BOKSING DEI: CHELSEA BILA COSTA, KANTE KUWEKA REKODI? ARSENAL KUFUTA VIPIGO MFULULIZO? MOYES AREJEA OLD TRAFFORD, KUIZUIA MAN UNITED USHINDI 4 MFULULIZO?

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumatatu Desemba 26

1530 Watford v Crystal Palace              

1800 Arsenal v West Bromwich Albion            

1800 Burnley v Middlesbrough              

1800 Chelsea v Bournemouth               

1800 Leicester City v Everton               

1800 Manchester United v Sunderland            

1800 Swansea City v West Ham United           

2015 Hull City v Manchester City 

++++++++++++++++++++++++++

EPL-MANAGERSMECHI za EPL, Ligi Kuu England,Jumatatu Desemba 26, Boksing Dei, zina matumaini tofauti kwa Klabu tofauti.

Siku hiyo zipo Mechi 8 na Arsenal wanataka kufuta vipigo viwili mfululizo mikononi mwa Everton na Manchester City wakiikaribisha West Bromwich Albion Uwanjani Emirates.

Kwa Vinara Chelsea, chini ya Meneja Antonio Conte, na kwa Manchester City, chini ya Meneja Pep Guardiola, hii ni mara yao ya kwanza kwao kushuhudia Mechi za Ligi katika kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya.

Conte, Raia wa Italy, na Guardiola, Mtu wa Spain, huko makwao Ligi zao husimama na Ligi kwenda Vakesheni katika kipindi hiki cha hizo Sikuku lakini kwa England ni utamaduni Mechi kuendelea bila kusitishwa.EPL-DES25

Chelsea wanaongoza EPL wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Liverpool na wanasaka ushindi wao wa 12 mfululizo kwenye EPL na kuweka Rekodi mpya Klabu kwao wakicheza na Bournemouth.

Conte amesema hii ni mara yake ya kwanza kufanya kazi katika hiki cha Sikukuu na huu utakuwa ni uzoefu mzuri kwake.

Lakini Chelsea watatinga Mechi hii wakiwa na pengo kubwa kwa kumkosa Straika wao mkubwa, Diego Costa, na Kiungo mahiri, N'Golo Kante, wote wakiwa Kifungoni Mechi 1 kwa kulimbikiza Kadi za Njano 5.

Nae Pep Guardiola pia anawajibika kuwa kazini kipindi hiki cha Sikukuu kwa mara ya kwanza lakini amesema hawajali hilo na wanajitayarisha kuikabili Timu ya Mkiani Hull City kama zilivyo Mechi zingine tu.

Kwa Jose Mourinho, Meneja wa Manchester United, yeye amesema hana wasiwasi kucheza kipindi hiki na yupo tayari kuikabili Sunderland Uwanjani Old Trafford wakisaka ushindi wao wa 4 mfululizo kwenye EPL wakiwania kutumbukia safu ya 4 bora.

Kwa Sunderland, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Meneja wao David Moyes kurejea tena Old Trafford tangu afukuzwe kazi na Man United Aprili 2014.

EPL, LIGI KUU ENGLAND

Ratiba:

**Saa za Bongo

Jumanne Desemba 27

2015 Liverpool v Stoke City                  

Jumatano Desemba 28

2245 Southampton v Tottenham Hotspur                  

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton             

Jumamosi Desemba 31

1800 Burnley v Sunderland         

1800 Chelsea v Stoke City          

1800 Leicester City v West Ham United           

1800 Manchester United v Middlesbrough                 

1800 Southampton v West Bromwich Albion              

1800 Swansea City v Bournemouth                 

2030 Liverpool v Manchester City         

Jumapili Januari 1

1630 Watford v Tottenham Hotspur                

1900 Arsenal v Crystal Palace               

Jumatatu Januari 2

1530 Middlesbrough v Leicester City               

1800 Everton v Southampton               

1800 Manchester City v Burnley            

1800 Sunderland v Liverpool                

1800 West Bromwich Albion v Hull City           

2015 West Ham United v Manchester United             

Jumanne Januari 3

2245 Bournemouth v Arsenal                

2300 Crystal Palace v Swansea City                

2300 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4

2300 Tottenham Hotspur v Chelsea                 

         

 

 

Habari MotoMotoZ