EPL: MTU 10 ‘WATAKATIFU’ WALIZWA NA SPURS!

SOUTHAMPTON-SPURSTOTTENHAM imewatandika Southampton Bao 4-1 katika Mechi pekee ya EPL, Ligi Kuu England, iliyochezwa Jana Usiku huko Uwanja wa Saint Mary huku Dele Alli akipiga Bao 2.

Ni Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, ndio waliotangulia kufunga katika Dakika ya Pili tu pale Virgil Van Dijk alipopiga Kichwa na kuunganisha Frikiki ya James Ward-Prowse.

Spurs wakasawazisha Dakika ya 19 kupitia Dele Alli alieunganisha Krosi ya Moussa Dembele.

Kipindi cha Pili, Dakika ya 52, Harry Kane akawapa Spurs Bao la Pili kwa Kichwa kufuatia Kona ya Christian Eriksen.EPL-DES29

Watakatifi wakabaki Mtu 10 Dakika ya 57 Nathan Redmond alipopewa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu Alli na Refa Mike Dean kutoa Penati ambayo Kane alipaisha.

Pengo hilo liliwapa mwanya Spurs kutawala na kuongeza Bao 2 kwenye Dakika za 85 na 87 Wafungaji akiwa Son Heung-Min na Alli na mwishowe kushinda 4-1.

Spurs wanabaki Nafasi ya 5 kwenye EPL lakini sasa pengo lao na Timu ya 4 Arsenal ni Pointi 1 tu na pia kuiacha Timu ya 6 Man United Pointi 3 nyuma.

Southampton wapo Nafasi ya 8 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Spurs.

VIKOSI:

SOUTHAMPTON: Forster, Cedric, Van Dijk, Fonte, Bertrand, Ward-Prowse, Davis, Romeu, Boufal, Redmond, Rodriguez

Akiba: Taylor, Yoshida, Long, Tadic, Martina, Reed, Hojbjerg.

TOTTENHAM: Lloris, Walker, Dier, Vertonghen, Rose, Wanyama, Dembele, Sissoko, Eriksen, Dele, Kane

Akiba: Vorm, Davies, Wimmer, Winks, Nkoudou, Son, Janssen

REFA: Mike Dean

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea