EPL: LEO ‘WATAKATIFU’ DHIDI YA SPURS!

SPURS-POCHETINOLEO Mechi pekee ya EPL, Ligi Kuu England, ni huko Uwanja wa Saint Mary kati ya Southampton, maarufu kama ‘Watakatifu’, na Tottenham Hotspur.

Mvuto wa Mechi hii ni ujio mwingine tena wa Meneja wa Spurs, Mauricio Pochettino, kwenye Klabu yake ya zamani aliyoihama Mei 2014 kwenda Spurs.

Wengine ambao watarejea kwenye Klabu yao ya zamani ni Wachezaji wa Spurs, Victor Wanyama kutoka Kenya ambae aliihama Southampton Mwezi Juni na Toby Alderweireld, aliesaini Spurs Julai 2015 baada ya kuwa kwa Mkopo Southampton kutoka Atlético Madrid.EPL-DES27

Kwenye EPL, Spurs wako Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 33 sawa na Timu ya 6 Man United huku juu yao wakiwa Arsenal wenye 37 wakati Southampton wapo Nafasi ya 8 wakiwa na Pointi 24.

Southampton watatinga kwenye Mechi hii wakiwa na hatihati kucheza kwa Mchezaji wao McCarthy ambae ana maumivu ya Musuli za Pajani lakini pia watawakosa Majeruhi Clasie, Targett, Austin na Pied.

Kwa upande wa Tottenham, hatihati ya kucheza ipo kwa Alderweireld, mwenye tatizo la Mgongo, na Janssen, mwenye maumivu ya Enka huku Lamela akiwa nje kutokana na kuumia Paja.

Uso kwa Uso

-Spurs hawajafungwa katika Mechi 4 zilizopita walizocheza Saint Mary Wakishinda 3 na Sare 1.

-Southampton wameifunga Tottenham Mechi 1 tu katika 8 zilizopita na hiyo ilikuwa Msimu uliopita, Mwezi Mei, waliposhinda 2-1 huko White Hart Lane.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:

SOUTHAMPTON: Forster, Soares, Yoshida, Van Dijk, Bertrand, Romeu, Ward-Prowse, Hojbjerg, Tadic, Boufal, Rodriguez

Akiba: McCarthy, Taylor, Martina, Gardos, Fonte, Long, Davis, Reed, Redmond, Stephens, Isgrove, Hesketh

TOTTENHAM: Lloris, Walker, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Wanyama, Dembele, Eriksen, Alli, Son, Kane

Akiba: López, Vorm, Trippier, Winks, Davies, Wimmer, Carter-Vickers, Dier, Janssen, Carroll, Onomah, Sissoko, Nkoudou

REFA: Mike Dean

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea