ROMELU LUKAKU: SASA RASMI KABISA ASAINI MAN UNITED!

KLABU KIGOGO ya Manchester United imethibitisha kuwa Straika Romelu Lukaku sasa ni Mchezaji wao rasmi baada ya kusaini Mkataba wa Miaka Mitano.

Man United imewalipa Everton Pauni Milioni 75 na inasemekana Dau hilo litapanda kwa nyongeza ya Pauni Milioni 15 kutegemea na kufikiwa kwa Vipengele kadhaa vinavyohusiana na mafanikio na Mechi atakazocheza.

MANUNITED LUKAKU ASAINIMabingwa wa England Chelsea walitaka sana kumrejesha kwao Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Belgium mwenye Miaka 24 lakini mwenyewe akaichagua Man United.

Chelsea walimsaini kutoka Anderlecht Agosti 2011 kwa Pauni Milioni 18.

Baadae Lukaku akakopeshwa kwa West Bromwich Albion na Everton kabla Julai 2014 Everton kuilipa Chelsea Pauni Milioni 20 na kumnunua moja kwa moja.

Akiongea mara baada ya Lukaku kusaini Mkataba, Meneja wa Man United Jose Mourinho ameeleza: “Romelu ni Mchechaji stahiki kwa Man United. Ana haiba kubwa na ni Mchezaji mubwa. Ni kawaida yeye kutaka kuendeleza Soka lake kwenye Klabu kubwa. Ni nyongeza safi sana kwa Kikosi chetu. Nangojea kwa hamu kufanya nae kazi tena.”

Nae Lukaku, ambae Mkataba wake na Man United una Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja, ameeleza: “Pale Manchester United na Jose Mourinho walipokuja kugonga Mlangoni kwangu, nikajua ni nafasi pekee katika maisha yangu na sikuweza kuikataa. Nangoja kwa hamu kubwa kutinga Old Trafford mbele ya Mashabiki 75,000!”

Kwa sasa Lukaku yupo huko USA ambako atajiunga na Kikosi cha Man United kilichokwenda huko kwa ajili ya matayarisho ya Msimu Mpya.

LUKAKU – TAKWIMU:

-Msimu uliopita Lukaku, aliifungia Everton Bao 2 Mwezi Machi na kufikisha Bao 20 za Ligi kwa Msimu Mmoja na kuikamata Rekodi ya Gary Lineker aliyoiweka Msimu wa 1985/86 akiichezea Everton.

-Lukaku ni Mchezaji wa 4 kufunga Bao zaidi ya 80 katika EPL, LIGI KUU ENGLAND, kabla kutimiza Umri wa Miaka 24 wengine wakiwa ni Michael Owen, Robbie Fowler na Wayne Rooney.

-Katika Historia ya EPL, Lukaku ndie Mchezaji pekee wa Everton aliefunga Bao nyingi, 68.

-Lukaku ni mmoja wa Wachezaji Watatu wa EPL ambao wamemudu kufunga zaidi ya Bao 10 kila Msimu katika Misimu Mitano iliyopita na wengine ni Olivier Giroud na Sergio Aguero.

MANCHESTER UNITED – MSIMU MPYA 2017/18: LEO MOURINHO ARUKA NA 27 ZIARANI USA!

MENEJA wa Manchester United Jose Mourinho ameteua Wachezaji 27 kwenda Los Angeles, United States of America kwa Ziara ya Mazoezi na Mechi za Kujipima nguvu kabla kuuanza Msimu Mpya wa 2017/18 Mwezi Agosti.

MANUNITED ZIARANIMiongoni mwa hao 27 ni Mchezaji Mpya Victor Lindelof na Chipukizi Scott McTominay na Demetri Mitchell.

Wakiwa huko USA, Man United watacheza Mechi 5.

Mechi ya kwanza ni Jumamosi ijayo dhidi ya LA Galaxy na Masaa 48 kuivaa Real Salt Lake.

Kisha zitafuata Mechi dhidi ya Manchester City, hapo Julai 20 huko Houston, ikiwa Mechi ya kwanza na Mahasimu wao hao nje ya England, na kisha kucheza na Real Madrid Julai 23 huko Santa Clara na Barcelona hapo Julai 26 huko Washington DC.

Baada kuondoka USA, Man United watacheza Mechi 2 Nchini Norway na Ireland dhidi ya Valerenga hapo Julai 30 huko Oslo na Sampdoria ya Italy huko Dublin hapo Agosti 2.

Mbali ya Kikosi hicho cha Wachezaji 27, Mchezaji Mpya Romelu Lukaku anatarajiwa kujiunga nao baada ya kukamilika taratibu zote za Uhamisho wake kutoka Everton.

MAN UNITED – KIKOSI KILICHOPAA LEO: De Gea, Romero, J Pereira, Valencia, Darmian, Fosu-Mensah, Bailly, Blind, Jones, Smalling, Lindelof, Tuanzebe, Rojo, Shaw, Mitchell, Young, Carrick, Fellaini, Herrera, McTominay, Pogba, Lingard, Mkhitaryan, Mata, A Pereira, Martial, Rashford.

Manchester United – Mechi za Matayarisho:

15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles

17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah

20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup)

23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup)

26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup)

30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo

2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin

8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup) 

NI RASMI LUKAKU YU MAN UNITED!

LUKAKU BEL9KLABU ya Manchester United imetoa tamko kwenye Tovuti yao kuwa wamekubaliana Ada ya Uhamisho na Everton ya Straika Romelu Lukaku.

Wamesema Uhamisho huo sasa unasubiri upimwaji Afya na kwa Mchezaji huyo kuafikiana na Man United kuhusu Maslahi Binafsi.
TAARIFA YA MAN UNITED:

MAN UNITED AGREE FEE WITH EVERTON FOR LUKAKU

Manchester United is delighted to announce that it has agreed a fee with Everton for the transfer of Romelu Lukaku. The transfer is subject to a medical and personal terms.

A further announcement will be made in due course.

 

HABARI KAMILI BAADAE.

ROMELU LUKAKU: CHELSEA YATOA OFA KWA EVERTON KAMA YA MAN UNITED, £75M!

Chelsea wametoa Ofa ile ile kama iliyotolewa na Manchester United ya Pauni Milioni 75 kumnunua Straika Romelu Lukaku.

Bosi wa Chelsea Antonio Conte amekuwa akiisisitizia Bodi ya Chelsea kuwa Lukaku ndie Sentafowadi anaemtaka na sasa wakuu hawa wamejibu mapigo ya Man united.

EVERTON LUKAKU GOLILakini hisia ndani ya Kambi ya Stamford Bridge ni kuwa Wakala wa Lukaku, Mino Raiola, ndie mwenye Trufu na anataka Mbelgiji huyo aende Man United licha kudaiwa Mchezaji mwenyewe anngependelea Chelsea ambako alikuwepo kabla kutolewa kwa Mkopo kwa Everton na hatimaye kuuzwa huko huko.

Chelsea walimsaini kutoka Anderlecht Agosti 2011 kwa Pauni Milioni 18.

Baadae Lukaku akakopeshwa kwa West Bromwich Albion na Everton kabla Julai 2014 Everton kuilipa Chelsea Pauni Milioni 20 kumnunua moja kwa moja.

Uamuzi huu wa Chelsea kutoa Ofa hii kwa sasa kutaanzisha ‘Vita ya Madau’ kati ya Klabu hizo kubwa zenye uwezo Kifedha na watakaonufaika haswa ni Everton, Wakala Mino Raiola na Lukaku mwenyewe.

++++++++++++++++++++++++

Wasifu:

Jina kamili: Romelu Menama Lukaku

Kuzaliwa: 13 Mei 1993 (Miaka 24)

Mahali: Antwerp, Belgium

Timu za Vijana

1999–2003   Rupel Boom

2003–2004   KFC Wintam

2004–2006   Lierse

2006–2009   Anderlecht

Timu za Wakubwa

2009–2011   Anderlecht Mechi 73 Goli (33)

2011–2014   Chelsea 10 (0)

2012–2013   West Bromwich Albion (Mkopo) 35 (17)

2013–2014   Everton (Mkopo) 31 (15)

2014– Everton 110 (53)

Belgium - Timu ya Taifa

2008   Belgium U15 Mechi 4 Goli (1)

2011   Belgium U18 1       (0)

2009   Belgium U21 5      (1)

2010– Belgium       57     (2)

++++++++++++++++++++++++

MPYA: MAN UNITED YAKUBALI KULIPA £75M KUMNUNUA LUKAKU!

=LUKAKU KUTUA OLD TRAFFORD KABLA WIKIENDI!

EVERTON LUKAKU GOLIManchester United wameafiki kulipa Ada inayodaiwa kuw Pauni Milioni 75 ili kumnunua Straika wa Everton Romelu Lukaku.

Kwa kumpata Lukaki sasa inaaminka Man United itaacha kabisa kumfuatilia Straika wa Spain anaechezea Real Madrid Alvaro Morata.
Mpasuko wa Habari hizi Mpya pia umesisitiza kununuliwa kwa Lukaku hakuhusiani na Dili yeyote ya Wayne Rooney kuondoka Man United kwenda Everton.
Uhamisho wa Lukaku kwenda Man United unatarajiwa kukamilika kabla Jumapili.
++++++++++++++++++++++++

Wasifu:

Jina kamili: Romelu Menama Lukaku

Kuzaliwa: 13 Mei 1993 (Miaka 24)

Mahali: Antwerp, Belgium

Timu za Vijana

1999–2003   Rupel Boom

2003–2004   KFC Wintam

2004–2006   Lierse

2006–2009   Anderlecht

Timu za Wakubwa

2009–2011   Anderlecht Mechi 73 Goli (33)

2011–2014   Chelsea 10 (0)

2012–2013   West Bromwich Albion (Mkopo) 35 (17)

2013–2014   Everton (Mkopo) 31 (15)

2014– Everton 110  (53)

Belgium - Timu ya Taifa

2008   Belgium U15 Mechi 4 Goli (1)

2011   Belgium U18 1       (0)

2009   Belgium U21 5      (1)

2010– Belgium       57     (2)

++++++++++++++++++++++++