UEFA EUROPA RAUNDI YA MTOANO: ZLATAN IBRAHIMOVIC HETITRIKI, MAN UNITED SAFI!

> GENK YA MBWANA SAMATTA 2-2 UGENINI NA ASTRA GIURGIU!

MANUNITED-IBRA-STETIENNEManchester United wakiwa kwao Old Trafford wameitwanga St-Etienne ya France 3-0 kwa Hetitriki ya Zlatan Ibrahimovic katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.

Bao hizo ziliendeleza Rekodi ya Zlatan Ibrahimovic ya kuibamiza St-Etienne kila akikutana nayo Rekodi ambayo aliiweka akiwa na Paris St-Germain ambako alifunga Bao 14 katika Mechi 13 dhidi yao.

Mvuto mwingine wa Mechi hii ni kupambanishwa kwa Mtu na Kaka yake Paul Pogba wa Man United na Kaka Mkubwa Florentin Pogba Beki wa St-Etienne ambae hakudumu Dakika 90 baada ya kuumia Dakika ya 79 na kubadilishwa huku Mdogo Mtu akikosa Bao kadhaa na kupiga Posti pia.

Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 15 kwa Frikiki ya Zlatan Ibrahimovic iliyombabatiza Mchezaji wa St-Etienne Pajot na kutinga.

Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.

Kipindi cha Pili Zlatan Ibrahimovic alifunga Bao nyingine 2 katika Dakika za 75 baada ya kazi njema ya Marcus Rashford na jingine Penati ya Dakika ya 88 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye boksi.MANUNITED-POGBAvPOGBA

Timu nyingine ya England ambayo iko EUROPA LIGI ni Tottenham ambayo ilifungwa 1-0 na Klabu ya Belgium Gent.

Nayo Klabu ya Straika wa Tanzania, Mbwana Samatta, Genk ya Belgium imetoka Sare 2-2 na Astra Giurgiu ya Romania kwenye Mechi iliyochezwa huko Nchini Romania na Wenyeji hao kunusurika kipigo kwa kusawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la Takayuki Seto.

Kwenye Mechi hiyo, ambayo Samatta alicheza Dakika zote 90, Genk walitangulia kufunga Dakika ya 25 kwa Bao la Timoty Castagne 25 na Astra kusawazisha Dakika ya 43 kwa Goli la Constantin Budescu 43.

Leandro Trossard, Dakika ya 83, allipa Genk Bao la Pili.

Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zitachezwa Alhamisi Februari 23.

VIKOSI:

Manchester United: Romero, Valencia, Smalling, Bailly, Blind, Mata [Rashford, 69’], Herrera, Fellaini [Lingard 45'], Martial [Young, 84’], Pogba, Ibrahimovic.
Akiba: de Gea, Rojo, Lingard, Young, Rashford, Schweinsteiger, Darmian.

Saint-Étienne: Ruffier, Malcuit, Perrin, Theophile-Catherine, Pogba [Beric, 79’], Jorginho, Veretout, Pajot [Selnaes, 70’], Monnet-Paquet [Roux 65'], Saivet, Hamouma.
Akiba: Moulin, Lacroix, Roux, Selnaes, Lemoine, Beric, Pierre Gabriel.

REFA: Pavel Královec (Czech Republic)

UEFA EUROPA LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 32

Mechi za Kwanza

Matokeo:

Krasnodar 1 Fenerbahce 0

AZ Alkmaar 1 Lyon 0

Celta Vigo 0 Shakhtar Donetsk 1

Borussia Monchengladbach 0 Fiorentina 1

Olympiakos 0 Osmanlispor 0

KAA Gent 1 Tottenham Hotspur 1

FK Rostov 4 Sparta Prague 0

Astra Giurgiu 2 Genk 2

Ludogorets 1 FC Copenhagen 2

Athletic Bilbao 3 Apoel Nicosia 2

Legia Warsaw 0 Ajax 0

Anderlecht 2 Zenit St Petersburg 0

Manchester United 3 Saint-Etienne 0

Villarreal 0 AS Roma 4

Hapoel Beer Sheva 1 Besiktas 3

PAOK 0 Schalke 3

UEFA EUROPA LIGI

Tarehe Muhimu:

16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza

23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano

09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza

16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza