ARSENAL ZIARA AUSTRALIA: WAICHAPA WESTERN SYDNEY 3!

ARSENAL ZIARA AUSTRALIAMBELE YA Mashabiki 83,221 ndani ya ANZ Stadium Mjini Sydney huko Australia, Arsenal wameshinda Mechi yao ya pili mfululizo ya Ziara yao kwa kuichapa Western Sydney Wanderers 3-1.

Majuzi, Arsenal, wakiwa Uwanja huo huo, waliifunga Sydney FC 2-0 huku Bao lao la Pili likifungwa na Mchezaji wao Mpya Alexandre Lacazette baada kuingizwa Kipindi cha Pili.

Leo Lacazette alianza lakini hakufunga Bao.

Arsenal waliongoza 3-0 kwa Bao za Olivier Giroud, Dakika ya 33, Aaron Ramsey, 38, na Mohamed Elneny, 44.

Bao pekee la Western Sydney lilifungwa Dakika ya 55 na Lustica.

Arsenal sasa watapaa hadi China kucheza Mechi mbili na Bayern Munich hapo Julai 19 huko na kisha Julai 22 kuivaa Chelsea Mjini Beijing.

Baada ya Mechi hizo, Arsenal itarudi kwao London kushiriki Kombe lao la Emirates Cup na kucheza dhidi ya Benfica na Sevilla.

VIKOSI VILIVYOANZA:

WESTERN SYDNEY: Janjetovic; Clisby, Hamill, Cornthwaite, Risdon; Melling, Baccus; Bonevacia; Lustica, Jumpei, Majok

ARSENAL:  Ospina; Koscielny, Elneny, Monreal; Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Xhaka, Maitland-Niles; Iwobi, Lacazette, Giroud

Arsenal

13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]

15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]

19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Cup

22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)

29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)

30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)

6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)

MANCHESTER UNITED NA CITY KUVAA NEMBO YA NYUKI!

MANCHESTER NYUKITIMU za Manchester United na City zitawaenzi Wahanga wa Mlipuko wa Bomu uliotokea Manchester Arena kwa kuvaa Jezi zenye Nembo ya Nyuki katika Mechi kati yao.

Baada ya Mechi hiyo Jezi hizo zitapigwa Mnada ili Mapato yake yaende kwenye Mfuko wa Hisani wa Kusaidia Wahanga wa Maafa hayo uitwao We Love Manchester Emergency Fund.

Mfuko huo umeshakusanya Zaidi ya Pauni Milioni 12 kusaidia Maafa hayo yaliyotokea Mei 22 na kuua Watu 22.

Man United na City zitavaa Jezi zenye Nembo ya Nyuki kwenye Dabi yao itakayochezwa Julai 20 huko Houston, USA ikiwa ni Dabi ya kwanza kati yao kuchezwa nje ya England.

Nembo ya Nyuki imekuwa ndio Alama ya Mshikamano kwa Watu wa Jiji la Manchester na imetumika sana tangu Maafa hayo huku wengine wakijichora Miilini mwao kwa Tattoo.

Imeeleza ‘Nyuki Mfanyakazi’ ndio Alama ya Asilia ya Jiji la Manchester tangu zama za Karne zilizopita ikisisitiza Jiji la Wafanyakazi wa kawaida waliohenya kulijenga Jiji hilo.

Mtendaji Kuu wa Man City, Soriano, ameeleza: “Alama ya Nyuki Mfanyakazi ni alama inayoonyesha kila kitu kuhusu Manchester na Wachezaji wetu watavaa Nembo ya Nyuki kwa fahari kubwa na mshikamano kwa Jamii ya Manchester.”

Nae Ed Woodward, Mwenyekiti Mtendaji wa Man United, ameeleza Jiji la Manchester limeonyesha nguvu na umoja tangu mashambulizi hayo ya Mabomu na kuionyesha Dunia kwamba Mji huo ni spesho.

Aliongeza: “Kwa kuvaa Nembo ya Nyuki, tutaonyesha ari ya Jamii yetu katika Mji wetu na Klabu zetu!”

WALKER AIKARIBIA CITY, CHALOBAH ATIMKA CHELSEA!

UHAMISHO ENGLAND:

Kyle Walker: Man City wakaribia kumsaini Fulbeki wa Tottenham

WALKER CITYManchester City wanakaribia kukamilisha wa Fulbeki wa Tottenham na England Kyle Walker.

Walker, mwenye Miaka 27, anatarajiwa Leo kupimwa Afya huko Etihad na kukamilisha Uhamisho huu baada ya Klabu hizo mbili kuafikiana Dau la Uhamisho la Pauni Milioni 50 na nyongeza kadhaa.

Walker, ambae alijiunga na Tottenham kutoka Sheffield United Mwaka 2009, atajiunga na Kikosi cha City Jumatatu ijayo tayari kwa safari ya USA.

Meneja wa City, Pep Guardiola, alimtaka Walker aje kuziba mapengo ya Mafulbeki wa Kulia, Pablo Zabaleta na Bacary Sagna, waliotemwa Hivi karibuni.

Walker ameichezea Spurs Mechi 183 za EPL, LIGI KUU ENGLAND, na pia kuichezea Timu ya Taifa ya England Mechi 27.

Mchezaji huyu atakuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Man City katika kipindi hiki wengine wakiwa ni Kiungo Bernardo Silva na Kipa Ederson Moraes.

Nathaniel Chalobah: Watford yamsaini Kiungo wa Chelsea

Watford imemsaini Kiungo Nathaniel Chalobah wa Chelsea kwa Mkataba wa Miaka Mitano bila Ada ya Uhamisho kutajwa.

Chalobah, mwenye Miaka 22, alikuwemo kwenye Kikosi cha England cha U-21 kilichofika Nusu Fainali kwenye Mashindano ya Vijana ya Ulaya.

Msimu uliopita, aliichezea Chelsea Mechi 10 za EPL, LIGI KUU ENGLAND.

Kwenye Msimu wa 2012/13, Chalobah alikuwepo Watford kwa Mkopo na kucheza Mechi 42 na pia kutolewa nje ya Chelsea kwa Mkopo mara 5 na ya mwisho alikuwa huko Italy akiichezea Napoli.

Chalobah amecheza Mechi 97 kwa Timu za Taifa za Vijana za England za ngazi mbalimbali.

IVAN PERISIC AITAKA MAN UNITED, INTER KIZINGITI!

Ivan Perisic anataka sana kujiunga na Manchester United lakini Klabu yake Inter Milan inaleta ugumu.
Jana Wakala wa Perisic alikutana na Viongozi wa Inter kujadili Uhamisho huo kwa mujibu wa Sky Sports News HQ.
PERISIC CROATIATatizo kubwa ni Dau la Uhamisho ambapo Inter wameshikilia walipwe Pauni Milioni 48 kwa Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Croatia.
Man United wametoa Ofa ya Pauni Milioni 39 ambayo Inter wameikataa.
Hivi sasa Perisic yuko kwenye Kikosi cha Inter kilichopiga Kambi ya Mazoezi huko Kaskazini ya Italy na Wiki ijayo kinaruka kwenda Ziarani huko China.
Pande zote mbili, Inter na Man United, wanataka maafikiano yafikiwe kabla Inter kwenda kwenye Tripu yao.
Perisic amekuwa akicheza huko Italy tangu 2015 akipiga Bao 18 katika Mechi 70 za Ligi Serie A baada ya kujiunga na Inter toka Klabu ya Germany Wolfsburg.
Staa huyo mwenye Miaka 28 ameifungia Nchi yake Croatia Bao 16 katika Mechi 57.

ERIC DIER AIPASULIA SPURS - NATAKA KWENDA MAN UNITED KWA MOURINHO!

ERIC DIERKIUNGO Eric Dier ameishitua Klabu yake Tottenham Hotspur kwa kuwapasulia kuwa anataka kujiunga na Manchester United ili afanye kazi na Jose Mourinho.
Baada ya kumkosa Kiungo wa Chelsea Nemanja Matic kwa sababu ya 'kuwapora' Romelu Lukaku, sasa Man United wapo njiani kuwasilisha Ofa ya Dau la Pauni Milioni 40 kumnunua Dier.
Lakini Dau hilo lipo chini ya Pauni Milioni 60 ambazo Spurs ndizo wanazoona ndio thamani halisi ya Eric Dier mwenye Miaka 23.
Hata hivyo, Man United wanaamini watafikia muafaka na Spurs ingawa wanamhofu Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy ambae ni mgumu mno kufanya nae biashara.
Hilo lilionekana wakati Man United walipowanunua kutoka Spurs Michael Carrick Mwaka 2006 na Dimitar Berbatov Mwaka 2008 na dili hizo kukamilishwa kwa mbinde na kwa bei ghali mno.
Lakini safari hii presha ya Mchezaji mwenyewe Dier kutaka kuhama huenda ikawasaidia mno Man United.
Tayari Dier ameshawaambia Maswahiba wa karibu yake kuwa anafurahia kufanya kazi na Mourinho.
Pia, mvuto mkubwa kwake Dier kwenda Man United ni kuongezeka mno kwa Mshahara wake kutoka Pauni 70,000 anazopata sasa huko Spurs na kupanda hadi zaidi ya Pauni 150,000 atakazopata akijiunga na Man United.