EPL: LEO MECHI 6, ZIMO CITY-BURNLEY, SUNDERLAND-LIVERPOOL, WEST HAM-MAN UNITED!

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United

+++++++++++++++++++++++++++++

EPL-2016-17-LOGO2MFULULIZO wa Mechi kemkem za EPL, Ligi Kuu England, unendelea Leo kwa Mechi 6.

Mechi ya kwanza kabisa hii Leo Mchana ni huko Riverside kati ya Middlesbrough, maarufu kama Boron a ambao wako Nafasi ya 16, dhidi ya EPL-JAN1Mabingwa Watetezi Leicester City walio Nafasi ya 15 huku Leicester wakiizidi Boro Pointi 2 tu.

Halafu zitafuata Mechi 4 ambazo zote zitaanza Saa 12 Jioni.

Huko Goodison Park Everton walio Nafasi ya 7 watacheza na Timu ya 9 Southampton.

Uwanjani Etihad, Man City, walioshushwa hadi Nafasi ya 5 hapo Jana, wapo vitani kucheza na Burnley, walio Nafasi ya 11, huku City wakiwa na Nafasi ya 3 wakishinda Mechi hii.

Liverpool, walio Nafasi yya Pili, wakiwa Ugenini huko Stadium of Light kucheza na Sunderland, wana nafasi murua kuwakaribia Vinara Chelsea na kuwa Pointi 3 nyuma yao wakishinda Mechi hii.

Mechi ya mwisho katika zile za Saa 12 Jioni ni huko The Hawthorns kati ya Timu ya 8 West Bromwich Albion na Hull City walio Nafasi ya 19 ikiwa ni moja tu toka mkiani.

Mechi ya mwisho hii Leo itachezwa Usiku huko London Stadium Jijini London kati ya West Ham, ambao wako Nafasi ya 12, na Manchester United walio Nafasi ya 6.

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba

**Saa za Bongo  

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford          

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea                 

 

 

Habari MotoMotoZ