TFF UCHAGUZI: 74 WAREJESHA FOMU, 10 KUGOMBEA URAIS!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                           JUNI 20, 2017

74 WACHUKUA FOMU, KUREJESHA TFF

Wanafamilia 74 wa mpira wa miguu, wamechukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

TFF TOKA SITHadi zoezi hilo linafungwa leo Juni 20, 2017 saa 10.00 jioni wagombea wote wamerejesha ambako kwenye nafasi ya urais, jumla ya wagombea 10 walijitokeza kuomba nafasi hiyo wakati kwenye makamu rais wamejitokeza sita.

Wadau 58 wamejitokeza kuwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji katika Katika Kanda mbalimbali. Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa mujibu wa Kanuni ya 10, limefanyika kwa siku tano kuanzia Juni 16, 2017 hadi Juni 20, mwaka huu.

Siku ya kwanza ilipoanza tu, Jamal Malinzi alikuwa wa kwanza kuchukua fomu na kurejesha huku akifuatiwa na Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.

Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

Soloum Chama

Kaliro Samson

Leopold Mukebezi

Abdallah Mussa

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

Vedastus Lufano

Ephraim Majinge

Samwel Daniel

Aaron Nyanda

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

Benista Rugora

Mbasha Matutu

Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

Omari Walii

Sarah Chao

Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

John Kadutu

Issa Bukuku

Abubakar Zebo

Francis Michael

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

Kenneth Pesambili

Baraka Mazengo

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;

Elias Mwanjala

Cyprian Kuyava

Erick Ambakisye

Abousuphyan Silliah

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

James Mhagama

Golden Sanga

Vicent Majili

Yono Kevela

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

Athuman Kambi

Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;

Hussein Mwamba

Mohamed Aden

Musa Sima

Stewart Masima

Ally Suru

George Benedict

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

Charles Mwakambaya

Gabriel Makwawe

Francis Ndulane

Hassan Othman ‘Hassanol’

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

Khalid Mohamed

Goodluck Moshi

Thabit Kandoro

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

Emmanuel Ashery

Ayoub Nyenzi

Saleh Alawi

Shaffih Dauda

Abdul Sauko

Peter Mhinzi

Ally Kamtande

Said Tully

Mussa Kisoky

Lameck Nyambaya

Ramadhani Nassib

Aziz Khalfan

Jamhuri Kihwelo

Saad Kawemba

Bakari Malima

Kwa siku tatu, kuanzia kesho Juni 21 hadi 23, mwaka huu kwa mujibu wa kanuni ya 11.1 ya Uchaguzi wa TFF, Kamati ya Uchaguzi itaanza mchujo wa awali kwa wote waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali kama inavyojionesha hapo juu.

………………………………………………………………………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

BMT YABARIKI UCHAGUZI TFF, LATOA MAAGIZO

TFF TOKA SITBaraza la Michezo Tanzania (BMT), limebariki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likisema: “Tunaitakia TFF uchaguzi mwema wenye amani, upendo na utulivu.”

Pamoja na baraka hizo, Baraza limeiagiza TFF kuwaelekeza wagombea wote kuzipitia sheria za Baraza la Michezo, Kanuni za Baraza na kanuni za Usajili, hususani kanuni ya 8 (1) na (2).

Kanuni hiyo ya 8 (1) na (2), inaagiza kuwa endapo wagombea wote watakaoshinda nafasi wanazowania kwa sasa ndani ya TFF, hawana budi kuachia nafasi mojawapo katika uongozi wa mpira kwa miguu katika ngazi ya wilaya au mkoa aliyoshinda awali.

BMT imetoa agizo hilo ikiwa ni kukumbushana juu ya utii wa sheria na kuepuka kushika nyadhifa mbili kwa wakati mmoja.

Katika barua yake iliyoandikwa Juni 19, mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, Baraza hilo limesema: “Uchaguzi huu usivuruge amani iliyopo nchini. Wagombea wakumbuke kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.”

Baraza limesisitiza kuwepo na haki katika mchakato mzima kuelekea kwenye uchaguzi. Uchaguzi na mchakato wake uwe huru na amani na usiwe ni kichocheo cha uvunjifu wa amani.

Baada ya viongozi kupatikana, watakula kiapo cha utii, na kujaza fomu Namba 5 ya BMT ya utekelezaji majukumu yao kama Kanuni ya 8 (4) inavyoeleza.

Kadhalika, mara baada ya uchaguzi, Baraza limeagiza kuhusisha baadhi ya vifungu vya sheria ya Baraza ili viendane na katiba za TFF na wadau pamoja na kanuni zao.

………………………………………………………………………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

TFF UCHAGUZI : WAGOMBEA WAFIKA 62, MWISHO KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU JUMANNE JUNI 20!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                           JUNI 19, 2017

MCHAKATO WA UCHUKUAJI FOMU TFF

Wakati kesho Jumanne Juni 20, 2017 itakuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wagombea 62 tayari wamejitokeza.

TFF TOKA SITWanafamilia hao ni wale waliojitokeza kuanzia Ijumaa iliyopita Juni 16, mwaka huu wakiongozwa na Jamal Malinzi aliyekuwa wa kwanza kuchukua fomu kati ya wagombea tisa walioomba nafasi hiyo.

Fomu hizo zinachukuliwa na kurejeshwa katika ofisi za TTF, Karume jijini Dar es Salaam na Uchaguzi wa TFF utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Mbali ya Malinzi, wengine waliochukua fomu hizo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela na Ally Mayay wakati waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais wako Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani na Robert Selasela.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

Soloum Chama

Kaliro Samson

Samwel Daniel

Leopold Mukebezi

Abdallah Mussa

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

Vedastus Lufano

Ephraim Majinge

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

Benista Rugora

Mbasha Matutu

Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

Omari Walii

Sarah Chao

Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

John Kadutu

Issa Bukuku

Abubakar Zebo

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

Kenneth Pesambili

Baraka Mazengo

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya na Iringa;

Elias Mwanjala

Cyprian Kuyava

Erick Ambakisye

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

James Mhagama

Golden Sanga

Vicent Majili

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

Athuman Kambi

Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;

Hussein Mwamba

Mohamed Aden

Musa Sima

Stewart Masima

Ally Suru

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

Charles Mwakambaya

Gabriel Makwawe

Francis Ndulane

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

Khalid Mohamed

Goodluck Moshi

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

Emmanuel Ashery

Ayoub Nyenzi

Saleh Alawi

Shaffih Dauda

Thabit Kandoro

Abdul Sauko

Peter Mhinzi

Ally Kamtande

Said Tully

Mussa Kisoky

Lameck Nyambaya

Ramadhani Nassib

Aziz Khalfan

GHARAMA ZA KUCHULIA FOMU.

 1. Rais TSHS 500,000/=
 2. Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
 3. Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/-

SIFA ZA WAGOMBEA.

 1. Awe raia wa Tanzania.
 2. Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha   Elimu ya Sekondari).
 3. Awe na uzoefu wa uendeshaji Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
 4. Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
 5. Awe na umri angalau miaka 25.
 6. Awe amewahi kuwa ama Mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au ngazi ya daraja la kwanza.
 7. Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
 8. anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 16-20/06/2017 saa kumi (10:00) jioni

..……………………………………………………………………………………………..

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

TOKA TFF: UCHAGUZI KINAMAMA JULAI 8, UCHAGUZI TFF FOMU TOVUTINI, PONGEZI AMIN MICHAEL, RAIS MALINZI AMSHUKURU MGOYI!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI                  JUNI 16, 2017

PONGEZI KWA FRANCIS AMIN MICHAEL

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, amempongeza Francis Amin Michael kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Sudan Kusini (SSFA).

Amin - Mfanyabiashara aliyepata kuwa Mjumbe wa Bodi ya timu Atlabara FC, alishinda nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Juba ambako aliwashinda Lual Maluk Lual na Arop Joh Aguer baada ya kuvuna kura 22 kati ya 34.

TFF-TOKA-SITAmin anamrithi Chabur Goc Alei, ambaye hakutetea nafasi hiyo.

Katika salamu za pongezi, Rais Jamal Malinzi amesema kwamba ana imani na Amin katika nafasi hiyo kwa kuwatumikia vema Wana Sudan Kusini kama alivyoahidi mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.

Rais Malinzi anaamini kwamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Serikali ya Sudan Kusini, ataendeleza mpira wa miguu hususani katika Baraza la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki ambako Tanzania na Sudan Kusini ni nchi wanachama.

TFF YARAHISISHA UPATIKANAJI FOMU ZA UCHAGUZI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwatangazia wanafamilia wote wa mpira wa miguu wenye nia ya kuwania uongozi kuwa limewarahisishia namna ya kupata fomu baada ya tovuti ya TFF: www.tff.or.tz kuwa kwenye marekebisho.

Kwa wanafamilia ambao wapo nje ya Dar es Salaam, wanaotaka fomu hizo kwa sasa hawana budi kutuma ujumbe wa barua pepe kwenda kwenye anwani ya This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. na moja kwa moja atajibiwa kwa kupata fomu hizo ziliazoanza kutolewa leo Juni 16, mwaka huu. Kwa walioko Dar es Salaam, wanaweza kupata fomu hizo katika ofisi za TFF zilizo Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mwanafamilia wa mpira wa miguu mwenye nia ya kugombea ataweza kufungua fomu hizo na kuzijaza huku akifuata utaratibu wa kulipia kwenye nambari ya akaunti 01J1019956700 katika Benki ya CRDB.

Zoezi hili kuchukua fomu na kuzirejesha fomu lililoanza leo Juni 16, litafikia kikomo Juni 20, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya 10.8 ya Uchaguzi kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya TFF.

Mara baada ya kulipia, Mgombea atawajibika kuwasilisha stakabadhi ya malipo kutoka benki na kupewa fomu ya nafasi husika.

Gharama za kuchukulia fomu ni.

1.   Rais TSHS 500,000/=

2.   Makamu wa Rais TSHS 300,000/=

3.   Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/=

RAIS MALINZI AMSHUKURU MGOYI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi amempongeza Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ahmed Mgoyi kwa utumushi mara baada ya kutangaza kutowania nafasi yoyote ya uongozi.

Mjumbe Mgoyi anayewakilisha Mikoa ya Kigoma na Tabora aliandika waraka jana Juni 15, 2017 akielezea kutogombea tena katika Uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

“Nimefanya kazi na Wajumbe wangu wote wa Kamati ya Utendaji. Tumefanya kazi kwa uadilifu mkubwa. Wakati Tukielekea kwenye uchaguzi, mwenzetu ametangaza kutogombea tena, lakini kwa namna nilivyofanya naye kazi, kwangu mimi naamini anahitajika mno, lakini uamuzi wake ni mwisho unakuwa ni wa kwao.

“Naamini kwamba bado ni mwanafamilia wa mpira wa miguu na pindi atakapohitajika kwa lolote lile kama vile ushauri na masuala mengine, basi hatutasita kuwafuata kwa sababu lengo ni kujenga na kuendeleza mpira wetu,” amesema Malinzi.

Katika ujumbe wake, Rais Malinzi amesema kwamba hadhani kama Mgoyi hao atasita au kukataa kutoa ushirikiano kwa uongozi wa shirikisho pindi akihitajika kutoa msaada wao wa mawazo na ushauri.

Rais Malinzi amemtakia kila la kheri katika majukumu yake mengine aliyojipangia kuyafanya huku akiwa bado mwanafamilia wa mpira wa miguu.

MCHAKATO WA UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA LA WANAWAKE TANZANIA (TWFA)

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA), leo Juni 16, 2017 imetangaza rasmi Uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, George Mushumba amesema kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hizo zitaanza kutolewa Juni 19, mwaka huu na kwamba mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa 10.00 jioni. Ratiba kamili kuelekea uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:-

Juni 23, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.

Juni 24, 2017- Kamati ya Uchaguzi kutangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba au kanuni za TWFA.

Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.

Juni 29, 2017-  Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.

Juni 30, 2017-  Usaili kwa wagombea waliotangazwa

Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa

Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa

Julai 03, 2017-  Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa

Julai 04, 2017   Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea

Julai 04 hadi 07, 2017-Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili

Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA

Mushumba amesema kwamba nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji. Sifa ya elimu kwa wagombea wote ni kidato cha nne.

Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi fomu zitanunuliwa kwa Sh 200,000 wakati nafasi za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji fomu zitapoatikana kwa Sh 100,000. Fomu zitapatikana ofisi za Hosteli ya TFF zilizoko Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

.……………………………………………………………………………………………..

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

MUSONYE AZILAUMU KENYA, UGANDA, TANZANIA, RWANDA KWA ‘KUIUA’ CECAFA!

CECAFA, Chombo cha Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati, kimezilaumu Nchi 4 kwa matatizo makubwa yanayowakabili yakiwemo kushindwa kuendesha Mashindano ya Chalenji na Kombe la Kagame kwa Miaka Miwili sasa.

CECAFAKatibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, amesema Nchi za Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda ndizo zinazorotesha shughuli zao.

Musonye amedai matatizo yote yamezuka baada ya Uchaguzi wa CECAFA wa 2015 ambapo Rais wa Chama cha Soka cha Sudan, Muatasim Gafe, alipochaguliwa kuwa Mkuu wa CECAFA.

Musonye amedai zipo siasa nyingi miongoni mwa CECAFA ambayo Wanachama wake ni 12 lakini amezilaumu mno Nchi hizo 4.

Musoke amelalamika: “Wakitaka kuiua CECAFA sawa, ni mtoto wao, Chama chao!”

Alifafanua: “Rais wa Sudan alichaguliwa Rais wa CECAFA katika uchaguzi huru na wa haki. Hawa Wanne wakaamua kutomsapoti Rais mpya! CECAFA si Kampuni yangu! Waache waiue!”

+++++++++++

CECAFA - Wanachama:

NCHI

MWAKA KUJIUNGA

CHAMA

Burundi

1998

Fédération de Football du Burundi

Djibouti

1994

Fédération Djiboutienne de Football

Eritrea

1994

Eritrean National Football Federation

Ethiopia

1983

Ethiopian Football Federation

Kenya

1973

Football Kenya Federation

Rwanda

1995

Fédération Rwandaise de Football Association

Somalia

1973

Somali Football Federation

South Sudan

2012

South Sudan Football Association

Sudan

1975

Sudan Football Association

Tanzania

1973

Tanzania Football Federation

Uganda

1973

Federation of Uganda Football Associations

Zanzibar

1973

Zanzibar Football Association

+++++++++++

Musonye alienda mbali mno na kudai kuzorota kwa CECAFA kumesababisha hata Wanachama wake washindwe kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON.

Amedai: “Kuna uongozi mbovu katika Kanda yetu kwa Miaka mingi nah ii imeathiri Soka. Wanachama wa CECAFA hawalipi Ada zao za Mwaka, hawalipi Ada za Viingilio vya Mashindano. Wanataka kucheza bure!”