EPL – BOKSING DEI: CHELSEA YAPETA KILELENI, MAN UNITED SAFI TU, ARSENAL YAJIKONGOJA BAO LA MWISHONI!

>MKHITARYAN ‘HATARIII’ APIGA BAO HATARI!

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 26

Watford 1 Crystal Palace 1          

Arsenal 1 West Bromwich Albion 0        

Burnley 1 Middlesbrough 0         

Chelsea 3 Bournemouth 0           

Leicester City 0 Everton 2           

Manchester United 3 Sunderland 1                 

Swansea City 1 West Ham United 4                

2015 Hull City v Manchester City 

++++++++++++++++++++++++++

MANUNITED-MKHITARYAN-HATARI-SUNDERVINARA Chelsea wamepaa Pointi 9 juu kwenye EPL, Ligi Kuu England, baada kuichapa Bournemouth huku Arsenal wakishinda mwishoni na kushika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi sawa na Liverpool walio Nafasi ya Pili wakati Manchester United wakiiwasha Sunderland na kuifikia kwa Pointi Timu ya 5 Tottenham.

Huko Stamford Bridge, Chelsea wamejizatiti kileleni kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Bournemouth kwa Bao za Pedro, Bao 2, na Penati ya Eden Hazrad.

Ushindi huu wa Chelsea ni wa 12 mfululizo kwenye EPL kwa Klabu hiyo na kujiwekea Rekodi yao wenyewe.

Huko Old Trafford Manchester United wameitandika Sunderland 3-1 katika Mechi ya kwanza kwa David Moyes kwa mara ya kwanza tangu atimuliwe Umeneja na Man United Aprili 2014.EPL-DES26

Huo ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Man United katika EPL na Bao zao zilipachikwa na Daley Blind, Zlatan Ibrahimovic Na Bao tamu sana la alieanzia Benchi Henrikh Mkhitaryan.

Nako huko Emirates, Arsenal ilibidi wasubiri hadi Dakika ya 86 kwa Olivier Giroud kuwafungia Bao pekee na la ushindi walipoitungua West Bromwich Albion 1-0.

Mechi za EPL zitaendelea Jumanne kwa Mechi moja huko Anfield kwa Liverpool kuikaribisha Stoke City na Jumatano Mechi moja kati ya Southampton na Tottenham.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumanne Desemba 27

2015 Liverpool v Stoke City                  

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea