KEPTENI SAMATTA APIGA 2, STARS 2 BOTSWANA O!

STARS-SAMATTA-BOTSWANAKEPTENI wa Taifa Stars, Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Mbwana Samatta, Leo amefunga Bao zote 2 wakati wakiwachakaza Botswana 2-0 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambayo miongoni mwa Wahudhuriaji wake ni Waziri mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dokta Harison Mwakyembe.

Hii ilikuwa ni Mechi ya Kwanza kwa Kocha Mpya wa Stars, Salum Mayanga, na Kepteni Samatta hakupoteza muda alipoipa Stars Bao la Kwanza Dakika ya 3 tu.

Bao la Pili la Stars lilifungwa Dakika ya 87 kwa Frikiki murua ya Samatta.

Botswana, chini ya Kocha Peter Buffler, ilionyesha Soka la kuridhisha lakini ukali wa Mchezaji wa Kulipwa Samatta, anaechezea KRC Genk huko Belgium, ndio uliwaua.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine dhidi ya Burundi Jumanne ijayo, Machi 28.

VIKOSI:

TANZANIA: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Abdi Banda, Himid Mao [Jonas Mkude], Simon Msuva [Said Ndemla], Frank Domayo [Muzamil Yassin], Mbwana Samatta, Ibrahim Ajib, Shiza Kichuya [Farid Mussa]

BOTSWANA: Kabelo Dambe, Tapiwa Gadibolae, Kaone Vanderwesthuizem, Lesenya Ramoraka, Lesego Galenamotlhale, Ofentse Nato, Lebogang Ditsele, Omaaatla Kebatho, Mosha Gaolaolwe, Thacng Sesenyi, Mogakolod Ngele

TOKA TFF: REFA ADONGO ‘APIGWA DONGO’ MECHI SIMBA-MBEYA CITY!

>TFF YASHUSHA VIINGILIO STARS v BOTSWANA TAIFA JUMAMOSI!

SERENGETI BOYS WACHANJWA

STARS-BOTSWANATimu ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys leo Machi 24, wamefanyiwa chanjo ya ugonjwa wa manjano (yellow fever) kabla ya kuanza safari ya kwenda Morocco, Cameroon na Gabon.

Timu hiyo imefuzu kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali hizo zinatarajiwa kuanza Mei 14 mwaka huu na mapema mwezi ujao itasafiri kwenda Morocco kwa ajili ya kambi.

Kambi hiyo itakuwa ni ya mwezi mmoja (Aprili 5 hadi Mei 1, 2017) kabla ya kuwa na kambi ya wiki moja huko Cameroon (Mei mosi hadi Mei 7, mwaka huu) na baadaye itafanya kambi nyingine Gabon (Mei 7 mpaka Mei 13) angalau kwa wiki moja kabla ya kuanza fainali hizo Mei 14, mwaka huu.

TFF YAPUNGUZA KIINGILIO MECHI TAIFA STARS

Taifa Stars - timu ya Tanzania ya mpira wa miguu kwa mwaka 2017 inaingia uwanjani kucheza na Botswana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ya kirafiki ya kimataifa katika wiki ya kalenda ya FIFA.

Kwa umuhimu wa mchezo huo na hamasa ambayo uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania umeona hivyo TFF imeatangaza kushusha bei ya kiingilio kwa watu watakaokaa mzunguko kutoka Sh 5,000 hadi Sh. 3,000.

“Wavutieni Watanzania wakaishangilie timu yao, wekeni viingilio vya bei ya chini ambayo Mtanzania itamweka katika mazingira ya kuchangia gharama kidogo kwa timu. Toeni hiyo Sh 5,000 yenu. Wekeni angalau Sh. 3,000,” ameagiza Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Pamoja na punguzo hilo kwa mashabiki wa mpira wa miguu watakaoketi Majukwaa Maalumu - VIP “A” watalipia Sh 15,000 na wale watakaoketi VIP “B” na “C” watalipia Sh 10,000.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salum Mayanga kwa upande wake aliwathibitishia Waandishi wa Habari kwamba kikosi chake kiko imara kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika kuanzia saa 10.00 jioni.

“Tuna morali wa hali ya juu,” alisema Mayanga ambaye aliteuliwa kuinoa timu hiyo mapema mwaka huu.

Kwa upande wa Peter Buffler – Kocha Mkuu wa Botswana, alisema kwamba anatarajiwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa sababu amegundua kuwa kikosi cha Taifa Stars kina vijana wengi ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Mbali ya mchezo huo wa kesho, Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine dhidi ya Burundi Jumanne ijayo, Machi 28, mwaka huu. Mchezo ambao pia ni wa kirafiki wa kimataifa unatarajiwa kuanza saa 10.00 jioni.

MWAMUZI ADONGO AONYWA

Mwamuzi Jacob Adongo amepewa ONYO KALI kwa kushindwa kutafsiri vizuri sheria katika mechi namba 186 kati ya Simba na Mbeya City iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Onyo hilo limetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Kadhalika katika mchezo huo namba 186 (Simba 2 vs Mbeya City 2). Klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa timu yake kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu.

Adhabu dhidi ya Mbeya City imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

Mechi namba 190 (Kagera Sugar 1 vs Majimaji 0). Klabu ya Majimaji imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kosa la kutokuwa na Daktari kwenye Kikao cha Maandalizi ya Mechi (Pre Match Meeting) na hata uwanjani wakati wa mchezo. Kitendo hicho ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Kuu, na adhabu ni uzingativu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.

Pia kwa kutumia Kanuni ya 9(8) ya Ligi Kuu imefuta kadi ya njano aliyooneshwa mshambuliaji Jaffari Salum wa Mtibwa Sugar katika mechi hiyo namba 175 kati ya African Lyon na Mtibwa Sugar iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kubaini haikuwa sahihi.

Klabu ya Yanga iandikiwe barua ya Onyo Kali kutokana na benchi lake la ufundi kumlalamikia mara kwa mara Mwamuzi wakati wa mechi ya utangulizi ya U20 kati ya timu hiyo na Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   Kuhusu mechi za Ligi Daraja la Pili (SDL Play Off)

Mechi namba 3 (Oljoro 1 vs Transit Camp 1). Klabu ya Oljoro imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu hiyo kumrushia mawe Mwamuzi akiwa uwanjani.

……………………………………………………………………………… …………..

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

TOTAL CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: YANGA YAPANGWA NA TIMU YA ALGERIA!

CAF-TOTAL-CC-17MABINGWA WA TANZANIA BARA, Yanga, ambao Juzi walitupwa nje ya TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI na kuangukia TOTAL CAF Kombe la Shirikisho, Leo wamepangwa kucheza Raundi ya Mchujo na Klabu ya Algeria MC Alger.

Mc Alger, kirefu ni Mouloudia Club d'Alger, ni Klabu ambayo Makao Makuu yake ni Mji Mkuu wa Algeria, Algiers.

Washindi 16 wa Raundi hiyo watacheza Hatua ya Makundi.

Droo ya Raundi ya Mchujo ya TOTAL CAF Kombe la Shirikisho imefanyika muda mchache uliopita huko Makao Makuu ya CAF Jijini Cairo Nchini Egypt.

Droo hii imekutanisha Timu 16 zilizoshinda Raundi ya Kwanza ya Mashindano haya na kupambanishwa na Timu 16 zilizotupwa nje ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI na mojawapo ni hii Yanga yetu.

DROO KAMILI:

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO

Raundi ya Mchujo

Young Africans v MC Alger

TP Mazembe v JS Kabylie

AC Léopards v Mbabane Swallows

FUS Rabat v MAS Fez

Enugu Rangers v ZESCO United

CF Mounana v ASEC Mimosas

Rail Club du Kadiogo v CS Sfaxien

Bidvest Wits v Smouha

CNaPS Sport v Recreativo do Libolo

KCCA v Al-Masry

Gambia Ports Authority v Al-Hilal Al-Ubayyid

AS Port-Louis 2000 v Club Africain

Rivers United v Rayon Sports

Barrack Young Controllers v SuperSport United

AS Tanda v Platinum Stars

Horoya v IR Tanger

**Mechi kuchezwa Aprili 7-9 na Marudiano ni Aprili 14-16.

-Washindi 16 kusonga Hatua ya Makundi

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: TAMBUA WAPINZANI WANAOWEZA KUIVAA YANGA RAUNDI YA MCHUJO!

CAF-TOTAL-CC-17MABINGWA WA TANZANIA BARA, Yanga, Juzi walitupwa nje ya CAF CHAMPIONZ LIGI na kuangukia CAF Kombe la Shirikisho ambako watacheza Raundi ya Mchujo itakayotoa Timu 16 za kucheza Hatua ya Makundi.
Raundi ya Mchujo ya CAF Kombe la Shirikisho inakutanisha Timu 16 zilizoshinda Raundi ya Kwanza ya Mashindano hayo na kupambanishwa na Timu 16 zilizotupwa nje ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI na mojawapo ni hii Yanga yetu.
Droo ya kupanga Mechi hizi za Raundi ya Mchujo itatangazwa na CAF hivi karibuni.
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
Washiriki Raundi ya Mchujo
**Timu kutoka Kombe la Shirikisho itakutanishwa na Timu kutoka CAF CHAMPIONZ LIGITimu 16 zilizoshinda Raundi ya Kwanza ya CAF Kombe la Shirikisho:
 JS Kabylie
 MC Alger
 Recreativo do Libolo
 Al-Masry
 Smouha
 IR Tanger
 MAS Fez
 Rayon Sports
 Platinum Stars
 Club Africain
 CS Sfaxien
 ZESCO United
Timu 16 zilitolewa Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI:
 Rail Club du Kadiogo
 CF Mounana
 CNaPS Sport
 FUS Rabat
 Rivers United
 Young Africans
 KCCA
**Mechi kuchezwa Aprili 7-9 na Marudiano ni Aprili 14-16. 
-Washindi 16 kusonga Hatua ya Makundi.
 

ULIMWENGU KUIKOSA STARS, AZAM FC YABAMIZWA 3, NJE AFRIKA!

TOKA TFF:

ULIMWENGU AZIKOSA BOTSWANA, BURUNDI

TFF-TOKA-SIT-1Wakati timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kikitarajiwa kuingia kambini leo Machi 19, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam, kikosi hicho cha Kocha Salum Mayanga, kitamkosa Thomas Ulimwengu kutoka AFC Eskilstuna ya Sweden.

Taarifa ambazo Mayanga amezipata kutoka Sweden ni kwamba Ulimwengu kwa sasa yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo ya AFC Eskilstuna. Hivyo sasa Mayanga atabaki na washambuliaji Mbwana Samatta  (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).

Mbali ya hao, nyota wengine aliowataja Jumatatu iliyopita ni  walinda milango, Aishi Manula  (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe    (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).

Mayanga aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni   (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao     (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).

Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla  (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya    (Simba SC).

Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati wasaidizi wake ni Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata; Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timuatakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo   akiwa ni Gilbert Kigadya.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

IMETOLEWA NA TFF

AZAM FC YATUPWA NJE AFRIKA BAADA KUBAMIZWA 3

LEO huko Mbabane, Swaziland, Azam FC imechapwa Bao 3-0 na Mbabane Swallows ikiwa ni Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya CAF Kombe la Shirikisho na kutupwa nje ya Mashindano hayo kwa Jumla ya Bao 3-1.

Azam FC walishinda 1-0 kwenye Mechi ya Kwanza katika Uwanja wao huko Chamazi.

Mbabane Swallows sasa wanatinga Raundi ya Mchujo ya Mashindano hayo na watacheza na moja kati ya Timu 16 ambazo zimetupwa nje ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya CAF CHAMPIONZ LIGI.