UEFA EUROPA LIGI: MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI!

>KRC GENK YA SAMATTA NAYO IPO ROBO FAINALI, DROO BAADAE LEO!

MANUNITED-ROSTOVManchester United imetinga Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI baada ya kuifunga FC Rostov 1-0 katika Mechi ya Pili iliyochezwa Old Trafford Jijini Manchester.

Katika Kipindi cha Kwanza Man United walitawala chote na mara mbili Zlatan Ibrahimovic kupiga Posti na Henrikh Mkhitaryan kupoteza nafasi ya wazi akiwa uso kwa uso na Kipa Medvedev.

Hadi Haftaimu Man United 0 FC Rostov 0.

Bao la ushindi la Man United lilifungwa Dakika ya 70 na Juan Mata baada ya Man United kuunasa Mpira katikati ya Uwanja na kupigwa Pasi pembeni Kulia kwa Mkhitaryan aliemwingizia Ibrahimovic alietoa Pasi ya Kisigino kwa Mata na kufunga Bao safi.

Man United sasa wametinga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 2-1 baada ya Sare ya 1-1 kwenye Mechi ya Kwanza.

+++++++++++++++++++

Robo Fainali – Timu zilizofuzu:

-Besiktas                            

-Celta Vigo

-KRC Genk

-Man United

-Schalke

-Lyon

-Anderlecht

-Ajax

+++++++++++++++++++

Huko Belgium, Klabu ya Staa wa Tanzania, Mbwana Samatta, KRC Genk imesonga Robo Fainali baada ya Sare ya 1-1 na Mahasimu wao wa Nchini KAA Gent na wao kufuzu kwa Jumla ya Bao 6-3.

Bao la Genk lilifungwa na Castagne Dakika ya 20 na Gent kusawazisha Dakika ya 84 kupitia Verstraete,

Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali itafanyika Saa 9 Mchana hii Leo huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA.

Mechi za Robo Fainali zitachezwa Aprili 13 na Marudio ni Aprili 20.

VIKOSI:

MAN UNITED: Romero; Bailly, Smalling, Rojo; Valencia, Pogba [Fellaini 48'], Herrera, Mata, Blind [Jones 63’], Mkhitaryan, Ibrahimovic

Akiba: De Gea, Jones, Lingard, Carrick, Young, Rashford, Fellaini

FC ROSTOV: Medvedev; Bayramyan [Kireev 82'], Mevlja, Navas, Kudryashov, Terentyev; Noboa, Prepelita [Devicat 79’], Erokhin; Poloz, Azmoun [Bukharov 61’]

Akiba: Goshev, Kireev, Bukharov, Devic

REFA: Gediminas Mazeika (Lithuania)

EUROPA LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16 – Mechi za Pili

Ahamisi Machi 16

***Kwenye Mabano Mabao kwa Mechi 2

Besiktas 4 Olympiakos 1 (5-2)

FK Krasnodar 0 Celta Vigo 2 (1-4)

KRC Genk 1 KAA Gent 1 (6-3)

Ajax 2 FC Copenhagenb 0 (3-2)

Borussia Mönchengladbach 2 FC Schalke 2 (3-3, Schalke wasonga Bao za Ugenini)

Manchester United 1 FC Rostov 0 (2-1)

Roma 2 Lyon 1 (4-5)

RSC Anderlecht 1 Apoel Nicosia 0 (2-0)

+++++++++++++++++++++++++++++

UEFA EUROPA LIGI

Tarehe Muhimu:

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza

20/04/17: Robo Fainali, Mechi za Pili

04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

FAINALI

24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden

UEFA EUROPA LIGI: ALHAMISI MAN UNITED KUIFYEKA FC ROSTOV? SHUJAA WA TANZANIA MBWANA SAMATTA KUWINI ‘VITA’ YA WABELGIJI KRC GENK NA KAA GENT?

MANUNITED-ROSTOVMechi za Pili za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI zitachezwa Alhamisi na mvuto mkubwa ni huko Old Trafford Jijini Manchester, England na kule Fenix Stadion Jijini Genk, Belgium.

Huko Old Trafford, Manchester United, baada ya kupata Sare 1-1 huko Rostyov Wiki iliyopita kwenye Uwanja mbovu ambao sasa umefungiwa, watarudiana tena na FC Rostov wakihitaji Sare ya 0-0 au ushindi ili kutinga Robo Fainali.

Meneja wa Man United, Jose Mourinho, amesema licha ya kulazimika kucheza mfululizo na hasa Jumatatu Usiku walipotolewa 1-0 kwenye FA CUP na Chelsea Kikosi chake ki tayari ingawa kitawakosa Majeruhi Kepteni wao Wayne Rooney na Anthony Martial.

Lakini habari njema kwao ni kurejea Kikosini kwa Mfungaji wao mkubwa Zlatan Ibrahimovic alieikosa Mechi ya Chelsea kutokana na kuwa Kifungoni Mechi 3.

Kifungo hicho ni kwa Mechi za England tu na hakihusiana na Mechi za Ulaya,

Wiki iliyopita, wakiwa Ugenini kwa Mahasimu wao wa Nchini kwao Belgium, KRC Genk iliichapa KAA Gent 5-2 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi hii huku Shujaa wa Tanzania, Mbwana Samatta, akipiga Bao 2.

Safari hii, Mechi ya Marudianio ipo Nyumbani kwa KRC Genk, Fenix Stadion Jijini Genk, ambao wanatarajia matokeo mema ili kutinga Robo Fainali.

Droo za Robo Fainali zitafanyika Ijumaa.

UEFA EUROPA LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Mechi za Kwanza [Marudiano Machi 16]

Matokeo:

EUROPA LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 16 – Mechi za Pili

Ahamisi Machi 16

**Saa za bongo

***Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwnza

2100 Besiktas v Olympiakos (1-1)

2100 FK Krasnodar v Celta Vigo (1-2)

2100 KRC Genk v KAA Gent (5-2)

2305 Ajax v FC Copenhagen (1-2)

2305 Borussia Mönchengladbach v FC Schalke 04 (1-1)

2305 Manchester United v FC Rostov (1-1)

2305 Roma v Lyon (2-4)

2305 RSC Anderlecht v Apoel Nicosia (1-0)

+++++++++++++++++++++++++++++

UEFA EUROPA LIGI

Tarehe Muhimu:

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza

20/04/17: Robo Fainali, Mechi za Pili

04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza

11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili

FAINALI

24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden

MAN UNITED YASHITAKIWA NA FA, ROJO APONA!

MANUNITED-MOU-MAJIManchester United wamefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kushindwa kudhibiti Wachezaji wao huko Stamford Bridge Juzi walipofungwa 1-0 na Chelsea na kutolewa nje ya FA CUP kwenye Mechi hiyo ya Robo Fainali.
Shitaka hilo linatokana na Wachezaji wa Man United kumzonga Refa Michael Oliver alipoamua kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu Kiungo wao Ander Herrera katika Dakika ya 35.
Herrera alitolewa baada ya kupewa Kadi za Njano 2 ambazo Meneja wao Jose Mourinho amedokeza hazikustahili na pia 'kumtuhumu' Refa Oliver 'kuiwinda' Man United kwa kutoa Penati 3 na Kadi Nyekundu 1 dhidi yao Msimu huu.
Kwenye Mechi 3 za Ligi Kuu England Refa Oliver alizoichezesha Man United Msimu huu, zile walizofungwa na Watford na sare na Liverpool na Everton, zote Refa Oliver alitoa Penati dhidi yao.
FA imeipa Man United hadi Saa 3 Usiku Ijumaa kujibu Shitaka lao.
Kawaida kosa kama hili huadhibiwa kwa Faini.
Wakati huo huo Refa Michael Oliver 'amemwokoa' Beki wa Man United Marcos Rojo kukumbana na Shitaka la FA baada kuonekana akimtimba Kifuani Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard kwenye Mechi hiyo ya. Juzi.
Imebainika Refa Oliver ameliingiza tukio hilo kwenye Ripoti yake ya Mechi na kusema alichukua hatua stahiki na hivyo kuibana FA kutofungua Mashitaka.
Laiti kama Refa Oliver asingelibaini tukio hilo kwenye Ripoti basi FA ingekuwa huru kumshitaki Rojo.
 
 

EMIRATES FA CUP: CHELSEA YAWATOA MABINGWA MAN UNITED, KUCHEZA NUSU FAINALI NA SPURS

FACUP-CHE-MUNJana Chelsea wakiwa kwao Stamford Bridge waliwafunga Mabingwa Watetezi.Manchester United 1-0 na kutinga Nusu Fainali ambako watacheza na Mahasimu wao wa London Tottenham Hotspur.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Arsenal na Manchester City.
Mechi zote za Nusu Fainali zitachezwa Wembley Jijini London hapo Aprili 22 na 23.
Katika Robo Fainali ya mwisho iliyochezwa Jana, Bao la N'Golo Kante la Dakika ya 51  liliwapa Chelsea ushindi wa 1-0 kwenye Mechi ambayo Man United walicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 35 kufuatia Kiungo wao Ander Herrera kupewa Kadi za Njano 2 tata na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu. 
FA CUP
Ratiba
Raundi ya 6 [Robo Fainali]
**Saa za Bongo
Jumamosi Machi 11
Middlesbrough 0 Man City 2
Arsenal 5 Lincoln City 0    
Jumapili Machi 12
Tottenham Hotspur 6 Millwall 0
Jumatatu Machi 13
Chelsea 1 Manchester United 0

EMIRATES FA CUP – TATHMINI – LEO VINARA WA LIGI CHELSEA NA MABINGWA WATETEZI MANCHESTER UNITED

FACUP-CHE-MUNJUMATATU Usiku Jose Mourinho anarejea tena Stamford Bridge Jijini London kwa mara ya Pili akiwa Meneja wa Manchester United kuiongoza Timu yake hiyo kuikwaa Timu yake ya zamani Chelsea kwenye Mechi ya Robo Fainali ya FA CUP ambayo wao ndio Mabingwa Watetezi.

Safari hii jambo jipya kwa Mechi hii ya Mashindano haya ni kuwa kuanzia Hatua hii ya Robo Fainali hamna tena Marudiano ikiwa Timu zitatoka Sare katika Dakika 90 na hivyo upo uwezekana wa Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 na pia kupigwa Mikwaju ya Penati Tano Tano ili tu kupata Mshindi hiyo hiyo Jumatatu Usiku.

Vile vile, mabadiliko mengine ni kuwa kila Timu ipo ruksa kuingiza Mchezaji wa Nne kutoka Benchi ikiwa tu Mechi hiyo itafikia Dakika za Nyongeza 30.

Mechi kwa hii kwa Man United hasa tu kwa vile Alhamisi Usiku walikuwa huko Urusi kucheza na FC Rostov katika Mechi ya UEFA EUROPA LIGI na sasa wamesafiri tena kwenda Jijini London.

Vile vile, mara ya mwisho kwa Timu hizi kukutana Chelsea iliitwanga Man United 4-0 kwenye Mechi ya Ligi lakini tangu wakati huo Man United wameselelea kwenye wimbi la kutofungwa kwenye Ligi hata mara moja.

+++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-FA CUP 2016/17, ambalo pia hujulikana kama FA Challenge Cup, ni mara ya 136 kushindaniwa kila Mwaka tangu lilipoanzishwe na linatambuliwa kama ndio Mashindano ya kale kupita yote Duniani.

-Kombe hili linadhaminiwa na Kampuni ya Ndege ya Emirates na kwa sababu za kiudhamini linaitwa Emirates FA Cup.

-Timu 736 zilikubaliwa kushiriki Mashindano haya Msimu huu na yalianza kwa Raundi ya Awali na yatafikia Tamati kwa Fainali itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London hapo Mei 27, 2017.

-Mshindi wa FA CUP ataingizwa Hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI Msimu wa 2017/18.

-Bingwa Mtetezi ni Manchester United.

KUANZIA MSIMU HUU – KUANZIA Robo Fainali:

-Hamna Marudiano ikiwa Timu zipo Sare baada ya Dakika 90. Sare itafuatia Dakika za Nyongeza 30 na kama Gemu bado Sare, zitafuatia Penati ili kupata Mshindi.

-Kila Timu inaruhusiwa kubadili Wachezaji si zaidi ya Wanne lakini huyo wa Nne ni pale tu Gemu ipo Dakika za Nyonfeza 30.

+++++++++++++++++++

Kwa Chelsea, tangu wafungwe na Tottenham katika Mechi yao ya kwanza ya Mwaka 2017 hawajafungwa tena katika Mechi 10 na pia tangu Meneja wao Antonio Conte aanze kibarua wamefungwa mara 1 tu Uwanjani kwao Stamford Bridge na hiyo ilikuwa ni Septemba walipocheza na Liverpool.

Kwenye FA CUP, Man United na Chelsea zimevaana mara 13 na Man United kushinda mara 8, Sare 2 na Kufungwa 3.

Kila Timu inatarajiwa kuwa na Kikosi chao kamili lakini Man United wana pigo kubwa la kumkosa Mfungaji wao Bora Zlatan Ibrahimovic ambae ataanza Kifungo cha Mechi 3 kuanzia Mechi hii.

Tegemezi kubwa la Chelsea na tishio lao kubwa ni Mafowadi wao Eden Hazard na Diego Costa huku Kiungo wao N'Golo Kante ndio Kiungo Mkabaji wao akisimama imara kuilima Difensi yao ya Mtu 3 kwenye Mfumo wao 3-4-3 ambao umewapa mafanikio makubwa tangu wauanze walipocharazwa 3-0 Mwezi Septemba Mwaka Jana.

+++++++++++++++++++

Uso kwa Uso:

Ushindi:

-Chelsea 44 Man United 59 Sare 46

+++++++++++++++++++

Mshindi wa Mechi hii ataungana na Man City, Arsenal na Tottenham ambazo tayari zimetinga Nusu Fainali na Droo ya kupanga Mechi hizo za Nusu Fainali itafanywa Jumatatu Usiku mara baada ya kumalizika kwa Mechi kati ya Chelsea na Man United.

Mechi za Nusu Fainali zote zitafanyika Uwanjani Wembley Jijini London hapo Aprili 22 na 23.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

CHE-MUN-VIKOSI

REFA: Michael Oliver

FA CUP

Ratiba

Raundi ya 6 [Robo Fainali]

**Saa za Bongo

Jumamosi Machi 11

Middlesbrough 0 Man City 2

Arsenal 5 Lincoln City 0    

Jumapili Machi 12

Tottenham Hotspur 6 Millwall 0

Jumatatu Machi 13

2245 Chelsea v Manchester United