EPL: LEO WHITE HART LANE JIJINI LONDON NI DABI SPURS v CHELSEA!

>CHELSEA KUFYATUA REKODI USHINDI MECHI 14 MFULULIZO?

>PATA TATHMINI!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea

+++++++++++++++++++++++++++++

SPURS-CHELSEALEO ni Dabi ya Jiji la London Uwanjani White Hart Lane wakati Tottenham Hotspur wakiivaa Chelsea ambao ni Vinara wa EPL, Ligi Kuu England, walio kwenye wimbi la ushindi Mechi 13 mfululizo wakisaka ushindi ili kuweka Rekodi ya kushinda Mechi nyingi mfululizo ndani ya Msimu mmoja.

Hii ni mara ya pili kwa Timu hizi kukutana katika EPL na katika Mechi ya kwanza huko Stamford Bridge, Chelsea iliifunga Spurs 2-1.

Msimu uliopita, kwenye Mechi kama hii Uwanjani White Hart Lane, Timu hizi zilitoka 0-0.

Chelsea, chini ya Meneja kutoka Italy Antonio Conte, wanaongoza EPL wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 19 wakifuatia Liverpool wenye Pointi 44 kwa Mechi 20.

Spurs, chini ya Meneja kutoka Argentina Mauricio Pochettino, wao wapo Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 39 kwa Mechi 19.

Msisimko kwa Mechi hii ni kuona Mastraika hatari wa Timu hizi, Harry Kane wa Spurs mwenye Bao 10, na Diego Costa, mwenye Bao 14, wakichacharika kuipa ushindi Timu yao.

Hali za Timu

Chelsea watakuwa nae Kikosini Pedro ambae alikuwa Kifungoni na pengine pia kumtumia Kiungo Nemanja Matic aliepumzishwa Mechi iliyopita walipoifunga Stoke City lakini Nahodha wao John Terry bado ni Majeruhi.EPL-JAN4

Nao Spurs wanaweza kuwa nao Wachezaji wao Wawili waliomaliza Kifungo, Kyle Walker na Jan Vertonghen, ambao waliikosa Mechi yao iliyopita waliyoifunga Watford pamoja na Mousa Dembele aliepumzishwa lakini watamkosa Majeruhi Erik Lamela.

Uso kwa Uso:

-Tottenham wameshinda Mechi 4 tu kati ya Mechi 49 za Ligi dhidi ya Chelsea wakitoka Sare 19 na Kufungwa 26 lakini Mechi zao zote 4 za ushindi zilikuwa Uwanjani White Hart Lane.

-Katika Mechi 10 zilizopita za EPL Uwanjani White Hart Lane, Chelsea wameshinda mara 1 tu, 4-2 hapo Oktoba 2012 nyingine ni Sare 5 Kufungwa 4.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

TOTTENHAM: Lloris, Trippier, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Dier, Wanyama, Eriksen, Alli, Son, Kane

Akiba kutokana na: Vorm, López, Davies, Wimmer, Carter-Vickers, Carroll, Winks, Onomah, Sissoko, Nkoudou, Janssen

CHELSEA: Courtois, Azpilicueta, David Luiz, Cahill, Matic, Kante, Moses, Alonso, Willian, Costa, Hazard

Akiba kutokana na: Begovic, Eduardo, Ivanovic, Zouma, Aina, Mikel, Pedro, Fàbregas, Van Ginkel, Loftus-Cheek, Chalobah, Solanke, Batshuayi

REFA: Martin Atkinson

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Saturday 14th January 2017

1530 Tottenham Hotspur v West Bromwich Albion     

1800 Burnley v Southampton               

1800 Hull City v Bournemouth              

1800 Sunderland v Stoke City               

1800 Swansea City v Arsenal                

1800 Watford v Middlesbrough             

1800 West Ham United v Crystal Palace           

2030 Leicester City v Chelsea                

Sunday 15th January 2017

1630 Everton v Manchester City

1900 Manchester United v Liverpool                

 

 

Habari MotoMotoZ