EPL: FUNGA MWAKA KUANZA IJUMAA, BIGI MECHI JUMAMOSI LIVERPOOL-CITY!

>VINARA CHELSEA NA STOKE, MAN UNITED NA BORO!

LIVER-CITY-DEC31MECHI za Kufunga Mwaka 2016 za EPL, Ligi Kuu England, zitaanza Ijumaa Usiku huko Kingston Communications Stadium wakati Hull City wakipambana na Everton kwenye Mechi pekee Siku hiyo.

Jumamosi Desemba 31, Mechi 7 za EPL zitauaga rasmi Mwaka 2016 na Bigi Mechi Siku hiyo ni huko Anfield wakati Timu ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi hiyo Liverpool ikikwaana na Manchester City ambao ni wa 3 wakiwa Pointi 1 tu nyuma ya Liverpool.

Siku hiyo hiyo, Vinara Chelsea, wanaoongoza Ligi wakiwa Pointi 6 mbele ya Liverpool, wapo kwao Stamford Bridge kuivaa Stoke City walio Nafasi ya 13 na Pointi 25 nyuma ya Chelsea.

Mabingwa Watetezi Leicester City, ambao hawana matumaini tena ya kutetea EPL-DES29Taji lao wakiselelea Nafasi ya 16 na Pointi 29 nyuma ya Vinara Chelsea, wapo kwao King Power Stadium kucheza na West Ham United ambao wako Nafasi ya 11.

Vigogo wa England Manchester United ambao wako Nafasi ya 6 watakuwa kwao Old Trafford kucheza na Middelsbrough ambao maarufu kama ‘Boro’.

Januari Mosi zipo Mechi 2 za kukamilisha Raundi ya 19 ambayo ni Nusu ya Mechi zote za EPL Watford kuikaribisha Tottenham na Arsenal kuwa kwao Emirates kucheza na Crystal Palace.

Ratiba:

**Saa za Bongo

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea