MABINGWA WAPYA CHELSEA WATWANGANA 4-3 NA WATFORD

=LEO ARSENAL-SUNDERLAND, CITY-WBA!
CHELSEA17-BINGWAMABINGWA WAPYA Chelsea wamesherehekea Ubingwa wao mpya wa EPL, LIGI KUU ENGLAND, wakicheza kwa mara ya kwanza Uwanjani kwao Stamford Bridge tangu waubebe Ubingwa kwa kutwangana 4-3 na Watford katika Mechi ya kukamilisha Ratiba kwao.
Mwishoni mwa Mechi hiyo Meneja Antonio Conte na Wachezaji wake walizunguka Uwanja kushukuru Mashabiki wao huku wakishangiliwa.
Kepteni John Terry, ambae anastaafu mwishoni mwa Msimu huu baafa ya Utumishi wa Miongo Miwili, ndie alieifungia Chelsea Bao la Kwanza likiwa ni Bao la 100 kwa Chelsea Msimu huu.
Lakini Terry alifanya makosa na kuruhusu Watford kusawazisha kupitia Etienne Capoue.
Cesar Azpilicueta akaipeleka Chelsea 2-1 mbele kabla Haftaimu na mara tu baada Kipindi cha Pili kuanza Michy Batshuayi, ambae Juzi ndie aliefunga Bao la ushindi Chelsea ikiichapa West Brom 1-0 na kutwaa Ubingwa, akapiga Bao la 3 na Chelsea kuongoza 3-1.
Watford wakaja juu na kupata Bao lao la Pili lililofungwa na Daryl Janmaat na kisha Stefano Okaka, Mchezaji 'alievumbuliwa' na Antonio Conte huko Italy, akaisawazishia Watford.
Hata hivyo, zikibaki Dakika 3 Mpira kwisha, Cesc Fabregas, alietokea Benchi, aliwasha Shuti toka nje ya Boksi na kuipa Chelsea ushindi wa 4-3.
Mbali ya kufungwa, Watford walimaliza Mechi wakiwa Mtu 10 baada Sebastian Prodl kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 92 baada kuzoa Kadi za Njano 2.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

Jumatatu Mei 15

Chelsea 4 Watford 3             

Jumanne Mei 16

2145 Arsenal v Sunderland         

2200 Manchester City v West Bromwich Albion          

Jumatano Mei 17

2145 Southampton v Manchester United         

Alhamisi Mei 18

2145 Leicester City v Tottenham Hotspur         

Jumapili Mei 21

Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni

Arsenal v Everton            

Burnley v West Ham United                 

Chelsea v Sunderland                 

Hull City v Tottenham Hotspur              

Leicester City v Bournemouth               

Liverpool v Middlesbrough          

Manchester United v Crystal Palace                 

Southampton v Stoke City          

Swansea City v West Bromwich Albion            

Watford v Manchester City

PALACE YAEPA KWA KUISHUSHA HULL, LIVERPOOL YAJIKITA 4 BORA, SPURS YAAGA WHITE HART LANE KWA KUIPIGA MAN UNITED ‘ILIYOZUBAA’ NA EUROPA!

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Matokeo:

Jumapili Mei 14

Crystal Palace 4 Hull City 0

West Ham United 0 Liverpool 4   

Tottenham Hotspur 2 Manchester United 1

+++++++++++++++++++++++++

SPURS-BAIBAI-WHITEHARTLANECRYSTAL PALACE imejihakikishia kubaki EPL, LIGI KUU ENGLAND, baada kuichapa 4-0 Hull City ambayo sasa imeungana na Sunderland na Middlesbrough kushuka Daraja na kucheza Daraja la chini la Championship Msimu ujao.

Pia, Liverpool sasa imejihakikishia uwezo wa kubaki 4 Bora upo mikononi mwao wenyewe kwa kuitwanga 4-0 West Ham United.

Nao, Man United, wakiwa washakata tamaa kutinga 4 Bora na kuelekeza nguvu zao kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo watacheza na Ajax na wakishinda kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI, Leo walishusha Kikosi ‘laini’ huko White Hart Lane Jijini London na kuipa Tottenham Hotspur njia laini kushinda kwenye Mechi yao ya mwisho Uwanjani hapo ambao utafungwa kwa Matengenezo makubwa na kuunganishwa na Uwanja Mpya Jirani na huo.

Palace, wakiwa kwao Selhurst Park Jijini London, waliitandika Hull 4-0 kwa Bao za Wilfried Zaha, Christian Benteke, Luka Milivojevic, kwa Penati, na Patrick van Aanholt.EPL-MEI14

Liverpool, wakicheza Ugenini London Stadium, walipata ushindi wao wa 4-0 kwa Bao za Daniel Sturridge, Philippe Coutinho, Bao 2, na Divock Origi.

Ikiwa Liverpoo, wataifunga Middlesbrough, Timu ambayo imeshashuka Daraja, huko Anfield Jumapili ijayo huko Anfield katika Mechi ya mwisho kabisa ya Ligi Msimu huu basi watakuwemo 4 Bora.

Nao Tottenham walifunga Bao zao kupitia Victor Wanyama, Dakika ya 6, na Harry Kane, Dakika ya 48, huku Man United wakipata Bao lao Dakika ya 71 kupitia Kepteni wao Wayne Rooney.

Mara baada ya Mechi kwisha, Mashabiki wa Spurs walivamia Uwanjani kuuga Uwanja wao.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

Jumatatu Mei 15

2200 Chelsea v Watford             

Jumanne Mei 16

2145 Arsenal v Sunderland         

2200 Manchester City v West Bromwich Albion          

Jumatano Mei 17

2145 Southampton v Manchester United         

Alhamisi Mei 18

2145 Leicester City v Tottenham Hotspur         

Jumapili Mei 21

Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni

Arsenal v Everton            

Burnley v West Ham United                 

Chelsea v Sunderland                 

Hull City v Tottenham Hotspur              

Leicester City v Bournemouth               

Liverpool v Middlesbrough          

Manchester United v Crystal Palace                 

Southampton v Stoke City          

Swansea City v West Bromwich Albion            

Watford v Manchester City

EPL: BATSHUAYI AWAPA UBINGWA WA ENGLAND CHELSEA!

CHELSEA-BATSHUAYI-UBINGWAEPL, LIGI KUU ENGLAND

Matokeo:

Ijumaa Mei 12

Everton 1 Watford 0          

West Bromwich Albion 0 Chelsea 1

+++++++++++++++++++++++++

Chelsea wametwaa Ubingwa wa England huko The Hawthorns baada kuitungua West Bromwich Albion 1-0 katika Mechi ya EPL, LIGI KUU ENGLAND, kwa Bao la Dakika ya 82 la Michy Batshuayi alietokea Benchi.

Chelsea sasa wanaongoza Ligi hii wakibakisha Mechi 2 na wana Pointi 87 kwa Mechi 36 ambazo haziwezi tena kufikiwa na Timu ya Pili Tottenham Hotspur ambao wana Pointi 77 kwa Mechi 35.

Batshuayi, Mchezaji kutoka Belgium mwenye Miaka 23, alikuwa hajaifungia Chelsea tangu Agosti, aliingizwa Dakika ya 76 kumbadili Pedro na kuseleleka kuunganisha Pasi ya Cesar Azpilicueta na kufunga Bao lililoipa Chelsea Ubingwa chini ya EPL-MEI13Meneja Mpya wa Msimu huu Mtaliana Antonio Conte.

++++++++++++

JE WAJUA?

-Chelsea wametwaa Taji la 6 la Ubingwa England na la 5 kwenye zama hizi za EPL, Ligi Kuu England. Timu pekee iliyotwaa Mataji mengi ya Ubingwa England ya EPL ni Manchester United yenye Mataji 13 ya EPL na 20 kwa Ujumla.

-Antonio Conte ni Meneja wa 4 kutoka Italy aliewahi kutwaa Ubingwa wa England kufuatia Carlo Ancelotti, Roberto Mancini na Claudio Ranieri.

++++++++++++

Sasa kibarua kinachofuata ni cha Antonio Conte kumuiga alichofanya Carlo Ancelotti Mwaka 2010 alipotwaa Dabo katika Msimu wake wa kwanza na Chelsea kwa hapo Mei 27 kwa kuifunga Arsenal Wembley katika Fainali ya FA CUP.

Kwenye Mechi nyingine ya EPL iliyochezwa Jana huko Goodison Park, Everton pia iliitungua Watford 1-0 kwa Bao la Dakika ya 56 la Ross Barkley Mchezaji ambae amegoma kusaini Mkataba Mpya akishinikiza kuhama.

VIKOSI:

WEST BROM:Foster, Dawson, McAuley [Wilson, 64], Evans, Nyom, Fletcher, McClean [Chadli], Livermore, Field [Yacob, 51], Brunt, Rondon.

Akiba:Robson-Kanu, Yacob, Morrison, Marc Wilson, Myhill, Chadli, Leko.

CHELSEA:Courtois, Azpilicueta, Luiz, Cahill, Moses [Zouma, 86], Fabregas, Matic, Alonso, Pedro [Batshuayi, 76], Hazard [Willian, 75], Costa.

Akiba:Begovic, Zouma, Ake, Kante, Willian, Batshuayi, Terry.

REFA:MICHAEL OLIVER

CHELSEA-MABINGWA16-17

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

Jumamosi Mei 13

1430 Manchester City v Leicester City             

1700 Bournemouth v Burnley                

1700 Middlesbrough v Southampton     

1700 Sunderland v Swansea City 

1930 Stoke City v Arsenal 

Jumapili Mei 14

1400 Crystal Palace v Hull City    

1615 West Ham United v Liverpool       

1830 Tottenham Hotspur v Manchester United 

UEFA EUROPA LIGI: FAINALI NI MAN UNITED NA AJAX!!

Nusu Fainali – Mechi za Marudiano

***Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi Mbili

Alhamisi Mei 11

Manchester United 1 Celta Vigo 1 [2-1]

Olympique Lyonnais 3 Ajax Amsterdam 1 [4-5]

+++++++++++++++++++++++++++++

MANUNITED-FELLAINI-FAINALIManchester United na Ajax Amsterdam zimetinga Fainali ya UEFA EUROPA LIGI baada kupeta Mechi zao za Marudiano za Nusu Fainali.

Man United walitoka Sare 1-1 na Celta Vigo na wao kusonga kwa Jumla ya Bao 2-1 kwa vile walishinda 1-0 Wiki iliyopita huko Spain wakati Ajax wamefungwa 3-1 lakini wamesonga kwa Jumla ya Bao 5-4 baada ya kushinda Mechi ya Kwanza 4-1.

Man United walitangulia kufunga Dakika ya 17 kwa Bao la Kichwa la Marouane Fellaini alipounganisha Krosi ya Marcus Rashford.

Celta Vigo walisawazisha Dakika ya 86 kwa Bao la Kichwa la Fancundo Roncaglia.

Dakika chache baada ya Bao hilo la kusawazisha, Refa aliwatoa kwa Kadi Nyekundu Eric Bailly wa Man United na Roncaglia kwa kuvaana.

VIKOSI:

MAN UNITED: Romero; Valencia, Bailly, Blind, Darmian; Fellaini, Herrera, Pogba; Lingard [Rooney, 88’], Mkhitaryan [Carrick, 77], Rashford Smalling, 88]

Akiba: De Gea, Jones, Smalling, Carrick, Mata, Rooney, Martial

CELTA VIGO: Alvarez; Mallo, Cabral, Roncaglia, Jonny; Wass [Jozabed, 45], Radoja [Bongonda, 67], Hernandez; Aspas, Guidetti, Sisto [Beauvue, 79’]

Akiba: Villar, Fontas, Diaz, Bongonda, Beauvue, Jozabed, Gomez

REFA: Ovidiu Alin Hategan [Romania]

UEFA EUROPA LIGI

Tarehe Muhimu:

FAINALI

24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden

UEFA EUROPA LIGI: LEO MAN UNITED KUIVAA CELTA VIGO, KUWANIA FAINALI!

>MOURINHO: ‘HII NI MECHI YETU YA MSIMU!’

Nusu Fainali – Mechi za Marudiano

**Saa za Bongo

***Kwenye Mabano Magoli Mechi ya Kwanza

Alhamisi Mei 11

2205 Manchester United v Celta Vigo [1-0]

2205 Olympique Lyonnais v Ajax Amsterdam [1-4]

+++++++++++++++++++++++++++++

MANUNITED-EUROPAMECHIMSIMUKABLA ya Jana Jose Mourinho alisema Mechi yao ya Marudiano na Celta Vigo itakayochezwa Leo Uwanjani Old Trafford ya kuwania kutinga Fainali ya UEFA EUROPA LIGI, UEL, ndio Mechi yao ya Msimu.

Hilo lilitokana na ukweli kuwa Bingwa wa UEL hucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI wakati sasa Man United wanashikilia Nafasi ya 6 kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, wakiwa nje ya 4 Bora huku Mechi zikibaki 3 tu na hivyo hatarini kuikosa UCL Msimu ujao.

Jana Meneja huyo wa Man United, Jose Mourinho, alisisitiza kuwa wao kuipa kipaumbele UEFA EUROPA LIGI si makosa wala kucheza tombola kwani ndio ukweli.

Hii Leo Man United wanatinga kwao Old Trafford wakiwa kifua mbele 1-0 baada ya kuifunga Celta Vigo Ugenini Wiki iliyopita.

Mourinho, akisisitiza msongo wa Ratiba, ameeleza: “Mechi 17 ndani ya Wiki 7 si mchezo. Hii  [KUTILIA MKAZO UEL] si tombola ndio hali yetu! Ulikuwa uamuzi rahisi kufuatana na hali yetu!”

Mourinho amesema hatasikitika ikiwa hawatatwaa Taji la UEL na kudai: “Tutaona kama tutaweza. Tukishindwa hatujali. Hatutajutia, tumejitolea kila kitu, Wachezaji na mimi!”

Ikiwa Man United watatinga Fainali hii Leo basi upo uwezekano mkubwa wa kuivaa Ajax Amsterdam ya Netherlands ambao nao Leo wapo Ugenini kucheza na Lyon lakini wao walishinda Mechi ya Kwanza 4-1.

DONDOO ZA MECHI YA LEO:

Man United wapo kwenye Mechi ya Leo wakiwa 1-0 mbele kwa Bao la Mchezaji wa Miaka 19 Markus Rashford, anaevaa Jezi Namba 19, kufunga Bao lake la 19 Msimu huu.

Wakati Jumapili, Celta Vigo wakipata kipigo chao cha 5 mfululizo kwa kuchapwa 3-0 na Malaga kwenye La Liga, Man United walifungwa 2-0 na Arsenal kwenye EPL, LIGI KUU ENGLAND, Mechi ambayo walichezesha Kikosi tofauti kidogo na rekodi yao ya kutofungwa Mechi 25 za Ligi kuvunjwa.

Msimu huu, Man United wamecheza Mechi 6 za Ulaya Uwanjani kwao Old Trafford na kushinda zote.

Nini Mameneja Wamesema?

-Eduardo Berizzo, Celta Vigo:

“Nategemea Man United kushambulia ili washinde..ni mtihani mkubwa. Man United ni Timu kubwa na huishi na na presha na wanaikabili kila Siku. Inabidi tutilie mkazo tunachoweza kufanya wenyewe!”

-José Mourinho, Manchester United

“Vikombe ni muhimu kwa Klabu na ni muhimu zaidi kuwa kwenye Fainali. Ni muhimu kwa Klabu hii kupigania Kombe ambalo hawajawahi kulibeba. Tutapigana kwa nguvu. Ni safari ndefu, Mechi ya 14 Ulaya kwenye EUROPA LIGI na tunataka kushinda”

VIKOSI:

MANCHESTER UNITED: Romero; Valencia, Bailly, Blind, Darmian; Fellaini, Herrera, Pogba; Lingard, Rashford, Mkhitaryan.

NJE - Majeruhi: Shaw, Ibrahimovic, Rojo

CELTA VIGO: Sergio; Mallo, Cabral, Roncaglia, Jonny; Radoja, Tucu; Wass, Aspas, Sisto; Guidetti.

NJE - Majeruhi:  Rossi, Planas

REFA: Ovidiu Alin Hategan[Romania]

UEFA EUROPA LIGI

Tarehe Muhimu:

FAINALI

24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden

Habari MotoMotoZ