DABI LONDON – DELE ALLI AITUMBUA CHELSEA, NDOTO ZAO KUFYATUA REKODI YAYU!

SPURS-CHELSEA-DELEDabi ya Jiji la London ilipigwa Uwanjani White Hart Lane na Tottenham Hotspur kuibuka kidedea kwa ushujaa wa Dele Alli kuwabwagaVinara wa EPL, Ligi Kuu England,ChelseaBao 2-0 na kuifyeka ndoto yao ya kuweka Rekodi ya ushindi wa Mechi 14 mfululizo kwenye Ligi hiyo.

Huku Timu zote zikitumia Mfumo wa aina moja, 3-4-3, Gemu ilichezwa sana kati kulikokuwa na lundo la la Wachezaji lakini Kipindi cha Kwanza chote Spurs walionekana wako ngangari na kutawala na kuleta kosakosa kadhaa langoni mwa Chelsea.

Presha yao ilitoa majibu pale Walker alipochomoka na Mpira na kumzidi maarifa Alonso na kisha kumrudishia Mpira Eriksen alietoa Krosi iliyounganishwa na Dele Alli kwa Kichwa ikimwacha Kipa Courtois akilala hoi na kutinga wavuni kuwaandikia Bao Dakika ya 46.

Hadi Haftaimu, Spurs 1 Chelsea 0.EPL-JAN5

Dakika ya 53, Spurs wakaenda 2-0 mbele baada ya Krosi ya Eriksen kuunganishwa kwa Kichwa na Dele Alli hadi wavuni.

+++++++++

JE WAJUA?

-Tottenham wameshinda Mechi 5 tu kati ya Mechi 49 za Ligi dhidi ya Chelsea wakitoka Sare 19 na Kufungwa 26 lakini Mechi zao zote 5 za ushindi zilikuwa Uwanjani White Hart Lane.

-Katika Mechi 10 zilizopita za EPL Uwanjani White Hart Lane, Chelsea wameshinda mara 1 tu, 4-2 hapo Oktoba 2012 nyingine ni Sare 5 Kufungwa 5.

+++++++++

Hii ilikuwa ni Mechi ya mwisho ya EPL baada kuchezwa Mechi mfululizo toka Krismasi na sasa inaenda Vakesheni kupisha Mechi za Raundi ya 3 ya FA CUP zinazoanza Ijumaa Usiku.

EPL itarejea dimbani Jumamosi Januari 14.

VIKOSI:

Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Alderweireld, Vertonghen, Walker, Wanyama, Dembele [Winks, 74’], Rose, Alli [Sissoko, 86’], Eriksen, Kane [Son Heung-min, 92’]

Akiba: Son Heung-min, Vorm, Trippier, Sissoko, Wimmer, Winks, Davies

Chelsea: Courtois, Azpilicueta, David Luiz, Cahill, Moses [Batshuayi, 85’], Kante [Fabregas, 79’], Matic, Alonso [Alonso, 65’], Pedro, Diego Costa, Hazard

Akiba: Begovic, Ivanovic, Fàbregas, Zouma, Willian, Batshuayi, Chalobah

REFA: Martin Atkinson

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumamosi Januari 14

1530 Tottenham Hotspur v West Bromwich Albion     

1800 Burnley v Southampton               

1800 Hull City v Bournemouth              

1800 Sunderland v Stoke City               

1800 Swansea City v Arsenal                

1800 Watford v Middlesbrough             

1800 West Ham United v Crystal Palace           

2030 Leicester City v Chelsea                

Jumapili Januari 15

1630 Everton v Manchester City

1900 Manchester United v Liverpool