EPL: MABINGWA LEICESTER JAHAZI LATOTA, WAIFIKIA REKODI YA CHELSEA YA 1956 KUCHAPWA MECHI 5 MFULULIZO!

EPL – Ligi Kuu England

LEICESTER-JAHAZI-LATOTARatiba/Matokeo:

Jumapili Februari 12

Burnley 1 Chelsea 1

Swansea City 2 Leicester City 0   

++++++++++++++++++++

MABINGWA WATETEZI wa England Leicester City sasa ni wazi hawawezi tena kutetea Ubingwa wao na kilichobaki ni vita ya kujinusuru kushuka Daraja baada ya Leo kupokea kipigo chao cha 5 mfululizo kwenye EPL, Ligi Kuu England huku wakiwa hawajafunga hata Bao kwenye Ligi Mwaka huu 2017.

Bao 2 za kabla ya Haftaimu, zilizofungwa na Alfie Mawson na Martin Olsson ziliwapa Swansea City ushindi wa 2-0 wakiwa Uwanja wa Nyumbani kwao Liberty Stadium.

++++++++++++++++++++

JE WAJUA?

-Leicester City, ndio Mabingwa wa Kwanza Watetezi wa England kufungwa Mechi 5 mfululizo tangu Chelsea wafanye hivyo Mwaka 1956.

++++++++++++++++++++

Kipigo hiki kimewashusha Leicester hadi Nafai ya 17 wakiwa juu tu ya Timu 3 za mkiani na Pointi 1 tu juuEPL-FEB12B yao na hali hii kuhatarisha usalama wao kubaki EPL mwishoni mwa Msimu kwani Timu 3 za mkiani ndizo huporomoka Daraja.

Kwa Swansea, ushindi huu ni ahueni kwani mwanzoni mwa Mwaka walikuwa mkiani na ujio wa Meneja wao mpya Paul Clement sasa umewapandisha hadi Nafasi ya 15.

VIKOSI:

SWANSEA CITY: Fabianski, Naughton, Fernandez, Mawson, Olsson, Fer, Cork, Carroll, Dyer, Llorente, Sigurdsson

Akiba: Ayew, Amat, Nordfeldt, Routledge, Rangel, Narsingh, Kingsley.

LEICESTER CITY: Schmeichel, Simpson, Huth, Morgan, Fuchs, Drinkwater, Ndidi, Mahrez, Gray, Albrighton, Vardy

Akiba: Chilwell, Musa, King, Amartey, Slimani, Okazaki, Zieler.

REFA: Jon Moss

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

Jumatatu Februari 13

2300 Bournemouth v Manchester City   

Jumamosi Februari 25

1800 Chelsea v Swansea City               

1800 Crystal Palace v Middlesbrough              

1800 Everton v Sunderland         

1800 Hull City v Burnley             

Southampton v Arsenal [IMEAHIRISHWA]

1800 West Bromwich Albion v Bournemouth              

2030 Watford v West Ham United         

Jumapili Februari 26

1630 Tottenham Hotspur v Stoke City             

Manchester City v Manchester United [IMEAHIRISHWA]

Jumatatu Februari 27

2300 Leicester City v Liverpool             

Jumamosi Machi 4

1530 Manchester United v Bournemouth         

1800 Leicester City v Hull City              

1800 Stoke City v Middlesbrough          

1800 Swansea City v Burnley                

1800 Watford v Southampton               

1800 West Bromwich Albion v Crystal Palace             

2030 Liverpool v Arsenal            

Jumapili Machi 5

1630 Tottenham Hotspur v Everton       

1900 Sunderland v Manchester City      

Jumatatu Machi 6

2300 West Ham United v Chelsea