UEFA EUROPA RAUNDI YA MTOANO: MAN UNITED KUIVAA ST-ETIENNE ALHAMISI!

>NI TIMU YA KAKA YAKE POGBA, GENK YA MBWANA SAMATTA NA ASTRA GIURGIU YA ROMANIA!

MANUNITED-POGBAvPOGBAALHAMISI Usiku, Manchester United wako kwao Old Trafford kucheza na St-Etienne ya France ikiwa ni Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.

St-Etienne, Timu ambayo Man United walikutana nayo kwa mara ya mwisho Mwaka 1977, ni Timu ambayo Kaka wa Kiungo wa Man United, Paul Pogba, anachezea ambae huitwa Florentin.

Mwaka huo 1977, Man United walitoka na St-Etienne 1-1 huko France na kuifunga 2-0 England katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Plymouth Argyle, Home Park, badala ya Old Trafford iliyofungiwa na UEFA kutokana na vurugu huko France katika Mechi ya kwanza.

Hili ni Kombe pekee la Ulaya ambalo Man United hawajawahi kulitwaa na litawakutanisha kwenye Mechi kwa mara ya kwanza Mtu na Kaka yake, Paul akiwa mdogo na wa kwanza ni Florentin Pogba ni mubwa na hucheza kama Beki.

Wakati Man United iko chini ya Meneja mzoefu Jose Mourinho, St-Etienne inaongozwa na Kocha Christophe Galtier tangu 2009 na Msimu wa 2012/13 aliiongoza Timu hiyo kutwaa Kombe la Ligi la France.

Hivi sasa St-Etienne wanakamata Nafasi ya 5 kwenye Ligi 1 huko France wakati Man United ni wa 6 kwenye EPL, Ligi Kuu England.

++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-Manchester United wamepoteza Mechi 1 tu kati ya 16 walizocheza mwisho na Klabu za France Wakishinda 9 na Sare 6.

-Straika wa Man United United Zlatan Ibrahimovic ambae alitokea Paris St-Germain ya France amefunga Bao 14 katika Mechi 13 dhidi ya St Etienne, ikiwa ni idadi kubwa kupita Timu yeyote nayo aliyokutana huko France.

++++++++++++++++++

Timu nyingine ya England ambayo iko EUROPA LIGI ni Tottenham ambayo itacheza na Klabu ya Belgium Gent.

Nayo Klabu ya Straika wa Tanzania, Mbwana Samatta, Genk ya Belgium imepangiwa Astra Giurgiu ya Romania.

Mechi hizo za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zitachezwa Alhamisi Februari 23.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

MAN UNITED: David de Gea, Eric Bailly, Matteo Darmian, Luke Shaw, Chris Smalling, Michael Carrick, Ander Herrera, Henrikh Mkhitaryan, Paul Pogba, Anthony Martial, Wayne Rooney

ST-ÉTIENNE: Stéphane Ruffier, Léo Lacroix, Kévin Malcuit, Florentin Pogba, Pierre-Yves Polomat, Kévin Théophile-Catherine, Bryan Dabo, Arnaud Nordin, Henri Saivet, Kévin Monnet-Paquet, Alexander Søderlund

REFA: Pavel Královec (Czech Republic)

UEFA EUROPA LIGI

Raundi ya Mtoano ya Timu 32

Mechi za Kwanza

**Saa za Bongo

1900 Krasnodar v Fenerbahce

2100 AZ Alkmaar v Lyon

2100 Celta Vigo v Shakhtar Donetsk

2100 Borussia Monchengladbach v Fiorentina

2100 Olympiakos v Osmanlispor

2100 KAA Gent v Tottenham Hotspur

2100 FK Rostov v Sparta Prague

2100 Astra Giurgiu v Genk

2100 Ludogorets v FC Copenhagen

2305 Athletic Bilbao v Apoel Nicosia

2305 Legia Warsaw v Ajax

2305 Anderlecht v Zenit St Petersburg

2305 Manchester United v Saint-Etienne

2305 Villarreal v Roma

2305 Hapoel Beer Sheva v Besiktas

2305 PAOK v Schalke

UEFA EUROPA LIGI

Tarehe Muhimu:

16/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Mechi za Kwanza

23/02/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Marudiano

09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza

16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano

13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza