EPL: MATA, IBRA WAIMALIZA MTU 10 WEST HAM, MAN UNITED USHINDI MECHI 6 MFULULIZO!

EPL – Ligi Kuu England

Matokeo:

Jumatatu Januari 2

Middlesbrough 0 Leicester City 0           

Everton 3 Southampton 0           

Manchester City 2 Burnley 1                 

Sunderland 2 Liverpool 2            

West Bromwich Albion 3 Hull City 1                

West Ham United 2 Manchester United 0

+++++++++++++++++++++++++++++

WESTHAM-MANUNITED-JONES-FEGHOULIMANCHESTER UNITED wamezoa ushindi wao wa 6 mfululizo kwenye EPL, Ligi Kuu England, kwa kuitandika Mtu 10 West Ham United Uwanjani kwao London Stadium Jijini London Bao 2-0.

Dakika ya 13 West Ham walipata pigo kwa Mchezaji wao kutoka Algeria Sofiane Feghouli kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya aliyomchezea Sentahafu wa Man United Phil Jones.

Licha ya upungufu huo, Timu hizo zilienda Haftaimu zikiwa 0-0 huku wote wakikosa nafasi moja kwa Valencia wa Man United kupiga Posti na Shuti la Lanzini wa West Ham kupanchiwa na Kipa David De Gea.EPL-JAN2B

Meneja wa Man United, Jose Mourinho, aliamua kumtoa Darmian kabla Kipindi cha Pili kuanza na kumuingiza Juan Mata na baadae kumwingiza Marcus Rashford kuchukua nafasi ya Lingard na hao ndio walileta uhai na kuipa ushindi Man United.

Dakika ya 63, kazi njema ya Rashford kwenye Winga ya Kushoto ilimpa nafasi ya kumpasia Mata na kuipa Man United Bao la kwanza.

Dakika ya 78 pasi ya Ander Herrera ilimkuta Zlatan Ibrahimovic aliandika Bao la Pili kwa Man United.

 

Kwa West Ham hiki ni kipigo chao cha 4 London Stadium Uwanja mpya walioanza kuucheza Msimu huu baada ya kuhama Upton Park na wapo Nafasi ya 13 huku Man United wakibakia Nafasi ya 6 lakini wako Pointi sawa na Tottenham iliyo Nafasi ya 5.

VIKOSI:

West Ham: Randolph, Obiang, Reid, Ogbonna, Cresswell, Kouyate [Fernandes, 82’], Nordtveit, Antonio, Feghouli, Payet [Carroll, 68’], Lanzini [Ayew, 88’]

Akiba: Carroll, Adrian, Noble, Ayew, Fletcher, Fernandes, Quina

Man United: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian [Juan Mata, 45’], Ander Herrera, Carrick, Pogba, Mkhitaryan [Smalling, 64’], Ibrahimovic, Lingard [Rashford, 58’]

Akiba: Mata, Martial, Smalling, Young, Rashford, Romero, Fellaini

REFA: Mike Dean

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford          

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea