NI RASMI, LACAZETTE YU ARSENAL KWA DAU LA REKODI, ROONEY NJIANI KURUDI EVERTON!

LACAZETTE ARSENAL RASMIWAKATI Arsenal ikitangaza rasmi kumsaini Straika wa France Alexandre Lacazette kwa dau la Rekodi kwa Klabu hiyo la Pauni Milioni 52.7, Kepteni wa Manchester United Wayne Rooney yupo kwenye mazungumzo mazito kurejea Klabu yake ya zamani Everton.

Mara ya mwisho kwa Arsenal kulipa Dau kubwa kabisa kumnunua Mchezaji ni Pauni Milioni 42.4 walipomnunua Mesut Ozil kutoka Real Madrid Mwaka 2013.

Huko London, Jana Lacazette alifanyiwa Vipimo vya Afya na Arsenal na Leo hii kutangazwa rasmi ni Mchezaji Mpya aliesaini Mkataba wa Miaka Mitano.

Jumapili, Lacazette, anaetokea Lyon ya France, anatarajiwa kusafiri na Kikosi cha Arsenal kinachoruka kwenda Sydney, Australia kwa ajili ya Matayarisho ya Msimu Mpya unaoanza Agosti.

Msimu uliopita, Lacazette ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi 1 huko France alikopiga Bao 28 na ameshapiga Jumla ya Bao 129 katika Mechi 275 tangu alipoanza kuichezea Timu ya Kwanza Msimu wa 2009/10.

Huko France, Msimu uliopita, ni Straika wa Paris St-Germain tu, Edinson Cavani, aliempiku kwa kufunga Bao nyingi kwa Mechi za Mashindano yote aliepachika Bao 35.

Lacazette, ambae ameichezea Timu ya Taifa ya France Mechi 11, alikuwa aende Atletico Madrid lakini Vigogo hao wa Spain walipata pigo baada ya Rufaa yao kupinga kufungiwa Kusajili Wachezaji Wapya walioiwasilisha CAS, Court of Arbitration for Sports, kutupwa chini na hivyo kubaki Kifungoni hadi Januari 2018.

Lacazette sasa anakuwa Mchezaji wa Pili kutua Arsenal katika Kipindi hiki baada ya Fulbeki wa Kushoto Sead Kolasinac, aliejiunga kutoka Schalke ya Germany.

WAKATI HUO HUO, Wayne Rooney yupo kwenye Mazungumzo yaliyofikia hatua za mwisho na Everton ili arejee huko kwenye Klabu aliyoanza kucheza nayo tangu Utotoni.

Lakini kikwazo ni mshahara wake mkubwa wa Pauni 250,000 kwa Wiki anaovuna na Man United hivi sasa ambako amebakisha Mkataba wa Miaka Miwili.

Rooney, mwenye Miaka 31, alijiunga na Man United Agosti 2004 na tangu wakati huo kutwaa Ubingwa wa England mara 5, UEFA CHAMPIONZ LIGI 1, FA CUP 1, Kombe la Ligi mara 3 na EUROPA LIGI 1.

Pia yeye ndie Mfungaji Bora wa Man United katika Historia yao kwa kupiga Bao 253.

LACAZETTE AKAMILISHA ‘AFYA’ EMIRATES, KUSAINI DILI YA PAUNI MILIONI 45 NA USHEI!

>KUVUNJA REKODI YA WENGER NA ARSENAL!

LACAZETTE ARSENALSTRAIKA wa Lyon  ya France Alexandre Lacazette amemaliza upimwaji Afya huko Arsenal Jijini London na yupo mbioni sasa kukamilisha Dili ambayo haitakuwa chini ya Pauni Milioni 45 na kumfanya yeye awe Mchezaji wa Bei Ghali Klabuni hapo.

Awali, Arsenal waligomewa Ofa yao na Lyon kwa ajili ya Straika huyo Kimataifa wa France mwenye Umri wa Miaka 26 lakini Mazungumzo yakadumishwa.

Ada kamili ya Uhamisho, ukichanganya na Vipengele vingine vyote, inaweza kufika Pauni Milioni 52 na kuipita ile Arsenal walilipa Pauni Milioni 42.4 kumnunua Mesut Ozil kutoka Real Madrid Mwaka 2013.

Msimu uliopita, Lacazette ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Ligi 1 huko France alikopiga Bao 28 na ameshapiga Jumla ya Bao 129 katika Mechi 275 tangu alipoanza kuichezea Timu ya Kwanza Msimu wa 2009/10.

Huko France, Msimu uliopita, ni Straika wa Paris St-Germain tu, Edinson Cavani, aliempiku kwa kufunga Bao nyingi kwa Mechi za Mashindano yote aliepachika Bao 35.

Lacazette, ambae ameichezea Timu ya Taifa ya France Mechi 11, alikuwa aende Atletico Madrid lakini Vigogo hao wa Spain walipata pigo baada ya Rufaa yao kupinga kufungiwa Kusajili Wachezaji Wapya walioiwasilisha CAS, Court of Arbitration for Sports, kutupwa chini na hivyo kubaki Kifungoni hadi Januari 2018.

Lacazette sasa anakuwa Mchezaji wa Pili kutua Arsenal katika Kipindi hiki baada ya Fulbeki wa Kushoto Sead Kolasinac, aliejiunga kutoka Schalke ya Germany.

BABA, WAKALA WA MORATA WAKUTANA NA REAL KUFOSI KUHAMIA MAN UNITED!

>EVERTON WAMSAINI SANDRO WA MALAGA, TERRY YUPO VILLA!

SOMA ZILIZOBAMBA ENGLAND:

BABA, WAKALA WA MORATA

REAL MORATAWAWAKILISHI wa Straika wa Spain Alvaro Morata wamekutana na Real Madrid Asubuhi hii kujadili hatima ya Straika huyo anaetaka kwenda Manchester United.

Manchester United wanataka kumsaini Morata ili ambadili Zlatan Ibrahimovic huku akiafiki Uhamisho huo.

Hii Leo, Wakala wa Morata, Juanma Lopez, na Baba Mzazi wa Mchezaji huyo, Alfonso Morata, walitua huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid na kufanya Mazungumzo ya Dakika 50 na Real Madrid.

Man United na Real zimekuwa zikivutana kuhusu Dau la Uhamisho ambalo Real wanataka Zaidi Pauni Milioni 70 kwa Straika huyo wa Miaka 24 wakati Man United walishatoa Ofa ya Pauni Milioni 52.4.

Everton yamsaini Straika wa Malaga Sandro Ramirez

Straika wa Malaga, Sandro Ramirez, amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Everton.

Msimu uliopita Chipukizi huyo wa Miaka 21 alifungia Malaga Bao 14 baada ya kujiunga nao kutoka Barcelona.

Everton wanatarajiwa kumasaini Beki wae, kwa Dau la Pauni Milioni 24.

Tayari Everton wameshawasaini Kipa wa England U-21 kutoka Sunderland,Jordan Pickford, kwa Pauni Milioni 30 na Kepteni wa Ajax ya Netherlands, Davy Klaasen, kwa Pauni Milioni 24.

Aston Villa yamsaini Kepteni wa zamani wa Chelsea na England John Terry

John Terry, mwenye Miaka 36, amesaini kuichezea Aston Villa ambayo sasa inacheza Daraja la chini yake EPL, LIGI KUU ENGLAND.

Terry, ambae Mkataba wake na Chelsea uliisha Juni 30, amedai alikataa kuchezea Klabu za EPL kwa vile hataki kuikabili Chelsea.

Akiwa na Chelsea, Terry aliichezea Mechi 717 na kutwaa Ubingwa wa EPL mara 5

ARSENAL 'WAMNUSA' LACAZETTE, KUVUNJA REKODI YAO!

Arsenal sasa wapo karibu mno kumsaini Straika wa France Alexandre Lacazette anaechezea Klabu ya Lyon.
LACAZETTE ARSENALMapema, Ofa ya Arsenal waligomewa wao Ofa yao kumnunua Straika huyo mwenye Miaka 26 lakini sasa inaaminika wapo karibu kukubaliwa.
Inadhaniwa Dau la Lacazette litavunja lile la Mwaka 2013 Arsenal walipoilipa Real Madrid kumnunua Mesut Ozil na kuweka Rekodi Mpya kwa Klabu hiyo.
Wakati huo Arsenal ililipa Pauni Milioni 42.4.
Mbali ya Staa huyo, Arsenal pia walikuwa Sokoni huko France lakini Ofa yao kimnunua Kiungo Thomas Lemar, mwenye Miaka 21, iligomewa.
Juzi, Mtendaji Mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis aliahidi kufanya Usajili mkubwa katika kipindi hiki.
Lakini hafi sasa Arsenal imemnunua Fulbeki wa Kushoto Sead Kolasinac akitokea Schalke ya Germany.
Lacazette, alieichezea France mara 11, alihusishwa pia na kujiunga na Atletico Madrid kabla karibuni Vigogo hao wa Spain kupigwa nyundo na CAS, Court of Arbitration for Sport, na Rufaa yao kutupwa na hivyo kutoruhusiea kusaini Mpya hadi Januari 2018.
Llacazette alichomoza Soka kuu kwa kuanza kuichezea Timu ya Kwanza ya Lyon Msimu wa 2009/10.
Tangu wakati huo amepiga Bao 129 katika Mechi 275.
Msimu uliopita alifunga Bao 28 kwenye Ligi 1 huko France akipitwa tu na Straika wa Paris St-Germain Edinson Cavani aliefunga Bao 35.

RIPOTI: MORATA ‘ABONYEZA’ WENZAKE YU NJIANI OLD TRAFFORD, WALKER ‘KUTEMBEA’ HADI CITY, AKE ANG’OKA CHELSEA!

>PATA RIPOTI ZILIZOBAMBA KUHUSU UHAMISHO ENGLAND!

MORATA ‘ABONYEZA’ WENZAKE YU NJIANI OLD TRAFFORD

REAL MORATAHivi Majuzi Straika wa Real Madrid Alvaro Morata alikatiza Fungate yake na kumwacha Mke Mpya pekee ili kumvaa Rais wa Real, Florentino Perez, akikusudia kulazimisha Uhamisho wake kwenda Manchester United.

Tayari Morata ashawatonya Maswahiba zake anahamia Manchester.

Hivi sasa, Man United na Real zinavutana kuhusu Dau la Uhamisho huku Real wakitaka Pauni Milioni 70 wakati Man United wamegota Pauni Milioni 60 kwa Staa huyo mwenye Miaka 24.

Morata, aliekulia Kisoka Real Madrid tokea akiwa Kinda, ameamua kutua Old Trafford baada ya Jose Mourinho kumhakikishia atavaa Namba 9 ya Zlatan Ibrahimovic.

Pia, Morata amependa kwenda Man United kwani hillo litampa nafasi ya kucheza sana na hivyo kuzidisha nafasi yake ya kuwemo kwenye Kikosi cha Spain kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia tofauti na Real ambako amekuwa haanzi mara kwa mara.

KYLE WALKER

Manchester City wamefungua mazungumzo na Tottenham ili wamsaini Beki Kyle Walker.

Walker, mwenye Miaka 27, amecheza Mechi za EPL, LIGI KUU ENGLAND, mara 183 tangu ajiunge na Spurs kutoka Sheffield United Mwaka 2009.

Baada ya Msimu kumalizika Mwezi Mei, Meneja wa City, Pep Guardiola, aliwaondoa Mafulbeki wote wa Kulia, Pablo Zabaleta na Bacary Sagna, AKEna hadi sasa hajasaini Mpya kuziba nafasi hiyo.

Mbali ya Walker, pia upo uwezekano wa Dani Alves, ambae Juzi amethibitishwa kuachwa na Mabingwa wa Italy Juventus, kutua City.

AKE AONDOKA CHELSEA

Bournemouth wamemsaini Mchezaji wa Chelsea Nathan Ake kwa Dau la Pauni Milioni 20.

Beki huyo alikuwa kwa Mkopo huko Bournemouth kwa Nusu Msimu kabla kurudishwa Stamford Bridge na Antonio Conte Mwezi Januari.

Lakini, aliporudi Chelsea, Ake aliichezea Mechi 5.