na Timu ya Taifa ya Portugal, alifunguliwa Kesi rasmi Mahakamani ya Ukwepaji Kulipa Kodi.
Wakili huyo amedai Kesi hiyo si haki na kuwa Mchezaji huyo Mwaka 2014 aliwasilisha Mapato yake yote yatokanayo na Mauzo ya Picha na Matangazo yake kama ipasavyo na kulipa Kodi zote stahiki.
Wakili Xavier amedai: "Hili la Kesi ni kitu cha kushtukiza na Ronaldo anahisi hatendewi haki!"
Aliongeza: "Si kwamba hakuwasilisha Mapato yake yote. Alipeleka kila kitu kwenye Mamlaka ya Kodi lakini inaelekea Wahusika hawakupendelea hilo. Hamna kwenye Sheria popote panaposema alivunja Sheria!"
Pia Wakili Xavier alidai Kesi hii ya Ronaldo na ile ya Lionel Messi ambayo alipigwa Faini na kuhukumiwa Kifungo cha Miezi 21 zina tofauti kwani Ronaldo alifuata ushauri wa kulipa Kodi.
Wakili huyo ameeleza: "Kesi ya Messi na wengine kuhusu Kodi ipo tofauti na ya Ronaldo kwani hao hawakusilisha Mapato yao wakati Ronaldo amepeleka kila kitu!"
Vile vile Lobo Xavier ametoboa kuwa Kesi hii ya Ronaldo imekimbizwa Mahakamani kwa sababu tu ya kukwepa kupoteza haki ya kumshitaki kutokana na muda kihalali wa kufanya hivyo unakaribia kwisha.
Lobo Xavier pia ametoboa kuwa kwa jinsi Ronaldo alivyowasilisha Mapato yake Mwaka 2014 na kulipa kwa Mkupuo Kodi husika upo uwezekano mkubwa alilipa Kodi zaidi kupita kama angelipa Kodi kila Mwaka kwa Miaka kati ya 2011 hadi 2014.
Alipohojiwa kuhusu uchunguzi dhidi yake na Redio ya Nchini kwao Ureno kuhusu tuhuma za Ukwepaji Kodi, Ronaldo alijibu:"Quien no debe no teme", ambayo tafsiri yake inamaanisha "Yule ambae hana cha kuficha, haogopi kitu!"
Kwa mujibu wa Magwiji wa Habari za Fedha, Forbes, Ronaldo ndie Mwanamichezo alievuna Pesa nyingi Duniani kwa Miaka Miwili mfululizo akizoa Dola Milioni 93 kutokana na Mshahara, Bonasi na Matangazo kwa Mwaka Jana

Habari MotoMotoZ