MAN UNITED: SHUGHULI PEVU APRILI – MECHI 9 SIKU 30!

MANUNITED-MATAJI-YANAKUJABAADA ya kukaa pembeni kwa Wiki Mbili kupisha Mechi za Kimataifa, Manchester United wanarudi kilingeni Jumamosi Aprili 1 kwa kucheza Nyumbani Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, dhidi ya West Bromwich Albion Uwanjani Old Trafford.

Mechi hiyo ni mwanzo wa mfululizo wa Mechi 9 ambazo watazicheza Mwezi Aprili na 7 kati ya hizo ni za EPL wakati 2 ni za UEFA EUROPA LIGI za Robo Fainali wakipambana na Klabu ya Belgium Anderlecht.

Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 5 kwenye Ligi wakiwa na Pointi 52 kwa Mechi 27 wakiwa nyuma ya Timu ya 4 Liverpool kwa Pointi 2 lakini Liverpool wamecheza Mechi 2 zaidi yao wakati Timu ya 3, Man City, wakiwa mbele yao kwa Pointi 5 lakini nao wamecheza Mechi 1 zaidi yao.

Timu ya Pili ni Tottenham wenye Pointi 59 kwa Mechi 28 na Vinara ni Chelsea wenye Pointi 69 kwa Mechi 28.

Mbali ya kuwania Nafasi ya 4 Bora kwenye EPL ili wacheze UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao, Man United wanaweza kutinga Mashindano hayo ikiwa watatwaa UEFA EUROPA LIGI na hivyo kikwazo cha kwanza kwao ni kuing’oa Anderlecht.

Lakini Mechi hizi mfululizo kwao si rafiki wao na hasa wakiwa na Majeruhi na Vifungo kwa Wachezaji wao.

Mfungaji wao Bora Zlatan Ibrahimovic na Kiungo Ander Herrera wapo Vifungoni na wote wataikosa Mechi na West Bromwich Albion wakimalizia Vifungo vyao vya Mechi 3 kwa Ibrahimovic na 2 kwa Herrera.

Lakini pia Mechi hiyo itawakosa Majeruhi Chris Smalling, Phil Jones, Marouane Fellaini na pengine Paul Pogba.

MAN UNITED – Ratiba Aprili 2017:

**Saa za Bongo

01 APR: Man United v West Bromwich Albion, EPL, Saa 1700

04 APR: Man United v Everton, EPL, 2200

09 APR: Sunderland v Man United, EPL, 1530

13 APR: Anderlecht v Man United, Europa Ligi Robo Fainali, 2205

16 APR: Man United v Chelsea, EPL, 1800

20 APR: Man United v Anderlecht, Europa Ligi Robo Fainali, 2205

23 APR: Burnley v Man United, EPL, 1615

27 APR: Man City v Man United, EPL, 2200

30 APR: Man United v Swansea City, EPL, 1400

CITY YADUNGWA FAINI, MORATA AITAKA CHELSEA!

CITY YADUNGWA FAINI

CITY-WAMZONGA-REFAManchester City wametwangwa Faini ya £35,000 na FA, Chama cha Soka England, kutokana na Utovu wa Nidhamu wa Wachezaji wao wakati walipotoka Sare 1-1 na Liverpool hapo Machi 19 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.

City ilikiri kosa la kutodhibiti Wachezaji wao kufuatia tukio la Dakika ya 50 ya Mechi hiyo ambapo Refa Michael Oliver aliipa Penati Liverpool na Refa huyo kumpa Kadi ya Njano Gael Clichy kwa Rafu iliyozaa Penati hiyo na David Silva kwa kulalamikia Penati hiyo huku Wachezaji kadhaa wakimzonga Refa.

James Milner alifunga Penati hiyo na Sergio Aguero kuisawazishia City katika Dakika ya 69.

ALVARO MORATA AITAKA CHELSEA

JANA zimeibuka ripoti kutoka Spain kwamba Alvaro Morata ataihama Real Madrid mwishoni mwa Msimu huu ili kuungana tena na Antonio Conte huko Chelsea.

Wawili hao walikuwa pamoja huko Italy Klabuni Juventus Msimu uliopita na kuisaidia kutwaa Ubingwa wa Serie A kabla hawajatengana kwa Morata kurejea Real na Conte kwenda Chelsea.

Lakini tangu arejee Real, Morata, mwenye Miaka 24 na ni Mchezaji wa Kimataifa wa Spain, amekuwa hana Namba ya kudumu ndani ya Kikosi cha Zinedine Zidane.

Ripoti hizo zimedai Conte ashamtonya Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kuhusu kumnunua Morata lakini vikwazo ni hatima za Wachezaji wao Eden Hazard na Diego Costa.

Hivi sasa Hazard anatajwa kuhamia Real huku kukiwa hamna lolote kuhusu Costa ingawa nae anavumishwa kutaka kuondoka Chelsea. 

KOMBE LA DUNIA 2018 – MBIO ZA RUSSIA: ENGLAND, MABINGWA WA DUNIA GERMANY ZAPETA!

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Ratiba/Matokeo:

Jumapili Machi 26

**Saa za Bongo

San Marino 0 Czech Republic 6 [Kundi C]

Armenia 2 Kazakstan 0 [Kundi E]

England 2 Lithuania 0 [Kundi F]

Azerbaijan 1 Germany 4 [Kundi C]        

21:45 Malta v Slovakia [Kundi F] 

21:45 Romania v Denmark [Kundi E]

21:45 Scotland v Slovenia [Kundi F]      

21:45 Northern Ireland v Norway [Kundi C]    

21:45 Montenegro v Poland [Kundi E]

++++++++

ENGLAND-DEFOE-WAYAHII LEO England wameendelea kupiga hatua kutinga Russia Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuifunga Lithuania 2-0 Uwanjani Wembley London ikiwa ni Mechi ya Kundi F.

Baada ya Mechi 5, England wapo kileleni mwa Kundi F lenye Timu 6 wakiwa na Pointi 13 wakifuata Slovenia wakiwa na Pointi 8 kwa Mechi 4.

Baadae Usiku huu, Slovenia watakuwa Wageni wa Scotland katika Mechi ngumu mno ya Kundi F.

Bao za England hii Leo zilifungwa na Jermaine Defoe Dakika ya 21, likiwa Bao lake la kwanza tangu Novemba 2013 kwa England alipoichezea kwa mara ya mwisho, na la Pili kupigwa na Jamie Vardy, alieingizwa Dakika ya 60, na kupachika Bao hilo Dakika ya 66.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

Kwenye Mechi nyingine za mapema hii Leo, Mabingwa wa Dunia Germany wamejiweka sawa kwenda Russia kwa kushinda Ugenini walipoicharanga Azerbaijan Bao 4-1 katika Mechi ya Kundi C na kuzidi kupaa kileleni.

Hadi Mapumziko, Germany waliongoza 3-1 kwa Bao za Andre Schurrle, Thomas Mueller na Mario Gomez huku Azerbaijan wakifunga kupitia Dimitrij Nazarov.

Germany walipata Bao la 4 Dakika ya 81 Mfungaji akiwa Andre Schurrle.

Baada ya Mechi 5, Germany wanaongoza Kundi C wakiwa na Pointi 15 na kufuata Czech Republic wenye Pointi 8.

VIKOSI:

England: Hart; Walker, Stones, Keane, Bertrand; Oxlade-Chamberlain, Dier; Sterling [Rashford, 60’], Alli, Lallana; Defoe [Vardy, 60’]

Lithuania:  Šetkus; Vaitkūnas, Kijanskas, Klimavičius, Slavickas; Kuklys, Žulpa; Novikovas [Grigaraviciu, 54’], Slivka [Paulius, 87'], Černych; Valskis [Matulevicius, 73']

REFA: Ruddy Buquet [France]

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Ratiba:

**Saa za Bongo

Ijumaa Juni 9

21:45 Bosnia And Herzegovina v Greece [Kundi H]

21:45 Netherlands v Luxembourg [Kundi A]

21:45 Belarus v Bulgaria [Kundi A]       

21:45 Latvia V Portugal [Kundi B]         

21:45 Sweden v France [Kundi A]        

21:45 Faroe Islands v Switzerland [Kundi B]   

21:45 Estonia v Belgium [Kundi H]       

21:45 Andorra v Hungary [Kundi B]      

21:45 Gibraltar v Cyprus [Kundi H]       

KOMBE LA DUNIA 2018 – MBIO ZA RUSSIA: JUMAPILI ENGLAND WAPO WEMBLEY NA LITHUANIA!

WC-2018-EURO-QJUMAPILI, England wako Nyumbani kwao kucheza na Lithuania ikiwa ni Mechi ya Kundi F la Ulaya la kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Baada ya Mechi 4 kwa kila Timu England ndio wanaongoza Kundi F lenye Timu 6 wao wakiwa na Pointi 10 wakifuatiwa na Slovenia wenye 8 na Lithuania wapo Nafasi ya wakiwa na Pointi 5.

Kwenye Mechi hii na Lithuania, England wataongozwa na Kipa Joe Hart ambae ndie amepewa Utepe wa Kepteni kwa vile Kepteni Wayne Rooney hayumo Kikosini kwa vile ni Majeruhi na Gary Cahill, ambae ndie alikuwa Nahodha Juzi walipofungwa 1-0 na Germany, yupo Kifungoni kwa Mechi 1.

Mara ya mwisho kwa Joe Hart, Kipa wa Man City anaecheza kwa Mkopo huko Italy na Torino, kuwa Nahodha wa England ilikuwa ni 2015 walipofungwa 2-0 na Spain.

Jumapili itamkosa pia Sentahafu wa Man United Chris Smalling ambae ameumia na hilo pamoja na kukosekana Cahill kumeifanya England kubakiwa na Masentahau Watatu ambao ni John Stones wa Man City, Michael Keane wa Burnley na Ben Gibson wa Middlesbrough.

++++++++

JE WAJUA?

-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia

-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia

-Washindi wa Pili 8 Bora toka Makundi hayo 9 watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia

++++++++

Takwimu

-England hawajafungwa Mechi yeyote Mchujo wa Mashindano makubwa kwa Mechi 33 sasa za Kombe la Dunia na EURO.

-Kwenye Kundi la EURO 2016, England iliifunga Lithuania mara 2, 4-0 hapo Wembley na 3-0 Ugenini.

-Pamoja na Germany, England ndio Timu pekee haijaruhusu kufungwa hata Bao 1 katika Mechi hizi za Makundi za Kombe la Dunia 2018.

Tathmini

KUNDI F

Kinara: England (Pointi 10)

Wa Pili: Slovenia (8)

Hali ilivyo hadi sasa

England, licha ya kuyumbishwa kwa mabadiliko ya Kocha katikati ya kampeni hii, bado wapo kileleni na katika Mechi yao ya mwisho waliwanyuka Mahasimu wao wa Jadi Scotland 3-0.

Slovenia, ambao walitoka 0-0 na England, wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 ya England na wapo Pointi 2 mbele ya Timu ya 3 Slovakia.

Matokeo muhimu

Slovakia 0-1 England, Slovenia 1-0 Slovakia, England 3-0 Scotland

Gemu zijazo

26 Machi 2017: England v Lithuania, Malta v Slovakia, Scotland v Slovenia

KOMBE LA DUNIA 2018 – MAKUNDI ULAYA

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Machi 25

20:00 Cyprus v Estonia [Kundi H]

20:00 Bosnia And Herzegovina v Gibraltar [Kundi H]  

20:00 Sweden v Belarus [Kundi A]        

20:00 Andorra v Faroe Islands [Kundi B]         

20:00 Switzerland v Latvia [Kundi B]

22:45 Luxembourg v France [Kundi A]  

22:45 Bulgaria v Netherlands [Kundi A] 

22:45 Belgium v Greece [Kundi H]        

22:45 Portugal v Hungary [Kundi B]

Jumapili Machi 26

19:00 San Marino v Czech Republic [Kundi C]  

19:00 Armenia v Kazakstan [Kundi E]   

19:00 England v Lithuania [Kundi F]

19:00 Azerbaijan v Germany [Kundi C]  

21:45 Malta v Slovakia [Kundi F] 

21:45 Romania v Denmark [Kundi E]

21:45 Scotland v Slovenia [Kundi F]      

21:45 Northern Ireland v Norway [Kundi C]    

21:45 Montenegro v Poland [Kundi E]

SPURS RUKSA WEMBLEY MECHI ZA NYUMBANI MSIMU UJAO!

>>KUPISHA KITU KIPYA WHITE HART LANE!

WHITEHARTLANE-MPYAMAOMBI ya Tottenham Hotspur kuutumia Uwanja wa Wembley Jijini London kwa Mechi zao za Nyumbani Msimu ujao yamekubaliwa.

Brent Council, Halmashauri ambayo Uwanja huo upo, imepitisha kwa Kura uamuzi wa kuiruhusu Spurs kutumia Wembley kwa Mechi zao 27 na kuruhusu Uwanja wote kujazwa Watu 90,000.

Spurs wamepewa hadi Machi 31 kuthibitisha matumizi hayo.

Hivi sasa Spurs wanajenga Uwanja wao mpya jirani na ule wa sasa White Hart Lane na ambao unatarajiwa kuwa tayari kutumika kwenye Msimu wa 2018/19.

Sasa Spurs wanatafakari kama waendelee kuutumia White Hart Lane kwa Msimu ujao na ule wa 2018/19 ili wahamie Uwanja Mpya Msimu wa 2019/20.

Spurs hawakutaka kuutumia Wembley huku wakiwekewa sharti la Uwanja kutojazwa na Halmashauri ya Brent ambayo baadhi ya Wajumbe wake walipinga Uwanja kujazwa wote kutokana na kuogopa vitendo vya kihuni vya Washabiki na pia kuzorotesha Usafiri wa Eneo lao.

Wajumbe hao walitaka Spurs waruhusiwe kutumia Wembley kwa ujazo wa Watu 61,000 tu na si 90,000 kama vile uwezo wa Wembley yenyewe.

Kukubaliwa kwa Spurs kucheza Mechi 27 tu kuna sharti kuwa Mechi zikizidishwa zaidi ya hapo basi hawataruhusiwa kuwa na Washabiki zaidi ya 50,835 kwa Mechi za ziada.