VPL KUANZA LEO MABINGWA YANGA NA JKT RUVU, VINARA SIMBA JUMAPILI NANGWANDA NA NDANDA FC!

VPL-LOGO-MURUAMABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Yanga, Leo wanaanza Raundi ya Pili ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, kwa kucheza na JKT Ruvu Uwanja wa Uhuru Jiini Dar es Salaam.

Hii Leo Yanga watakuwa na Kocha Mkuu Mpya kutoka Zambia George Lwandamina aliemrithi Hans van de Pluijm ambae amekuwa Mkurugenzi wa Ufundi.VPL-DES17

Pia Yanga, ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba, hii Leo wataingia Uwanjani wakiwa na Wachezaji Wapya Wawili baada ya kumsaini Kiungo kutoka Zambia Justin Zulu na Straika kutoka JKU ya Zanzibar Emmanuel Martin Joseph.

Mbali ya Mechi hii ya Yanga hii Leo pia zipo mechi nyingine 3 wakati Jumapili zipo Mechi 4 za VPL ikiwemo ile ya Vinara Simba huko Nangwanda, Mtwara wakicheza na Nda Nda FC.

Nyingine Jumapili ni ile ya Timu ya 3 Azam FC ambao ni Wageni huko Uhuru Stadium Jijini Dar Es Salaam kuivaa African Lyon.

VPL

Msimamo – Timu za Juu:

1 Simba Mechi 15 Pointi 35

2 Yanga Mechi 15 Pointi 33

3 Azam Mechi 15 Pointi 25

4 Kagera Mechi 15 Pointi 24

5 Mtibwa Mechi 15 Pointi 23

VPL

Ligi Kuu Vodacom

Mechi za Mzunguko wa Pili

Ratiba

Jumamosi Desemba 17

JKT Ruvu v Yanga [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Mbeya City v Kagera Sugar [Sokoine, Mbeya]

Ruvu Shhoting v Mtibwa Sugar [Mabatini, Mlandizi]

Mwadui FC v Toto African [Mwadui Complex, Mwadui]

Jumapili Desemba 18

Mbao FC v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]

Ndanda FC v Simba [Nangwanda, Mtwara]

African Lyon v Azam FC [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Tanzania Prisons v Majimaji FC [Sokoine, Mbeya]

MZAMBIA LWANDAMINA AMEANZA YANGA: KIPINDI CHA KWANZA KIKOSI HIKI, CHA PILI KINGINE LAKINI YANGA YALALA!

YANGA-ZAMA-MPYABAO 2 za Emmanuel Martin za mapema Kipindi cha Kwanza zimewapa JKU ya Zanzibar ushindi wa 2-0 walipocheza na Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga Mechi ya Kirafiki Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwenye Mechi ya kwanza kabisa chini ya Kocha kutoka Zambia George Lwandamina.

Lwandamina, aliechukua wadhifa huo Wiki 2 zilizopita kutoka kwa Mholanzi Hans van der Pluijm ambae amekuwa Mkurugenzi wa Ufundi hapo hapo Yanga, Leo alikuwa akisimamia Mechi yake ya kwanza na hilo lilionekana kwenye upangaji wa Timu kwani alijaribu kumpa nafasi kila Mchezaji.

Mzambia huyo, Kipindi cha Pili, alibadili Wachezaji 10 kwa kuwaingiza Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Vincent Bossou, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Simon Msuva, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.

Licha ya kosa kosa kadhaa, Mabadiliko hayo hayakuwapa Yanga Boa lolote.

Jumamosi ijayo Yanga watakuwa hapo hapo Uhuru

YANGA – Kikosi chao: Ally Mustafa 'Barthez', Hassan Kessy, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Nadir Haroub 'Cannavaro', Said Juma, Juma Mahadhi, Matheo Antony, Obrey Chirwa, Malimi Busungu, Geoffrey Mwashuiya

Akiba: Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent 'Dante', Simon Msuva, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Justin Zulu, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Deus Kaseke, Kelvin Yondani.

VPL

Ligi Kuu Vodacom

Mechi za Mzunguko wa Pili

Ratiba

Jumamosi Desemba 17

JKT Ruvu v Yanga [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Mbeya City v Kagera Sugar [Sokoine, Mbeya]

Ruvu Shhoting v Mtibwa Sugar [Mabatini, Mlandizi]

Mwadui FC v Toto African [Mwadui Complex, Mwadui]

Jumapili Desemba 18

Mbao FC v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]

Ndanda FC v Simba [Nangwanda, Mtwara]

African Lyon v Azam FC [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Tanzania Prisons v Majimaji FC [Sokoine, Mbeya]

 

KESI YA KESSY - UAMUZI HADHARANI!

SUALA LA MCHEZAJI HASSAN RAMADHANI KESSY
TFF-HQ-1-1Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka.
1.Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.
2.Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na klabu ya Simba.
3.TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na sura ya sasa na pengine usingekuwepo.
4.Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa Young Africans.
5.Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba.
6.Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa ya lazima.
HATUA:
Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania. 
Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini).
Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Azam FC kujipima na Mtibwa Sugar J’mosi

By Abducado Emmanuel on December 08, 2016
1KATIKA kujiandaa vilivyo kuelekea mechi za raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kukipima kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Jumamosi ijayo Desemba 10 saa 1.00 usiku.
Azam FC iliyoanza maandalizi ya mzunguko huo wa pili Jumatatu iliyopita, itautumia mchezo huo kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza mikikimikiki ya ligi, ambapo inatarajia kufungua pazia kwa kucheza na African Lyon Desemba 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Baadhi ya wachezaji wapya itakaowatumia katika mchezo huo ni washambuliaji Yahaya Mohammed (Aduana Stars) na Samuel Afful (Sekondi Hasaacas), ambao wametua nchini alfajiri ya leo Jumatano wakitokea nchini kwao Ghana sambamba na beki wa kati, Yakubu Mohammed (Aduana Stars) aliyekuja kufanya majaribio ya kujiunga na Azam FC.
Mabingwa hao wanawafanyia majaribio wachezaji wengine wawili kutoka Cameroon, beki wa kati Batetakang Flavius (Canon Yaoundé) na kiungo mkabaji Stephane Kingue (Coton Sport FC de Garoua), ambao nao wanatarajia kuwemo kwenye mtanange huo.
Hadi inamaliza raundi ya kwanza ya ligi, Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola kinachochangamsha mwili na kuburudisha koo pamoja na Benki bora kabisa nchini kwa sasa ya NMB, imejikusanyia jumla ya pointi 25 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa nyuma pointi 10 dhidi ya Simba (35).
Mbali na kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi, Azam FC pia inayatumia mazoezi hayo kujiandaa ipasavyo na michuano mingine ya Kombe la Mapinduzi, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Kombe la Shiikisho Afrika (CC), ili iweze kufanya vizuri.
IMETOLEWA NA AZAM FC

Bocco: Tutakaa nafasi nzuri raundi ya pili

IMG 0166IKIWA ni siku ya pili tu tokea Azam FC ianze mazoezi, nahodha wa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, John Bocco ‘Adebayor’, anaamini ya kuwa kikosi hicho kitakuwa vizuri na kukaa nafasi nzuri kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Azam FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola kinachosisimua koo na kuchangamsha mwili, pamoja na Benki bora kabisa nchini kwa usalama wa fedha zako ya NMB, tayari kimeanza mazoezi tokea jana asubuhi ili kujiweka fiti zaidi kwa ajili ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi.
Bocco ameunambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya leo ya asubuhi kuwa morali waliyokuwa nayo wachezaji pamoja na nguvu za nyota wapya walioongezwa kikosini kwenye usajili huu wa dirisha dogo, utaweza kuwasaidia kufanya vizuri.
“Tunamshukuru Mungu tumeweza kufika na kufanya mazoezi salama kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili, mazoezi tumeanza vizuri, wachezaji wote wanamorali, wamerudi wameonekana hawakwenda nyumbani tu kupumzika bali walikuwa wakifanya baadhi ya mazoezi, kwa hiyo naamini raundi ya pili itakuwa ni nzuri sana kwetu,” alisema.
Nahodha huyo aliongeza kuwa: “Ukizingatia hata katika usajili kuna nguvu tumeweza kuiongeza, kwa hiyo ninaimani wachezaji tutaweza kujituma na Mungu atatusaidia tutaweza kufanya vizuri raundi ya pili.”
Benchi la Ufundi la Azam FC kwa kushirikiana na uongozi wa timu hiyo, katika usajili huu wa dirisha dogo unaoendelea uwemeza kuongeza nguvu mpya kwa kuwasajili washambuliaji nyota wawili kutoka Ghana, Yahaya Mohamed anayetokea Aduana Stars na staa wa Sekondi Hasaacas, Samuel Afful.
Pia imeweza kuwarudisha kundini wachezaji wake wawili waliokuwa kwa mkopo, beki wa kati kinda Abdallah Kheri aliyekuwa Ndanda na winga wa kushoto Enock Atta Agyei (Medeama).
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii, wanaojiandaa pia na michuano ya Mapinduzi Cup, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Kombe la Shirikisho Afrika (CC), hadi inamaliza mzunguko wa kwanza wa ligi imefanikiwa kujikusanyia jumla ya pointi 25 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikizidiwa pointi 10 na kinara Simba aliyejikusanyia 35 na Yanga ikiwa nazo 33.
IMETOLEWA NA AZAM FC (By Abducado Emmanuel on December 06, 2016)