BAYERN WAGUTUKA, SANCHEZ ADAI PAUNI 420,000 KWA WIKI ILI ASAINI!

ARSENAL SANCHEZ HATIMABayern Munich wamestushwa mno na madai ya Alexis Sanchez ya kutaka alipwe Mshahara wa juu kabisa ili asaini kwa Mabingwa hao wa Bundesliga na Maafisa wao wanahisi ni ujanja wake ili achukuliwe na Manchester City.

Inaaminika Bayern Munich na Man City ndizo Timu pekee ambazo zinamwania Straika huyo kutoka Chile ambae yuko na Arsenal na Mkataba wake huko unamalizika Mwakani.

Arsenal wenyewe hawataki Mchezaji huyo auzwe kwa Mpinzani wao yeyote anaecheza EPL, Ligi Kuu England, lakini madai haya ya Sanchez kwa Bayern ni wazi yataifanya Klabu hiyo ya Germany ibwage manyanga kumnunua na kuwaachia City kuwa Wanunuzi pekee.

Imeripotiwa kuwa Sanchez anataka Bayern imlipe Mshahara wa juu mno, £420,000 kwa Wiki, kitu ambacho hakimo kabisa kwenye Mfumo wa Wajerumani hao.

Kizuizi kingine ni Dau wanalotaka Arsenal wakimuuza Sanchez ambalo ni Pauni Milioni 50 ambalo nalo ni kubwa mno kwa Mchezaji aliebakiza Mwaka Mmoja tu kwenye Mkataba wake na hivyo anaweza kuondoka Bure bila kulipwa Senti ikifika Mwakani.

Kwa upande wa Man City, wao wako tayari kumlipa Mshahara wa Pauni 300,000 kwa Wiki endapo Arsenal itaruhusu aende Etihad.

 

 

CARABAO CUP: DROO RAUNDI YA 1 TAYARI, MECHI AGOSTI 8 & 9

DROO ya kupanga Mechi za Raundi ya Kwanza ya Kombe la Ligi la England, EFL CUP, imefanyika Jana huko Bangkok, Thailand.

CARABAO-CUPKwa Msimu huu unaokuja wa 2017/18 Kombe hilo litajulikana kana CARABAO CUP kutokana na Udhamini wa Watengenezaji wa Kinywaji cha Kuongeza Nguvu kiitwacho Carabao.

Kampuni inayomiliki Kinywaji hicho imesaini Mkataba wa Miaka Mitatu wa kudhamini EFL CUP ambalo Mabingwa Watetezi wake ni Manchester United.

Kwenye Droo hii ya Raundi ya Kwanza Timu zote 48 za Madaraja ya Ligi England ya Ligi 1 na Ligi 2 zilikuwemo kwenye Chungu pamoja na Timu 22 kati ya 24 za Daraja la Championship.

Hull City na Middlesbrough, waliomaliza Nafasi za 18 na 19 za EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kushushwa kwenda Championship, hazitakuwemo kwenye Droo hiyo na zitaanza Raundi ya Pili lakini Sunderland, iliyomaliza Nafasi ya 20 kwenye EPL na kushushwa nao, Jana ilipangiwa Mpinzani.

Hull na Boro zitaanza Raundi ya Pili pamoja na Timu zote za EPL ambazo hazichezi Mashindano ya UEFA Ulaya.MANUNITED-MABINGWA-EFLCUP

Timu za EPL ambazo zipo Ulaya ni Chelsea, Tottenham, Man City, Liverpool na Man United ambazo zipo UEFA CHAMPIONZ LIGI na Arsenal na Everton zinazocheza UEFA EUROPA LIGI.

Timu hizo zitaanza Raundi ya Tatu.

Mechi za Raundi ya Kwanza zitachezwa Agosti 8 na 9.

Fainali ya CARABAO CUP itachezwa Wembley Februari 25, 2018.

+++++++++++++++++

JE WAJUA?

Kombe la Ligi England pia liliwahi kujulikana kama:

-Milk Cup, Littlewoods Challenge Cup, Rumbelows Cup, Coca Cola Cup, Worthington's Cup, Carling Cup, Capital One Cup, na Msimu uliopita, EFL Cup.

-Bingwa Mtetezi ni Manchester United alietwaa Kombe Februari kwa kuichapa Southampton 3-2.

+++++++++++++++++

DROO KAMILI:

North Section

Coventry v Blackburn

Nottingham Forest v Shrewsbury

Bradford v Doncaster

Mansfield v Rochdale

Grimsby v Derby

Barnsley v Morecambe

Oldham v Burton

Wigan v Blackpool

Bury v Sunderland

Sheffield Wednesday v Chesterfield

Accrington v Preston

Fleetwood v Carlisle

Rotherham v Lincoln

Sheffield United v Walsall

Scunthorpe v Notts County

Crewe v Bolton

Leeds v Port Vale

South Section

Birmingham City v Crawley Town

Exeter City v Charlton Athletic

QPR v Northampton Town

Newport County v Southend United

Bristol City v Plymouth Argyle

Cardiff City v Portsmouth

Millwall v Stevenage

Oxford United v Cheltenham Town

AFC Wimbledon v Brentford

Norwich City v Swindon Town

Bristol Rovers v Cambridge United

Peterborough United v Barnet

Wycombe Wanderers v Fulham

Colchester United v Aston Villa

Wolves v Yeovil Town

Reading v Gillingham

Forest Green Rovers v MK Dons

Luton Town v Ipswich Town

VICTOR LINDELOF: NI RASMI ASAINI MANCHESTER UNITED KWA £31M TOKA BENFICA!

>MOURINHO AMPA ERIC BAILLY ‘PACHA’ MUTRIBU!

MANCHESTER UNITED imekamilisha kumsaini Beki Victor Lindelof kutoka Benfica ya Ureno kwa Dau la Pauni Milioni 31.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Sweden mwenye Miaka 22 alitua Jiji la Manchester Jana kupimwa Afya na kuafiki Maslahi Binafsi na Jana Dili ilikamilika baada ya mambo yote kwenda sawa na kusaini Mkataba wa Miaka Minne na Kipengele cha Kuongeza Mwaka Mmoja juu yake.

MANUNITED-LINDELOF-SAINIMkataba huu unaanza rasmi Julai Mosi wakati Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa rasmi.

Lindelof, ambae ameichezea Sweden mara 12, sasa anakuwa ndie Beki alienunuliwa kwa Bei ghali na Man United tangu walipolipa Pauni Milioni 29.1 kumnunua Rio Ferdinand Mwaka 2002.

Victor Lindelof alijiunga na Benfica Mwaka 2012 akitokea Klabu ya kwao Sweden Vasteras SK na Msimu uliopita aliichezea Benfica mara 47 ikitwaa Dabo, Ubingwa na Kombe la Ureno.

Akiongea mara baada ya kusaini Mkataba, Lindelof alisema: “Nimefurahishwa mno. Nilifurahia muda wangu na Benfica na kujifunza mengi. Lakini sasa nangojea kwa hamu kucheza Ligi Kuu ndani ya Old Trafford na chini ya Jose Mourinho. Nipo tayari kuanza na kuchangia kwa Timu kutwaa Mataji.”

Nae Meneja Jose Mourinho ametamka: “Victor ni Kijana mwenye Kipaji kikubwa ambae mbeleni mwake ni kuzuri. Msimu uliopita ulituonyesha tunahitaji kuongeza nguvu na Vipaji kwenye Kikosi na Victor ni wa kwanza kujiunga!”

WACHAMBUZI:

Baadhi ya Wachambuzi wamedai Manchester United imekuwa ikipwaya kwenye idara ya Masentahafu tangu alipostaafu Meneja Sir Alex Ferguson Mwaka 2013.

Msimu uliopita, kuna kipindi sehemu hiyo ilitulia walipocheza pamoja Phil Jones na Marcos Rojo hadi ikamfanya Mourinho asimnunue Victor Lindelof Mwezi Januari.

Lakini wote wakaumia pamoja na Chris Smalling na ikabidi Daley Blind ajaze nafasi hiyo.

Akiwa na Urefu wa Futi 6 Inchi 2, Lindelof ni Jabali kwenye ngome na Umri wake wa Miaka 22 unamfanya awe Kijana zaidi kupita Rio Ferdinand alipojiunga na Man United Mwaka 2002 kutoka Leeds United.

Wachambuzi hao wanadai ikiwa Lindelof ataiga kiasi tu ya yale Rio aliyomletea Ferguson basi Mourinho atakuwa amepata Pacha safi mno wa Eric Bailly.

EPL, LIGI KUU ENGLAND MSIMU MPYA 2017/18: RATIBA HADHARANI, MABINGWA CHELSEA KUANZA NA BURNLEY!

MABINGWA Chelsea wataanza Msimu Mpya wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, wa 2017/18 utakaoanza Wikiendi Agosti 12 kwa kucheza Nyumbani na Burnley.
EPL-17-18-SITMechi ya Pili kwa Chelsea ni Ugenini huko Wembley kuivaa Tottenham ambao walimaliza EPL Nafasi ya Pili.
Arsenal wataanza kwao Emirates kucheza na Mabingwa wa zamani Leicester City lakini Agosti 26 wako huko Anfield kuivaa Liverpool.
Man United wataanzia kwao Old Trafford dhidi ya West Ham wakati Man City wapo Ugenini kucheza na Timu Mpya iliyopanda Daraja Brighton.
Wapya wengine, Mabingwa wa Daraja la Championship, Newcastle, wapo kwao St James' Park kucheza na Tottenham.
MECHI ZA UFUNGUZI - WIKIENDI YA AGOSTI 12:
Arsenal v Leicester City
Brighton and Hove Albion v Manchester City
Chelsea v Burnley
Crystal Palace v Huddersfield Town
Everton v Stoke City
Manchester United v West Ham United
Newcastle United v Tottenham Hotspur
Southampton v Swansea City
Watford v Liverpool
West Bromwich Albion v Bournemouth

KAA CHONJO: LEO RATIBA MSIMU MPYA 2017/18 EPL, LIGI KUU ENGLAND HADHARANI!

RATIBA ya EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwa Msimu Mpya wa 2017/18 itatangazwa Leo Saa 5 Asubuhi, Saa za Bongo.

Msimu Mpya wa EPL utaanza Jumamosi Agosti 12 lakini Agosti 6 ipo Mechi ya Kufungua Pazia Msimu ya kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa Chelsea na waliobeba FA CUP, Arsenal.

EPL-17-18-SITMsimu huu wa EPL wa 2017/18 utamalizika Jumapili Mei 13, 2018 ikiwa ni Wiki Moja mapema ili kupisha maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 zitakazochezwa huko Russia kuanzia Juni 14.

Kwenye EPL, Timu Mpya zilizopanda Daraja toka Championship ni Mabingwa wake Newcastle, Brighton na Huddersfield Town wakati zile ambazo zimeporomoka na kwenda Championship ni Hull City, Bournemouth na Sunderland.

Tarehe nyingine muhimu:

-Mashindano ya kugombea Kombe la Ligi, ambalo Msimu uliopita Mabingwa walikuwa Manchester United yataanza Agosti 7 kwa Raundi ya Kwanza ya Timu za Madaraja ya chini.

Msimu huu wa 2017/18, Kombe la Ligi, ambalo lilitwa EFL CUP Msimu uliopita kwa kukosa Udhamini, sasa litaitwa CARABAO CUP kutokana na Udhamini wa Vinywaji vya Kuongeza Nguvu kutoka huko Nchini Thailand.

-Manchester United, kama Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI Msimu uliopita, Agosti 8 watagombea UEFA SUPER CUP dhidi ya Mabingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI, Real Madrid.

-Liverpool wataanza Kampeni yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kucheza Mechi ya Raundi ya Mchujo hapo Agosti 15 au 16.

-Everton wataanza kampeni yao ya UEFA EUROPA LIGI kwenye Raundi ya Mchujo hapo Julai 27.

-Mechi za Makundi za UEFA CHAMPIONZ LIGI zitaanza Septemba 12 na 13 na Washiriki wa England ni Chelsea, Tottenham, Man City na Man United.

-Arsenal wao wataanza Makundi ya UEFA EUROPA LIGI hapo Septemba 14.

 

 

Habari MotoMotoZ