HERNANDEZ AFUNGIWA, CHICHARITO CHAMBO!

290C5A4B00000578-0-image-m-4 1432642828351Wakati Abel Hernandez wa Hull City akifungiwa Mechi 3 kwa kumtandika ngumi Phil Jones wa Manchester United, Javier Hernandez 'Chicharito' wa Manchester United  amebaki njia panda baada Real Madrid alikokuwa kwa Mkopo kukataa kumchukua kwa kudumu.
FA, Chama cha Soka England, Leo hii kimethibitisha kufungiwa Mechi 3 kwa Mchezaji wa Hull City Timu iliyoshuka Daraja toka Ligi Kuu England, Abel Hernandez, kwa kumpiga ngumi Beki wa Man United, Phil Jones, katika Dakika ya 70 ya Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England ambayo ilimalizika 0-0 na kuthibitisha Hull kushuka Daraja baada ya Newcastle kuicharaza West Ham 2-0 na kunusurika kushuka.
Tukio hilo la ngumi ya Hernandez halikuonwa na Refa lakini lilinaswa kwenye Video na FA kumfungulia Mashitaka na Mchezaji huyo kutoka Uruguay kukiri kosa na sasa atatumikia adhabu yake Msimu ujao akiwa Daraja la chini la Championship.
Nae Mchezaji wa Man United kutoka Mexico, Javier Hernandez 'Chicharito', amerudishwa kutoka Real Madrid alikokuwa kwa Mkopo Msimu uliopita baada ya Miamba hiyo ya Spain kukataa kutumia nafasi yao ya kumchukua moja kwa moja.
Lakini hata huko Man United inadaiwa Chicharito hatakaa kwani Meneja Louis van Gaal anatarajiwa kumtumia kama chambo ili kunawasa Mastaa anaowawinda yeye.
Inasemekana Van Gaal anaamini rekodi ya Chicharito ya kupiga Bao 5 katika Mechi zake 11 alizocheza mwisho na Real kutamfungulia Soko la kupata Timu haraka na yeye kupata upenyo kumnasa Mchezaji anaemtaka. 
 
 
 

EDDIE HOWE-NDIE MENEJA BORA ENGLAND, MOURINHO NI WA LIGI KUU TU!

EDIEHOWE-BOURNEMOUTHMeneja wa Bournemouth, Eddie Howe, ndie Meneja Bora wa Mwaka kwa mujibu wa Chama cha Mameneja wa Ligi huko England, LMA (League Managers Association).

Howe, Miaka 37, ametunukiwa Tuzo hiyo Jana Usiku katika Hafla maalum baada ya kuiongoza Bournemouth kushinda Ubingwa wa Ligi wa Daraja la Championship na kupanda Daraja kuingia Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza katika Historia ya Klabu hiyo.

Vile vile, Howe alitwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka wa Daraja la Championship wakati Jose Mourinho alitwaa ile ya Meneja Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu England baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa Ubingwa wa Ligi hiyo kwa mara ya kwanza katika Miaka Mitano.

Howe amekuwa Meneja wa pili nje ya Ligi Kuu England kutwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Mwaka wa England kufuatia Steve Coppell, aliekuwa Reading, kuitwaa Mwaka 2006.

Pamoja na Bournemouth, Timu nyingine zilizopanda Daraja kuingia Ligi Kuu England Msimu ujao ni Watford na Norwich City ambazo zinachukua nafasi za Hull City, QPR na Burnley zilizoshuka Daraja.

MABINGWA CHELSEA WAZUNGUSHA KOMBE MITAA YA LONDON MAGHARIBI!

CHELSEA-PAREDI15
Mabingwa wapya wa England, Chelsea, Leo wamezunguka Mitaa ya London ya Magharibi wakiwa juu ya Basi la Ghorofa la wazi wakiwa na Kombe lao la Ubingwa wa Ligi Kuu England pamoja na Vikombe vingine Vitatu ambavyo Klabu hiyo ilitwaa Msimu huu.
Chelsea wametwaa Ubingwa huu wa England kwa mara ya kwanza baada ya Miaka Mitano.
Baada ya Jana kukabidhiwa Kombe la Ubingwa na kufanya sherehe Usiku kucha Leo wamezungukana Mitaa ya London huku Washabiki wakisimama kando kando na kuwashangilia.
Juu ya Basi hilo la Ghorofa la wazi walikuwemo Wachezaji wa Timu ya Kwanza ya Chelsea wakiwa na Kombe la Ligi Kuu England na lile la Capital One Cup pamoja na wa Timu ya Vijana ambao nao walikuwa na Kombe la Vijana la FA na lile la Vijana la Ligi ya UEFA.
 
 

LIGI KUU ENGLAND: HULL YASHUKA, NEWCASTLE YABAKI!

MATOKEO:
Jumapili Mei 24
Arsenal 4 West Brom 1
Aston Villa 0 Burnley 1
Chelsea 3 Sunderland 1
Crystal Palace 1 Swansea 0
Everton 0 Tottenham 1
Hull 0 Man United 0
Leicester 5 QPR 1
Man City 2 Southampton 0
Newcastle 2 West Ham 0
Stoke 6 Liverpool 1
++++++++++++++++++++++++++
Newcastle 2 West Ham 0
BPL-2014-2015-LOGO-POABao za Kipindi cha Pili za Moussa Sissoko  na Jonas Gutierrez zimewapa Newcastle  ushindi wa 2-0 walipocheza na West Ham Uwanjani Saint James Park na kujihakikishia kubaki Ligi Kuu England huku Hull City wakishushwa kuungana na Burnley na QPR kucheza Daraja la chini la Championship Msimu ujao.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Janmaat, Williamson, Coloccini, Dummett, Colback, Anita, Riviere, Sissoko, Gutierrez, Cisse
Akiba: Ryan Taylor, De Jong, Gouffran, Perez, Cabella, Ameobi, Woodman. 
West Ham: Adrian, Reid, Jenkinson, Burke, Cresswell, Song, Nolan, Valencia, Kouyate, Downing, Cole
Akiba: Tomkins, Jarvis, Nene, O’Brien, Amalfitano, Jaaskelainen, Lee. 
REFA: Martin Atkinson
++++++++++++++++++++++++++
Hull 0 Manchester United 0
Hull City Leo imekuwa Timu ya 3 kuungana na Burnley na QPR kushushwa Daraja baada ya kutoka 0-0 na Man United Uwanjani KC Stadium.
Wakihitaji ushindi na kuomba Newcastle wasishinde, Hull City, chini ya Meneja wao Steve Bruce ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United ambae hajawahi kuifunga Timu yake ya akiwa kama Meneja katika Mechi 20, ameendeleza Rekodi yake hiyo huku Newcastle wakiifunga West Ham 2-0 na kubakia Ligi Kuu England.
Katika Mechi hii, Man United walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 77 baada ya Marouane Fellaini, ambae aliingizwa Dakika ya 59 kumbadili Ashley Young, kupewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu mbaya Paul McShane.
VIKOSI:
Hull: Harper, Chester, Dawson, McShane, Elmohamady, Meyler, Huddlestone, Quinn, Brady, N’Doye, Jelavic
Akiba: McGregor, Rosenior, Bruce, Hernandez, Sagbo, Aluko, Robertson. 
Man Utd: Valdes, Valencia, Smalling, Jones, Rojo, Blind, Mata, Ander Herrera, Di Maria, Young, Rooney
Akiba: Januzaj, Lindegaard, van Persie, Fellaini, McNair, Blackett, Wilson. 
REFA: Lee Probert
 

LIGI KUU ENGLAND MWISHO JUMAPILI, HULL AU NEWCASTLE NANI KUSHUKA?

BPL-2014-2015-LOGO-POALIGI KUU ENGLAND inafunga Msimu wake wa 2014/15 hapo Jumapili kwa Timu zote 20 kuwa dimbani kwa wakati mmoja kuanzia Saa 11 Jioni kucheza Mechi zao 10 za mwisho.
Tayari Bingwa ameshapatika, ambae ni Chelsea, na nyingine 3 zinazofuatia zitakazocheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao zimeshapatikana na hizo ni Man City, Arsenal na Man United.
Pia, Timu 2 kati ya 3 ambazo zitashuka Daraja kucheza Ligi ya Championship Msimu ujao zimepatikana na hizo ni Burnley na QPR na Timu ya 3 kuungana nao itapatikana hiyo Jumapili na ni moja kati ya Newcastle au Hull City.
Hull, ambao wako Nafasi ya 3 toka mkiani wako Pointi 2 nyuma ya Newcastle lakini Hull wana tofauti ya Magoli Bora kupita Newcastle.
Kila Timu inahitaji ushindi hiyo Jumapili maana ikiwa Newcastle itatoka Sare na West Ham watakapocheza Uwanjani Saint James Park, Nyumbani kwa Newcastle, na Hull City, ambao wako Nyumbani KC Stadium, wakiifunga Man United, licha ya sasa kufungana Pointi, basi Hull watapona na Newcastle kushushwa.
Timu zote hizo, Hull na Newcastle, zinacheza na Wapinzani ambao hawana cha maana kwenye Mechi zao mbali ya kukamilisha Ratiba tu.
Lakini Steve Bruce, Meneja wa Hull ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United, anajua fika nini ugumu wa kuifunga Man United maana katika Mechi 21 alizocheza dhidi ya Man United katika Miaka 17 ya kazi yake ya Umeneja hajawahi kuifunga Man United hata mara moja.
++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO-Timu za Mkiani:
**Mechi zilizochezwa/Tofauti ya Magoli/Pointi 
16 Aston Villa 37/-25/38
17 Newcastle 37/-25/36
----------------------------
18 Hull 37/-18/34
19 Burnley 37/-26/30
20 QPR 37/-27/30
++++++++++++++++++++++++
Hull na Newcastle zinatinga kwenye Mechi zao muhimu za mwisho zikiwa kwenye mwendo mbovu kabisa.
Baada kuzifunga Crystal Palace na Liverpool, Hull imepoteza Mechi 3 mfululizo na Newcastle imepoteza Mechi 9 kati ya 10 walizocheza mwisho.
Tangu John Carver ashike wadhifa kama Meneja wa Newcastle mwanzoni mwa Mwaka baada ya Alan Pardew kutimkia Crystal Palace, Meneja huyo ameshinda Mechi 2 tu na moja ni Januari 31 walipoitwanga Hull Bao 3-0.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumapili Mei 24
**Mechi za Mwisho
[Mechi zote kuanza Saa 11 Jioni]
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Burnley
Chelsea v Sunderland
Crystal Palace v Swansea
Everton v Tottenham
Hull v Man United
Leicester v QPR
Man City v Southampton
Newcastle v West Ham
Stoke v Liverpool
MSIMAMO:
**Mechi zilizochezwa/Tofauti ya Magoli/Pointi
1 Chelsea 37/39/84
2 Man City 37/43/76
3 Arsenal 37/32/72
4 Man United 37/25/69
----------------------------
5 Liverpool 37/9/62
6 Tottenham 37/4/61
7 Southampton 37/23/60
8 Swansea 37/-2/56
9 Stoke 37/-2/51
10 Everton 37/-1/47
11 West Ham 37/-1/47
12 Crystal Palace 37/-5/45
13 WBA 37/-10/44
14 Leicester 37/-13/38
15 Sunderland 37/-20/38
16 Aston Villa 37/-25/38
17 Newcastle 37/-25/36
----------------------------
18 Hull 37/-18/34
19 Burnley 37/-26/30
20 QPR 37/-27/30