FUNGA MWAKA – MAN UNITED v BORO, NI MOURINHO v KARANKA, MARAFIKI WEMA, MAADUI KWA MECHI 1!

MOURINHO-KARANKA

JUMAMOSI Old Trafford itashuhudia Mechi ya mwisho kabisa kwa Mwaka 2016 ya EPL, Ligi Kuu England, kati ya Manchester United na Middlesbrough, ambao ni maarufu kama Boro, lakini pia Mechi hii itakutanisha Mameneja ambao ni Marafiki mno.

Jose Mourinho, Meneja wa Man United, na Aitor Karanka, Meneja wa Boro, ni Marafiki wa dhati ndani na nje ya Soka.

Wawili hao walikuwa pamoja huko Real Madrid kuanzia 2010 kwa Kipindi cha Miaka Mitatu Mourinho akiwa ndie Meneja na Karanka Msaidizi wake na Msimu wa 2011/12 kutwaa Ubingwa wa La Liga.

Karanka amekiri waziwazi kuwa ni Mourinho aliemlea na kumfanya awe Kocha kiasi cha sasa kumfanya akiitazama Man United ahisi kama anaitazama Middlesbrough anaeifundisha yeye kwani mbinu nyingi za Timu hizo hufanana mno.

Lakini Karanka amebainisha kuwa Jumamosi itakuwa tofauti kwa kusema: “Sisi ni Marafiki wa dhati lakini kwa Dakika 90 Jumamosi hatuwezi kuwa Marafiki. Nitajaribu kumshangaza. Lakini ni ngumu kumshangaza Jose, yeye ndie Bora kupita yeyote!”

Tathmini

Kikosi cha Man United kipo kwenye mbio za kutofungwa katika Mechi 11 mfululizo na Jumatatu iliyopita waliitwangaSunderland 3-1 Uwanjani Old Trafford.

Wakicheza Siku hiyo hiyo Jumatatu iliyopita, wakiwa Ugenini, Boro walichapwa 1-0 na Burnley na kuachwa Nafasi ya 15 wakiwa Pointi 15 nyuma ya Man United ambao wako Nafasi ya 6.

Jumamosi, Man United watamkosa Nahodha wao Wayne Rooney kwa Mechi ya Pili mfululizo akiwa bado hajapona maumivu ya Paja akiungana na Majeruhi mwingine Luke Shaw.

Kwa upande wa Boro, wao watawakosa Majeruhi Fischer na Barragán ambae yuko Kifungoni Mechi 1.

Mvuto wa Mechi hii ni kurejea tena Old Trafford kwa Wachezaji Wawili waliowahi kuichezea Man United, Fabio da Silva na Victor Valdes.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

MAN UNITED: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Darmian, Carrick, Herrera, Mkhitaryan, Pogba, Martial, Ibrahimovic

Akiba: Romero, Johnstone, Depay, Lingard, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Schneiderlin, Young, Blind, Fellaini, Schweinsteiger, Rashford, Smalling, Mata, Bailly

MIDDLESBROUGH: Valdes, Da Silva, Chambers, Gibson, Friend, Clayton, De Roon, Forshaw, Traore, Ramirez, Negredo

Akiba: uzan, Ayala, Leadbitter, Stuani, Espinosa, Nsue, Downing, Rhodes, Nugent, De Sart

REFA: Lee Mason

EPL – Ligi Kuu England

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City