VPL: AZAM YASHINDA, YAZIKIMBIZA YANGA, SIMBA!

VPL
Ligi Kuu Vodacom
Matokeo:
Jumapili Februari 19
Ndanda FC 0 African Lyon 0
Mtibwa Sugar 0 JKT Ruvu 0
Azam FC 2 Mwadui FC 0
========================
VPL-DTB-SITAZAM FC Jana Usiku wakiwa kwao huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam waliichapa Mwadui FC 2-0 na kujichimbia Nafasi ya 3 ya VPL, Ligi Kuu Vidacom.
Sasa Azam FC wamecheza Mechi 23 na wana Pointi 41 wakiwa nyuma ya Timu ya Pili Yanga waliocheza Mechi 21 na wana Pointi 50 huku Simba wakiwa kikeleni kwa kuwa na Pointi 51 kwa Mechi 22.
Katika Mechi ya Jana, Timu zote zilivaa Vitambaa Vyeusi mkononi na pia Vikosi vyote Viwili pamoja na Mashabiki wote Uwanjani walisimama kimya kwa Dakika 1 kwa heshima ili kuomboleza kifo cha Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Tukuyu Stars, Tanzania Prisons na Yanga, Geoffrey Boniface Mwandanji, aliyefariki dunia katikati ya Wiki hii. 
Azam FC walikuwa 1-0 mbele wakati wa Haftaimu kwa Bao la Dakika ya 24 la Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Bao la Pili la Azam FC ni la kujifunga mwenyewe Mchezaji wa Mwadui FC Iddi Moby katika Dakika ya 88.
VIKOSI:
AZAM FC: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Bruce Kangwa, Abbrey Morris, Yakubu Mohammed, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Samuel Afful, 62), Frank Domayo, Yahya Mohammed (Erato Nyon, 88), Ramadhani Singano ‘Messi’, Joseph Mahundi (Masoud Abdallah, 70).
MWADUI FC: Shaaban Kado, Nassor Masoud ‘Chollo’, David Luhende, Iddi Mobby, Malika Ndeule, Razack Khalfan, Abdallah Seseme, Awadh Juma, Paul Nonga (Salum Iyee, 18), Miraj Athuman na Hassan Kabunda
VPL
Msimamo
**Kwa hisani ya Soka APP
IMG-20170220-WA0000
Ratiba
Jumatatu Februari 20
Toto Africans v Kagera Sugar
Jumanne Februari 21
Mbao FC v Maji Maji FC
Jumamosi Februari 25
Simba v Yanga

TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI: YANGA YASONGA, SASA KUCHEZA NA ZANACO YA ZAMBIA KUSAKA MAKUNDI!

>>JUMAPILI ZIMAMOTO ZENJI KULINDA USHINDI MSUMBIJI?

CAF-CC-17Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, Leo wametoka Sare ya 1-1 na Mabingwa wa Visiwa vya Comoro, Ngaya Club kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kutinga Raundi ya Kwanza ya TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI kwa Jumla 6-2 kwani walishinda Mechi ya Kwanza Ugenini Bao 5-1.

Ngaya ndio walitangulia katika Dakika ya 19 kwa Bao la Yanga kujifunga wenyewe baada ya Shuti la Zahir Mohammed kumgonga Beki Vincent Boussou na kutinga.

Dakika ya 43 Yanga walikuwa 1-1 kufuatia Shuti la mbali la Mwinyi Haji kutinga wavuni.

Kwenye Raundi ya Kwanza Yanga watacheza na ZANACO ya Zambia ambayo Leo iliifunga APR ya Rwanda 1-0 huko Kigali na kusonga kwa Jumla ya Bao 1-0 kwani Wiki iliyopita zilitoka 0-0 huko Zambia.

Bao la ushindi la ZANACO lilifungwa Dakika ya 15 na Taonga Bwembya kwa Frikiki.

Mechi hizi za Raundi ya Kwanza ya Yanga na Zanaco zitachezwa katikati ya Machin a Mshindi kutinga Hatua ya Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI huku yule aliefungwa kupelekwa Hatua ya Mchujo ya Kombe la Shirikisho.

++++++++++++++++++++++

Fahamu:

Safari hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.

Mshindi wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.

Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

++++++++++++++++++++++

Jumapili Wawakilishi ya Zanzibar katika Mashindano haya watajitupa huko Nchini Msumbiji kurudiana na Ferroviario huku wakiwa mbele 2-1 baada ya kushinda Mechi yao ya kwanza Wiki iliyopita.

VIKOSI:

YANGA: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul [Hassan Kessy, 71’], Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Boussou, Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke [Said Juma 'Makapu', 72’], Obrey Chirwa, Emmanuel Martin [Mahadhi, 59’].

NGAYA: Said Mmadi, Said Hachim, Chadhuili Mradabi, Said Anfane, Franck Said Abderemane, Youssouf Ibrahim Moidjie, Rakotoarimanana Falinirino [Chabane Saandi Youddouf, 70’], Berthe Alpha, Zamir Mohammed [Kadafi Said Mze, 57’], Mounir Moussa, Said Toihir

REFA: Alex Muhabi [Uganda]

CAF CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Awali

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

*Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza/Zote Mbili ikiwa Mechi ya Pili imechezwa

Jumamosi Februari 18

Young Africans – Tanzania 1 Ngaya Club – Comoros 1 [6-2]  

Armee Patriotique Rwandaise FC – Rwanda 0 Zanaco – Zambia 1 [0-1]     

Atlabara FC - South Sudan 1 Coton Sport FC – Cameroon 4 [1-6]   

17:00 Township Rollers – Botswana Vs Cnaps Sports – Madagascar [1-2] 

18:00 AS-FAN – Niger Vs AS Tanda - Ivory Coast [0-3]        

19:00 Bidvest Wits - South Africa Vs SS Saint-Louisienne – Reunion [1-2] 

20:00 El Merreikh - Sudan Vs Sony de Ela Nguema - Equatorial Guinea [1-2]

22:30 Fath Union Sport de Rabat – Morocco Vs FC Johansens - Sierra Leone [1-1]

Jumapili Februari 19

14:15 AS Port Louis 2000 – Mauritius Vs Tusker – Kenya [1-1]        

16:00 Kedus Giorgis – Ethiopia Vs Côte d'Or – Seychelles [2-0]      

16:00 CAPS United FC – Zimbabwe Vs Lioli Football Club – Lesotho [0-0]  

16:00 Ferroviario Beira – Mozambique Vs Zimamoto Fc – Zanzibar [1-2]   

16:00 Vitalo FC – Burundi Vs CF Mounana – Gabon [0-2]     

16:30 Al-Ahli Tripoli - Libya         Vs All Stars FC – Ghana [3-1]     

17:30 Diables Noirs – Congo Vs Rail Club du Kadiogo - Burkina Faso [0-3]

17:30 UMS de Loum - Cameroon Vs AC Leopards de Dolisie – Congo [0-1]

17:30 AS Vita Club - Congo, DR Vs Royal Leopards – Swaziland 1-0]        

18:00 Enugu Rangers – Nigeria Vs JS Saoura – Algeria [1-1]

18:00 Rivers United – Nigeria Vs  AS Real de Bamako – Mali [0-0]  

18:30 Sewe Sport - Ivory Coast Vs Gambia Ports Authority – Gambia [0-1]

19:00 Primeiro de Agosto – Angola Vs Kampala City Council FC – Uganda [0-1]

20:00 Stade Malien de Bamako – Mali Vs Barrack Young Controllers FC – Liberia [0-1]  

20:00 Horoya Athlétique Club – Guinea Vs US Gorée – Senegal [0-0]

TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI: LEO YANGA KUIBANJUA TENA NGAYA?

>>JUMAPILI ZIMAMOTO ZENJI KULINDA USHINDI MSUMBIJI?

CAF-CC-17Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, wanarudiana na Mabingwa wa Visiwa vya Comoro, Ngaya Club ambayo Wiki iliyopita walitwanga 5-1 huko Comoro katika Mechi ya Raundi ya Awali ya TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI.

Katika Mechi hiyo ya kwanza Bao za Yanga zilipigwa na Justin Zullu, 43', Saimon Msuva, 45', Obrey Chirwa, 59', Tambwe, na Kamusoko, 73'.

Hii Leo Yanga wanahitaji Sare tu au hata wakifungwa Magoli hafifu ya tofauti ya 5-1 basi watasinga Raundi ya Kwanza ya Mashindano haya makubwa kwa Klabuni Barani Afrika.

Jumapili Wawakilishi ya Zanzibar katika Mashindano haya watajitupa huko Nchini Msumbiji kurudiana na Ferroviario huku wakiwa mbele 2-1 baada ya kushinda Mechi yao ya kwanza Wiki iliyopita.

++++++++++++++++++++++

Fahamu:

Safari hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.

Mshindi wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.

Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

++++++++++++++++++++++

Yanga Vs Ngaya:

VIINGILIO:

-Kiingilio cha chini katika mchezo wa leo ni Sh. 3,000, VIP A Sh 20,000, VIP B Sh 10,000 na VIP C Sh 10,000

MAREFA:

-Marefa watoka Uganda na ni Alex Muhabi Nsulumb, akisaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello, Refa wa Akiba ni Brian Nsubuga Miro na Kamishna ni kutoka Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

MSHINDI:

Mshindi wa Mechi hii atatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda ambazo Wiki iliyopita zilitoka 0-0 huko Zambia.

YANGA KIKOSI KITATOKANA NA: Deogratius Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Justin Zullu, Saimoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima, Ali Mustafa, Hassani Kessy, Oscar Joshua, Emanuel Martin, Juma Mahadhi, Juma Saidi, Deusi Kaseke

CAF CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Awali

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

*Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Jumamosi Februari 18

16:00 Young Africans – Tanzania Vs Ngaya Club – Comoros [5-1]   

16:30 Armee Patriotique Rwandaise FC – Rwanda Vs Zanaco – Zambia [0-0]      

16:30 Atlabara FC - South Sudan Vs Coton Sport FC – Cameroon [0-2]     

17:00 Township Rollers – Botswana Vs Cnaps Sports – Madagascar [1-2] 

18:00 AS-FAN – Niger Vs AS Tanda - Ivory Coast [0-3]        

19:00 Bidvest Wits - South Africa Vs SS Saint-Louisienne – Reunion [1-2] 

20:00 El Merreikh - Sudan Vs Sony de Ela Nguema - Equatorial Guinea [1-2]

22:30 Fath Union Sport de Rabat – Morocco Vs FC Johansens - Sierra Leone [1-1]

Jumapili Februari 19

14:15 AS Port Louis 2000 – Mauritius Vs Tusker – Kenya [1-1]        

16:00 Kedus Giorgis – Ethiopia Vs Côte d'Or – Seychelles [2-0]      

16:00 CAPS United FC – Zimbabwe Vs Lioli Football Club – Lesotho [0-0]  

16:00 Ferroviario Beira – Mozambique Vs Zimamoto Fc – Zanzibar [1-2]   

16:00 Vitalo FC – Burundi Vs CF Mounana – Gabon [0-2]     

16:30 Al-Ahli Tripoli - Libya         Vs All Stars FC – Ghana [3-1]     

17:30 Diables Noirs – Congo Vs Rail Club du Kadiogo - Burkina Faso [0-3]

17:30 UMS de Loum - Cameroon Vs AC Leopards de Dolisie – Congo [0-1]

17:30 AS Vita Club - Congo, DR Vs Royal Leopards – Swaziland 1-0]        

18:00 Enugu Rangers – Nigeria Vs JS Saoura – Algeria [1-1]

18:00 Rivers United – Nigeria Vs  AS Real de Bamako – Mali [0-0]  

18:30 Sewe Sport - Ivory Coast Vs Gambia Ports Authority – Gambia [0-1]

19:00 Primeiro de Agosto – Angola Vs Kampala City Council FC – Uganda [0-1]

20:00 Stade Malien de Bamako – Mali Vs Barrack Young Controllers FC – Liberia [0-1]  

20:00 Horoya Athlétique Club – Guinea Vs US Gorée – Senegal [0-0]

CAF CHAMPIONZ LIGI: YANGA v NGAYA, REFA MGANDA, LEO SIMBA-LYON ASFC CUP, LIGI KUU KINAMAMA FEB 26!

PRESS RELEASE NO. 255                                     FEBRUARY 15, 2017

WAGANDA KUAMUA MCHEZO WA YOUNG AFRICANS V WACOMORO

TFF-TOKA-SITMchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.

Nsulumbi atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.

NI SIMBA, AFRICAN LYON KESHO ASFC UWANJA WA TAIFA

Kesho Alhamisi Februari 16, 2017 timu za mpira wa miguu za Simba na African Lyon zitacheza mechi yao katika Raundi ya Sita ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup.

Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 lakini ulirudishwa nyuma kwa sababu za kiufundi kutoka timu zote mbili.

Michuano ya raundi hiyo ya sita, itaendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaochezwa saa 1.00 jioni.

Michezo ya siku hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.

Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

LIGI KUU YA WANAWAKE SASA KUANZA FEBRUARI 26

Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora ambayo ilikuwa ianze Febrauri 18, 2017 Uwanja wa Karume, imesogezwa mbele kwa muda wa juma moja.

Ligi hiyo sasa itaanza rasmi Februari 26, 2017 kwenye uwanja huohuo wa kumbukumbu ya Karume, Ilala mahali zilipo ofisi za TFF. Hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu.

Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.

Ratiba mpya inaonesha kwamba siku ya Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.

Ratiba kamili kwa mechi inazofuata itatolewa wiki ijayo. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza au unaoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

TOKA TFF: VPL MECHI 2, SERENGETI WAKO SOBER HOUSE, HONGERA LIPULI KUPANDA, 6 BORA KINAMAMA, SIMBA-LYON ALHAMISI, MAYANGA NA PROGRAMU!

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA

TFF-TOKA-SITLigi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo miwili tu.    

Michezo ya kesho kwa mujibu wa Ratiba ya VPL ni kati ya Ndanda FC itakayoikaribisha Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Kagera Sugar ya Kagera itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi nyingine zitachezwa Februari 17, 18 na 19 kwa mujibu wa Ratiba ambayo nimeambatanisha hapo chini.

SERENGETI BOYS KUTEMBELEA SOBER HOUSE

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Jumamosi tarehe 04 Machi, 2017, watatembelea Kituo cha vijana wanaopatiwa matibabu baada ya kuathirika na dawa za kulevya.

Kituo hicho kinachoitwa Sober House kipo Bagamoyo mkoani Pwani. Ni kituo maalumu kwa tiba ya vijana kinaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Life and Hope Rehabilitation Centre chini ya Mkurugenzi, Al-Karim Bhanji. 

Ikiwa huko, vijana wa Serengeti Boys ambao kwa sasa wako kwenye kipindi cha mabadiliko ya katika sayansi ya mwili hivyo itakuwa somo kubwa kwao katika kujielimisha kuhusu mustakabali wa maisha yao.

Kwa upande wa TFF kuwapeleka vijana hao huko ni utekelezaji Kanuni ya 36 (7) ya Ligi Kuu ya Vodacom inayozungumza kukataa rushwa, madawa, ubaguzi, fujo, kamari na mambo mengine ya hatari kwa mchezo wa mpira wa miguu.

PONGEZI LIPULI KUPANDA DARAJA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameuandikia barua uongozi wa Lipuli ya Iringa kwa mafanikio ya kupanda daraja msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/18.

Lipuli ya Iringa imepanda daraja baada ya kupita miaka 17 na Rais Malinzi amesema katika barua yake hiyo kwenda kwa Katibu Mkuu wa Lipuli, akisema: “Nitumie fursa hii kukupongeza wewe, uongozi wa klabu yako, benchi la ufundi na wadau wote wa timu ya Lipuli kufuatia kupanda daraja kwenda Ligi Kuu. 

“Bila shaka ni kazi kubwa imefanyika ikihusisha kujitolea kwa ari na mali kuhakikisha mnafika hapa mlipo,” ilisema barua hiyo na kuongeza: “Rai yangu kwenu ni kuongeza juhudi na kuendesha klabu kwa weledi mkubwa zaidi ili muweze kuwa washindani wa kweli katika ligi.”

Lipuli iliyokuwa kundi “A” imepanda daraja na kuzipiku timu za Kiluvya United ya Pwani, Pamba ya Mwanza, African Sports ya Tanga, Polisi Dar, Ashanti United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam.

SITA BORA LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA BARA 2016/2017

Baada ya timu sita (6) kutinga hatua ya Sita Bora ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirilkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufahamika, ratiba rasmi ya michuano hiyo, imetoka na inaonyesha kuwa hatua hiyo ya kutafuta bingwa wa msimu, itaanza Februari 18, mwaka huu.

Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa. 

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.

Ratiba inaonesha kwamba siku ya Februari 18, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.

Februari 20, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Panama saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Fair Play.

Februari 22, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisterz na Marsh Academy saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na JKT Queens.

Februari 24, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na JKT Queens saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Mlandizi Queens.

Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Sisters saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Marsh Academy.

Februari 28, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Sisters na Mlandizi Queens saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Fair Play.

Machi 2, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Acedemy na Fair Play saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Panama.

Machi 3, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu saa 10.00 jioni ambako JKT Queens watamaliza na Sisterz.
SIMBA, AFRICAN LYON RAUNDI YA 6 AZAM SPORTS FEDERATION KUCHEZA ALHAMISI FEBRUARI 16

Raundi ya Sita ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup – 2016/17, itaanza Februari 16, 2017 badala ya Februari 24, mwaka huu.

Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja kabla ya kuendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaopigwa saa 1.00 jioni. 

Michezo hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.

Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

MAYANGA AKABIDHI PROGRAMU TFF 

Kocha Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga amekabidhi programu ya miezi sita kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi akianzia mechi ya kirafiki za kimataifa kabla ya mechi za ushindani.

Mechi hizo ni kwa za wiki kwa mujibu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ambako kwa kuanzia tu, ataanza maandalizi ya mechi za wiki ya FIFA ambazo zitachezwa kati ya Machi 21 na 29, mwaka huu. 

TFF bado inaratibu michezo dhidi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro kwa maana ya wapinzani wao hapo baadaye.

Mwezi Aprili, kati ya tarehe 20 hadi 22, 2017 kutakuwa na mechi za kufuzu kwa michuano ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaokipiga Ligi ya Ndani (CHAN) ambako Taifa Stars itacheza na Rwanda katika hatua za awali. Fainali za CHAN zitafanyika Kenya mwakani.

Kwa mujibu wa ratiba, Juni 6 hadi 13, mwaka huu kutakuwa na mechi za kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Lesotho katika mchezo utakaofanyika hapa Tanzania.

Kwenye AFCON Tanzania iko kundi “L” ambalo wapinzani wake wako Lesotho watakaoanza kucheza nao hapa nyumani kabla ya huko mbele kucheza na Uganda na Carpe Verde. Fainali za AFCON zinatarajiwa kufanyika Cameroon, mwaka 2019.

IMETOLEWA NA TFF