LIGI KUU ENGLAND: MAN UNITED SARE YA 4 MFULULIZO OLD TRAFFORD, MOURINHO ATIMULIWA UWANJANI!

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Matokeo:

Jumapili Novemba 27

Watford 0 Stoke City 1                  

Arsenal 3 Bournemouth 1              

Manchester United 1 West Ham United 1             

Southampton 1 Everton 0    

+++++++++++++++++++++++++++++

IBRA-GOLIMANCHESTER UNITED wametoka Sare yao ya 4 mfululizo ya EPL, Ligi Kuu England, Uwanjani kwao Old Trafford walipotoka 1-1 na West Ham.

Sekunde 90 tu tangu Mechi ianze, West Ham walifunga Bao kwa Frikiki ya Dimitri Payet kuunganishwa na Diafra Sakho na kuwapa Bao.

Man United walitulia na kukontroli Gemu na kusawazisha Bao Dakika ya 21 kufuatia muvu ya Pasi 22 ikiguswa na kila Mchezaji wa Man United na kisha kumfikia Paul Pogba na kummiminia Zlatan Ibrahimovic aliefunga kwa Kichwa.

Mabao hayo yalidumu hadi Haftaimu lakini matukio makubwa katika Kipindi cha Kwanza hicho ni Paul Pogba kupewa Kadi ya Njano na Refa Jon Moss kwa madai ya kujiangusha na Kadi hiyo kumfanya Pogba sasa apate Kifungo cha Mechi 1 kwa kuwa amezoa Kadi za Njano 5 na ataikosa Mechi ifuatayo Jumatano ya EFL CUP dhidi ya hao hao West Ham Uwanjani Old Trafford.

Tukio hilo lilimkasirisha sana Jose Mourinho na kuibutua Chupa ya Maji kwenye Eneo lake la Ufundi na Refa Moss kumtoa Uwanjani aende Jukwaani kwa Watazamaji akimwacha Msaidizi wake Lui Faria kukaimu.

+++++++++++++

JE WAJUA?

-Refa Jon Moss ashawahi kumtoa nje Jose Mourinho akae Jukwaani wakati ni Meneja wa Chelsea.

-Mourinho alimkabili tena Refa huyo Siku hiyo hiyo na FA kumfungia kukanyaga Uwanjani.

-Refa Jon Moss ameichezesha Man United Mechi 13 na kushinda 11 na Sare 2

+++++++++++++

Mechi inayofuata ya EPL kwa Man United ni Ugeni huko Goodison Park dhidi ya Everton ambao Leo walichapwa 1-0 huko Saint Mary EPL-NOV27Ckwa Bao la Sekunde ya 43 tu la Charlie Austin walipocheza na Southampton.

VIKOSI:

Manchester United: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Herrera, Pogba, Mata, Lingard, Ibrahimovic, Rashford

Akiba: Romero, Blind, Fellaini, Schweinsteiger, Mkhitaryan, Young, Rooney

West Ham: Randolph, Ogbonna, Collins, Kouyate, Antonio, Obiang, Noble, Cresswell, Lanzini, Payet; Sakho

Akiba: Adrian, Nordtveit, Feghouli, Zza, Ayew, Fletcher, Fernandes

REFA: Jon Moss

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Desemba 3

1530 Manchester City v Chelsea      

1800 Crystal Palace v Southampton          

1800 Stoke City v Burnley              

1800 Sunderland v Leicester City              

1800 Tottenham Hotspur v Swansea City             

1800 West Bromwich Albion v Watford                

2030 West Ham United v Arsenal              

Jumapili Desemba 4

1630 Bournemouth v Liverpool                

1900 Everton v Manchester United            

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City       

         

LIGI KUU ENGLAND: VICTOR MOSES AIPA USHINDI CHELSEA, WATWAA TENA UONGOZI!

>LEO EMIRATES ARSENAL-BOURNEMOUTH, OLD TRAFFORD NI MAN UNITED-WEST HAM!

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Matokeo:

Jumamosi Novemba 26

CHE-SPUBurnley 1 Manchester City 2           

Hull City 1 West Bromwich Albion 1           

Leicester City 2 Middlesbrough 2               

Liverpool 2 Sunderland 0               

Swansea City 5 Crystal Palace 4                

Chelsea 2 Tottenham Hotspur 1

+++++++++++++++++++++++++++++

BAADA ya uongozi wa EPL, Ligi Kuu England, kupokezana hapo Jana kwa mapema Man City kuutwaa, kisha Liverpool kuwa wao na hatimae mwishoe waliokuwa Vinara wake Chelsea kurejea tena kileleni baada ya kuifunga Tottenham 2-1 huko Stamford Bridge.

Kipigo hiki cha Spurs ni cha kwanza kwenye EPL Msimu huu na kufuta ile rekodi yao ya kuwa Timu pekee ambayo ilikuwa haijafungwa kwenye Ligi hiyo inayosifika kuwa ngumu na isiyotabirika Duniani.

Ushindi huo umehakikisha Spurs kutoifunga Chelsea Uwanjani Stamford tangu Februari 1990 na ulikuja kwa Bao la EPL-NOV27AVictor Moses, Mchezaji kutoka Nigeria, aliefunga kwa Shuti la chini katika Dakika ya 51.

Spurs ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 11 kufuatia kazi njema ya Moussa Dembele, Dele Alli na Mpira kumfikia Christian Eriksen alieachia kigongo cha mbali na kutinga.

++++++

JE WAJUA?

-Chelsea hawajafungwa na Tottenham Uwanjani Stamford Bridge katika Mechi 30.

-Mara ya mwisho Chelsea kufungwa Stamford Bridge na Spurs ni Februari 1990.

++++++

Chelsea walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Shuti la Pedro na Gemu kwenda Mapumziko ikiwa ni 1-1.

Baada Mechi 13, Chelsea sasa wanaongoza EPL wakiwa na Pointi 31 wakifuata Liverpool na City zenye 30 kila moja na Timu ya 4 ni Arsenal yenye Pointi 25 kwa Mechi 12.

Hii Leo zipo Mechi 4 za EPL lakini macho ni huko Emirates Arsenal wakicheza na Bournemouth na huko Old Trafford wakati Man United wakikipiga na West Ham United.

VIKOSI:

Chelsea: Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses, Kante, Matic, Alonso, Pedro, Costa, Hazard.

Akiba: Begovic, Ivanovic, Fabregas, Oscar, Willian, Batshuayi, Chalobah.

Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Wimmer, Vertonghen, Walker, Wanyama, Dembele, Son, Eriksen, Alli, Kane.

Akiba: Janssen, Vorm, Nkoudou, Trippier, Onomah, Winks, Carter-Vickers.
REFA:Michael Oliver

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumapili Novemba 27

1500 Watford v Stoke City             

1715 Arsenal v Bournemouth         

1930 Manchester United v West Ham United         

1930 Southampton v Everton         

Jumamosi Desemba 3

1530 Manchester City v Chelsea      

1800 Crystal Palace v Southampton          

1800 Stoke City v Burnley              

1800 Sunderland v Leicester City              

1800 Tottenham Hotspur v Swansea City             

1800 West Bromwich Albion v Watford                

2030 West Ham United v Arsenal              

Jumapili Desemba 4

1630 Bournemouth v Liverpool                

1900 Everton v Manchester United            

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City       

         

LIGI KUU ENGLAND: JUMAMOSI BURNLEY-CITY KUANZA, CHELSEA-SPURS KUMALIZA!

>>JUMAPILI: ARSENAL-BOURNEMOUTH, MAN UNITED-WEST HAM!

CHE-SPUEPL, Ligi Kuu England,ipo tena dimbani na Jumamosi zipo Mechi 6 lakini Bigi Mechi ni ile ya Stamford Bridge kati ya Wenyeji Chelsea na Tottenham Hotspur.

Mechi ya Kwanza Jumamosi ni kati ya Burnley na Manchester City na hiyo ni nafasi safi kwa City kutwaa uongozi wa EPL kutoka Nafasi ya 3 dhidi ya Burnley ambayo ipo ya 12.

Wakishinda, City watakuwa na Pointi 30 na kuwazidi Vinara Chelsea ambao wana Pointi 27 na wanacheza baadae hiyo Jumamosi, ikiwa ni Mechi ya mwisho ya Siku hiyo, kwenye Dabi ya Jiji la London dhidi ya Spurs ambao wako Nafasi ya 5 na wana Pointi 24.

Kati ya Mechi hizo za Kwanza na za Mwisho hiyo Jumamosi zipo Mechi 4 na moja ni ile ya huko Anfield ambapo Liverpool, ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 27, watacheza na Sunderland ambao wako Nafasi ya Pili toka mkiani.EPL-NOV26

Jumapili zipo Mechi 4 lakini macho ya Wadau wengi ni huko Emirates Jijini London na Old Trafford Jijini Manchester wakati Arsenal, walio Nafasi ya 4, watacheza na Bournemouth walio Nafasi ya 10 huku Man United, ambao ni wa 6, wataivaa Timu ya 17 West Ham United.

EPL - LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Novemba 26

1530 Burnley v Manchester City               

1800 Hull City v West Bromwich Albion                

1800 Leicester City v Middlesbrough          

1800 Liverpool v Sunderland          

1800 Swansea City v Crystal Palace           

2030 Chelsea v Tottenham Hotspur           

Jumapili Novemba 27

1500 Watford v Stoke City             

1715 Arsenal v Bournemouth         

1930 Manchester United v West Ham United         

1930 Southampton v Everton         

Jumamosi Desemba 3

1530 Manchester City v Chelsea      

1800 Crystal Palace v Southampton          

1800 Stoke City v Burnley              

1800 Sunderland v Leicester City              

1800 Tottenham Hotspur v Swansea City             

1800 West Bromwich Albion v Watford                

2030 West Ham United v Arsenal              

Jumapili Desemba 4

1630 Bournemouth v Liverpool                

1900 Everton v Manchester United            

Jumatatu Desemba 5

2300 Middlesbrough v Hull City                

STEVEN GERRARD ASTAAFU SOKA!

STEVEN-GERRARDNAHODHA wa zamani wa Liverpool na England Steven Gerrard ametangaza rasmi kustaafu kucheza Soka la Kulipwa.

Gerrard alianza Soka lake huko Liverpool tangu Utoto wake na kuibuka kuwa Kepteni wao wa muda mrefu kabisa katika Historia ya Klabu ambayo aliichezea Mechi 710 na kuiwezesha kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mwaka 2005 pamoja na FA CUP mara 2 Miaka ya 2001 na 2006, Kombe la Ligi mara 3, Miaka ya 2001, 2003 na 2012 na UEFA CUP 1 Mwaka 2001 katika himaya yake ya Miaka 18 huko Anfield.

Kwenye Timu ya Taifa ya England, Gerrard aliichezea Mechi 114 na yeye ni Mchezaji wa 4 wa Nchi hiyo kuichezea Mechi nyingi akitanguliwa tu na Peter Shilton, Wayne Rooney na David Beckham.

Gerrard aliiongoza England kama Nahodha kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 na 2014 na pia EURO 2012.

Baada ya kuacha kuichezea Liverpool, Gerrard alihamia huko USA Mwaka 2015 kwenda kuichezea Klabu ya LA Galaxy na sasa, akiwa na Miaka 36, ameamua kabisa kustaafu Soka.

IBRAHIMOVIC KUONGEZEWA MWAKA 1 ZAIDI MAN UNITED!

MANUNITED-IBRA-SHUJAAZlatan Ibrahimovic huenda akaongezewa Mkataba wa Mwaka Mmoja zaidi huko Manchester United.

Meneja wa Vigogo hao wa England Jose Mourinho ametoboa kuwa Man United itatumia kipengele cha uwezo wao kumwongeze Mchezaji huyo wa Sweden Mwaka mwingine mmoja baada ya Mkataba wake kumalizika mwishoni mwa Msimu huu Mwezi Juni Mwakani.

Ibrahimovic, mwenye Miaka 35, alihamia Old Trafford kama Mchezaji Huru Mwezi Julai baada ya Mkataba wake na Paris Saint-Germain ya France kumalizika na kusaini kwa Mwaka Mmoja na Man United huku kukiwa na Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja.

Akiongea na Wanahabari kuhusiana na Mechi yao ya Alhamisi Usiku ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI dhidi ya Feyenoord Uwanjani Old Trafford, Mourinho alitamka: “Mambo ni rahisi kuhusu Zlatan. Anayo 1 jumlisha 1. Tuna furaha na yeye. Tutatumia nyongeza ya Mwaka Mmoja mwishoni mwa Msimu. Baada ya hapo atafanya analotaka.”

Akiichezea Man United, Ibrahimovic amefunga Bao 8 katika Mechi 17 alizocheza.

Akigusia uwezekano wa kubakia Old Trafford kwa Msimu wa 2017/18, mwenyewe Gwiji huyo wa Sweden amesema yeye atabaki tu ikiwa ataona anastahili kubakia.

Ibrahimovic ametwaa Mataji 11 ya Ligi katika Nchi 4 na kuweka Rekodi ya Magoli kwa kuifungia Nchi yake Sweden Mabao 62 katika Mechi 116.

Hivi sasa amestaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Sweden tangu Mwezi Juni walipotupwa nje ya EURO 2016.