VPL: MABINGWA YANGA WAREJEA PENYEWE, WASHIKA HATAMU!

VPL-DTB-SITMABINGWA WATETEZI wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga Leo wameinyuka Mwadui FC 2-0 kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kushika uongozi wa Ligi hiyo.

Bao zote za Yanga zilifungwa Kipindi cha Pili na Mzambia Obrey Chirwa alieingizwa Kipindi hicho kutoka Benchi kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima.

Bao la Kwanza kwa Yanga lilifungwa Dakika ya 69 baada ya Kipa wa Mwadui FC Shaaban Kado kutema Shuti la Simon Msuva na VPL-JAN29Chirwa kuutokea Mpira na kuukwamisha wavuni.

Chirwa tena akapiga Bao la Pili Dakika ya 83 baada ya kumalizia Krosi ya Mwinyi Haji iliyoparazwa kwa Kichwa na Thabani Kamusoko.

Ushindi huu umewaweka Mabingwa Yanga kileleni mwa VPL baada ya kuing’oa Simba walioshikilia kilele tangu Agosti.

Yanga sasa wana Pointi 46 na Simba 45 huku zote zikiwa zimecheza Mechi 20 kila moja.

VIKOSI:

YANGA: Deo Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe [Said Juma ‘Makapu’, 81’], Haruna Niyonzima [Obrey Chirwa, 68;’], Deus Kaseke [Emmanuel Martin, 52’]

MWADUI FC: Shaaban Kado, Nassor Masoud 'Chollo', Malika Ndeule, Yassin Mustafa [David Luhende, 81’], Iddi Mobby, Razack Khalfan, Hassan Kabunda [Salum Kanoni, 89’], Awadh Juma, Paul Nonga, Salim Khamis [Joseph Kimwaga, 86’], Abdallah Seseme

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba/Matokdeo:

Jumapili Januari 29

Yanga 2 Mwadui FC 0

Jumatatu Januari 30

Kagera Sugar v Mtibwa Sugar

JKT Ruvu v Stand United

VPL: KEPTENI BOCCO AIPIGA SIMBA ‘BOKO’ 1, DABI SOKOINE PRISONS YAILAZA MBEYA!

>JUMAPILI MABINGWA YANGA KUWALAZA MWADUI NA KUSHIKA HATAMU?

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba/Matokdeo:

Jumamosi Januari 28

Simba 0 Azam FC 1

Tanzania Prisons 2 Mbeya City 0

Ndanda FC v Majimaji FC

Toto Africans v African Lyon

+++++++++++++++++++++++++

VPL-DTB-SITSimba, ambao ni Vinara wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo Jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa wamefungwa 1-0 na Azam FC na huko Sokoine, Mbeya kwenye Dabi ya Mji huo, Tanzania Prisons imeifunga Mbeya City 2-0.

Kwa Simba, hiki ni kipigo cha pili mfululizo toka kwa Azam FC ambao Januari 13 waliichapa Simba 1-0 na kubeba Kombe la Mapinduzi huko Amaan Stadium Zanzibar.

Kwenye Mechi hiyo, Mfungaji alikuwa Himid Mao lakini Leo ni Kepteni wao John Bocco ndie alifunga Bao 1 na la ushindi katika Dakika ya 70.

Matokeo haya yameibakisha Simba kileleni mwa VPL wakiwa na Pointi 45 kwa Mechi 20 na kufuata Yanga wenye Pointi 43 kwa Mechi 19 wakati Azam FC ni wa 3 wakiwa na Pointi 34 kwa Mechi 20.

Yanga Kesho wapo dimbani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Mwadui FC na ushindi kwao utawaweka kileleni.

Nako huko Sokoine, Mbeya kwenye Dabi kati ya Tanzania Prisons imewachapa Mbeya City Bao 2-0 kwa Bao za Samatta na Asukile.

VIKOSI:

SIMBA: Daniel Agyei, Janvier Bokungu [Ibrahim Hajib, 59’], Mohammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Said Ndemla, Jamal Mnyate [Shiza Kichuya, 47’], Muzamil Yassin, Pastory Athanas, Juma Luizio [Laudit Mavugo, 65’]

AZAM FC: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue [Mudathir Yahya, 77’], Himid Mao, Joseph Mahundi, Frank Domayo, John Bocco [Abdallah Kheri, 83’], Ramadhani Singano [Yahya Mohammed, 63’]

REFA: Erick Onoka

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba/Matokdeo:

Ijumaa Januari 27

Mbao FC 2 Ruvu Shoooting 0

Jumapili Januari 29

Yanga v Mwadui FC

Jumatatu Januari 30

Kagera Sugar v Mtibwa Sugar

JKT Ruvu v Stand United

TFF YAMSHUKURU RAIS DOKTA MAGUFULI, WAZIRI NAPE KWA KURIDHIA TAIFA KUTUMIKA TENA KISOKA!

PRESS RELEASE NO. 243                                             JANUARI 27, 2017

TFF YAMSHUKURU RAIS DK. MAGUFULI

TFF-HQ-1-1Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kufunguliwa tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kadhalika, TFF inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa juhudi zake na kwamba namna aliyoonesha ushirikiano kufanikisha suala la kufunguliwa uwanja huo uliofungiwa matumizi yake na Serikali, Oktoba mwaka uliopita.

TFF inachukua nafasi hii kuahidi kuwa itasimamia matumizi mazuri ya uwanja huo kwa kutoa elimu kwa wadau ili kuutumia uwanja huo vema ikitambua kuwa ni hazina ambayo imetokana na nguvu na gharama kubwa za Serikali kuujenga uwanja huo.

TFF inatahadharisha mashabiki wa mpira wa miguu kwamba uwanja huo umejengwa kwa gharama kubwa hivyo ni jukumu letu kuutuza na kuutumia vema kwa sababu ni hazina kubwa tuliyonayo na ni miongoni mwa urithi bora kwa vizazi vijavyo.

Kwa sasa tumetuma maombi yetu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba kuutumia uwanja huo kwenye mchezo wa kesho Jumamosi Januari 28, mwaka huu kati Simba na Azam utapigwa kwenye uwanja huo wa Taifa, Dar es Salaam kadhalika keshokutwa katika mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Mwadui ya Shinyanga.

Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaonesha kuwa ligi hiyo huko Mbeya kutakuwa na ‘derby’ kwa maana ya mchezo wa upinzani baina ya timu zinazotoka mkoa mmoja wa Mbeya ambazo ni Tanzania Prisons na Mbeya City utakaochezwa na Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Keshokutwa Jumapili Januari 29, mwaka huu kutakuwa na mchezo mwingine ambao Young Africans itacheza na Mwadui jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Majimaji ya Songea itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Jumatatu Januari 30, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

TFF YAITUPA RUFAA DHIDI YA SIMBA!

PRESS RELEASE NO. 242
RUFAA YA POLISI DAR ES SALAAM
TFF-HQ-1-1-1-1Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea rufaa kutoka Klabu ya Polisi Dar es Salaam dhidi ya Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji Novalty Lufunga katika mchezo wao wa Raundi ya Tano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2017.
Madai ya Polisi ni kwamba Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo kati ya Simba na Coastal Union katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 uliofanyika Uwanja wa Taifa, Aprili 11, mwaka jana.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetupilia mbali rufaa hiyo kwa kukosa vigezo vya kikanuni katika uwasilishaji wake na hivyo kukosa sifa ya kusikilizwa. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 18 (1) na (2) ya Kanuni za Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD.
Kanuni ya 18 (1) inasema: “Malalamiko yoyote kuhusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi kwa kamishna wa mchezo au TFF sio zaidi ya masaa sabini na mbili (72hrs) baada ya kumalizika mchezo.”
Kanuni ya 18 (2) inasema: Ada ya malalamiko ni shilingi laki tatu (Tshs 300,000.00). Malalamiko yo yote yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada na kuwasilishwa nje ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.”
Hata hivyo, Shirikisho linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Mchezaji Novalty Lufunga katika mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2016/2017.
Kwa utaratibu wa mashindano haya ambayo ni ya mtoano, adhabu za kadi (njano na nyekundu) zitolewazo uwanjani, zinakoma mwisho wa msimu wa shindano husika isipokuwa kadi hizo zikiongezwa adhabu ya kinidhamu (suspension) ambayo itafahamisha kwa klabu na mchezaji kwa maandishi.
Kadhalika, Kanuni ya 16 ya Kanuni za Kombe la Shirikisho Sehemu ya Tatu inaeleza wazi kuwa matumizi ya kanuni za ligi zitahusika maeneo yanayoruhusu uendeshaji wa shindano la mtoano.
“Adhabu zote zinazohusisha katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam HD zitahusisha na shindano hili tu,” inasema kanuni ya 16 (3) na (4).
KAMBI YA KILIMANJARO WARRIORS
Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ inatarajiwa kuingia kambini Janauri 29, 2017 kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali za Olimipiki zitakazofanyika jijini Tokyo, Japan mwaka 2020.
Kambi hiyo ya wiki moja itafanyika kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.
Tanzania haijapata kushiriki Michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu jambo ambalo limeisukuma TFF kuona kuwa ni fursa ya mpira wa miguu kuchezwa hivyo inashirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kufanikisha mipango na taratibu.
Tanzania kwa sasa ina vijana wengi waliotokana na michuano ya Mradi wa kuibua na kukuza vipaji wa Airtel kadhalika na Cocacola ambao wamekuwa chachu ya maendeleo ya timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
Vijana hawa wa Airtel, Copa Cocacola na Serengeti Boys wataungana na baadhi ya vijana waliofanya vizuri kwenye Ligi ya Vijana wenye umri wa chini miaka 20 kutoka timu za Ligi Kuu ambao wamezaliwa baada ya tarehe 1 Januari 1997 ili kuunda kikosi imara cha awali kuelekea kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo Japan, mwaka 2020.
Kwa kufuata utaratibu wa maandalizi ya Serengeti Boys na kwa kushirikiana na TOC timu hii itapewa mazoezi na michezo  ya kujipima nguvu ndani na nje ya nchi.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

VPL: DIMBANI IJUMAA, JUMAMOSI BIGI MECHI SIMBA-AZAM, DABI SOKOINE PRISONS-MBEYA, JUMAPILI MABINGWA YANGA NA MWADUI!

VPL-DTB-SITVPL, Ligi Kuu Vodacom, ipo kilingeni kuanzia Ijumaa kwa Mechi 1 na Jumamosi ni lukuki yake lakini Siku hiyo ‘Macho Kodo’ yapo Jijini Dar es Salaam kwa Bigi Mechi kati ya Simba na Azam FC na huko Sokoine, Mbeya kwenye Dabi kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Ijumaa ipo Mechi moja huko CCM Kirumba Mwanza kati Ya Mbao FC na Ruvu Shooting Timu ambazo zimepishana Pointi 4 wakati Ruvu Shooting ikiwa Nafasi ya 8 na ina Pointi 24 na Mbao FC wapo wa 12 wakiwa na Pointi 20.

Jumamosi zipo Mechi 4 na mbili kati ya hizo zina majina moja ikiwa ni BIGI MECHI na nyingine ni DABI.

BIGI MECHI ipo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kati ya Simba na Azam FC na DABI ni huko Sokoine Jijini Mbeya kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Simba ndio Vinara wa VPL wakiwa mbele ya Azam FC, walio Nafasi ya 4, kwa Pointi 12.VPL-JAN25

Mbeya City, ambao wako Nafasi ya 6, wamecheza Mechi 2 zaidi ya Tanzania Prisons ambao wako Nafasi ya 9 wakiwa Pointi 4 nyuma yao.

Jumapili, Mechi pekee ni Jijini Dar es Salaam ambayo huenda ikapigwa Uwanja wa Taifa kama si Uhuru, ambapo Mabingwa Watetezi Yanga watakapokumbana na Mwadui FC.

Yanga wao wapo Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba na Mwadui FC wako Nafasi ya 10 wakiwa Pointi 21 nyuma ya Yanga.

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba

Ijumaa Januari 27

Mbao FC v Ruvu Shoooting

Jumamosi Januari 28

Toto Africans v African Lyon

Simba v Azam FC

Tanzania Prisons v Mbeya City

Ndanda FC v Majimaji FC

Jumapili Januari 29

Yanga v Mwadui FC

Jumatatu Januari 30

Kagera Sugar v Mtibwa Sugar

JKY Ruvu v Stand United