VPL: VINARA SIMBA WAPIGWA STOPU MORO, SASA WAKO 2 TU MBELE YA MABINGWA YANGA!

VPL-DTB-SITVINARA wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba Leo wametoka 0-0 na Mtibwa Sugar huko Uwanja wa Jamhuri Jijini Morogoro na kufyekwa pengo lao na Timu ya Pili Yanga kuwa Pointi 2 tu.

Jana Yanga, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa VPL, walicheza Ugenini huko Uwanja wa Majimaji Jijini Sokoine na kutoka na ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Majimaji FC kwa Bao la mapema la Deus Kaseke na kuikaribia Simba wakiwa Pointi 1 tu nyuma yao lakini Leo pengo hilo limekuwa 2 tu badala ya 4 walizotegemea Wadau wa Mtaa wa Msimbazi Jijini Dar.VPL-JAN18A

Usiku huu, huko Azam Complex, Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC watacheza na Mbeya City katika Mechi ya VPL.

VIKOSI:

MTIBWA SUGAR: Said Mohamed, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Henry Joseph, Salim Mbonde, Shaban Nditi, Haruna Chanongo, Ally Makarani, Rashid Mandawa, Jaffary Salum [Hussein Javu, 84’], Vicent Barnabas [Kevin Friday, 78’]

SIMBA: Daniel Agyei, Hamadi Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Method Mwanjali, Abdi Banda, Jonas Mkude, Shiza Kichuya [Jamal Mnyate, 82’], James Kotei, Juma Luizio, Laudit Mavugo [Ibrahim Hajib, 54’], Mwinyi Kazimoto [Pastory Athanas, 75]

VPL - LIGI KUU VODACOM

Ratiba/Matokeo:

**Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni isipokuwa inapotajwa

Ijumaa Januari 13

JKT Ruvu 1 Ruvu Shooting 1

Jumamosi Januari 14

Stand United 2 Mwadui FC 0

Kagera Sugar 2 Ndanda FC 0

Jumapili, Januari 15

Mbao FC 0 African Lyon 0

Jumatatu Januari 16

Toto Africans 1 Tanzania Prisons 1

Jumanne Januari 17

Majimaji FC 0 Yanga 1

Jumatano Januari 18

Mtibwa Sugar 0 Simba 0

1900 Azam FC v Mbeya City [Chamazi, Dar es Salaam]

 

VPL: MABINGWA YANGA WAIPIGA CHINI MAJIMAJI FC!

VPL-DTB-SITVPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo imeendelea huko Uwanja wa Majima Mjini Songea wakati Majimaji FC ilipofungwa 1-0 na Mabingwa Watetezi Yanga.
Bao la ushindi la Yanga lilipachikwa Dakika ya 14 na Deus Kaseke.

Matokeo haya yamewaweka Yanga kuwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Simba ambao kesho wapo huko Jamhuri Jijini Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar.VPL-JAN17
Mechi nyingine ambayo pia itachezwa kesho ni huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Mbeya City.
VPL - LIGI KUU VODACOM
Ratiba/Matokeo:
**Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni isipokuwa inapotajwa
Ijumaa Januari 13
JKT Ruvu 1 Ruvu Shooting 1
Jumamosi Januari 14
Stand United 2 Mwadui FC 0
Kagera Sugar 2 Ndanda FC 0
Jumapili, Januari 15
Mbao FC 0 African Lyon 0
Jumatatu Januari 16
Toto Africans 1 Tanzania Prisons 1
Jumanne Januari 17
Majimaji FC 0 Yanga 1
Jumatano Januari 18
Mtibwa Sugar v Simba [Jamhuri, Morogoro]
1900 Azam FC v Mbeya City [Chamazi, Dar es Salaam]

VPL: LEO MABINGWA YANGA WAKO SONGEA NA MAJIMAJI FC!

VPL-DTB-SITVPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo ipo huko Uwanja wa Majima Mjini Songea wakati Majimaji FC ikicheza na Mabingwa Watetezi Yanga.
Majimaji FC, chini yacKocha Kalimangonga 'Kally' Ongala, wapo Nafasi ya 14 wakiwa na Pointi 17 wakati Yanga wapo Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 40 huku Vinara ni Simba wenye Pointi 44.
Yanga, chini ya Kocha Mkuu wao George Lwandamina, walitua huko Songea tangu Juzi lakini bila ya Wachezaji wao kadhaa maarufu.
Wachezaji ambao hawapo Kikosini ni Beki Vincent Bossou alieko kwenye AFCON 2017 huko Gabon na Nchi yake Togo na Majeruhi Mzimbabwe Donald Ngoma pamoja na Wazambia wao Wawili Justin Zulu na Obrey Chirwa.
Pia Mchezaji wao mpya, Emmanuel Martin, ambae amepatwa na Msiba.
MSIMAMO:
1 Simba SC Mechi 18 Pointi 44
2 Young Africans 18  40
3 Kagera Sugar    19  31
4 Azam FC            18  30
5 Mtibwa Sugar   18  30
6 Stand United     19  25
7 Mbeya City        18  24
8 Ruvu Shooting  19  24
9 Tanzania Prisons 18  22
10 Mwadui FC          19 22
11 African Lyon        18 20
12 Mbao FC              18 19
13 Ndanda FC           19 19
14 Majimaji                18 17
15 Toto Africans       18 16
16 JKT Ruvu              19 15
VPL - LIGI KUU VODACOM
Ratiba/Matokeo:
**Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni isipokuwa inapotajwa
Ijumaa Januari 13
JKT Ruvu 1 Ruvu Shooting 1
Jumamosi Januari 14
Stand United 2 Mwadui FC 0
Kagera Sugar 2 Ndanda FC 0
Jumapili, Januari 15
Mbao FC 0 African Lyon 0
Jumatatu Januari 16
Toto Africans 1 Tanzania Prisons 1
Jumanne Januari 17
Majimaji FC v Yanga [Majimaji, Songea]
Jumatano Januari 18
Mtibwa Sugar v Simba [Jamhuri, Morogoro]
1900 Azam FC v Mbeya City [Chamazi, Dar es Salaam]

VPL: STAND UNITED, KAGERA SUGAR ZASHINDA KWAO, BAO 2 KILA MMOJA!

VPL-DTB-SITVPL, Ligi Kuu Vodacom, ilikuwepo Leo kwenye Viwanja Viwili na kushuhudia Timu za Nyumbani zote zikishinda 2-0.

Huko Shinyanga, Stand United imewacharaza wenzao wa Mkoa huo Mwadui FC Bao 2-0 kwa Bao za Jacob Massawe na Adeyum Salehe na kujikita Nafasi ya 6 wakati Mwadui wapo wa 10.

Huko Kaitaba Mjini Bukoba, Kagera Suga imeifunga Ndanda FC 2-0 kwa Mabao ya Mbaraka Yusuph aliefunga zote.

Ushindi huu umewaweka Kagera Sugar Nafasi ya 3 wakati Ndanda FC wakiwa wa 13.

VPL itaendelea Jumapili kwa Mechi 1 huko CCM Kirumba, VPL-JAN14Mwanza kati ya Mbao FC na African Lyon.

VPL - LIGI KUU VODACOM

Ratiba/Matokeo:

**Mechi zote kuanza Saa 10 Jioni isipokuwa inapotajwa

Ijumaa Januari 13

JKT Ruvu 1 Ruvu Shooting 1

Jumamosi Januari 14

Stand United 2 Mwadui FC 0

Kagera Sugar 2 Ndanda FC 0

Jumapili, Januari 15

Mbao FC v African Lyon [CCM Kirumba, Mwanza]

Jumatatu Januari 16

Toto Africans v Tanzania Prisons [CCM Kirumba, Mwanza]

Jumanne Januari 17

Majimaji FC v Yanga [Majimaji, Songea]

Jumatano Januari 18

Mtibwa Sugar v Simba [Jamhuri, Morogoro]

1900 Azam FC v Mbeya City [Chamazi, Dar es Salaam]

 

MAPINDUZI CUP: HIMID MAO AIPA AZAM FC KOMBE, SIMBA CHALI!

MAPINDUZI17-AZAM-SIMBAHIMID MAO amepeleka Kombe la Mapinduzi ambayo ni Mashindano ya kuenzi Miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Visiwa vya Zanzibar na Pemba, kwa Bao lake pekee wakati Azam FC ikifunga Simba 1-0 Uwanjani Amaan Stadium huko Zanzibar Jana Usiku.

Mao alifunga Bao hilo Dakika ya 13 kwa Shuti kali la Mita 25 ambalo Kipa wa Simba Daniel Agyei hakuona ndani.

Baada ya Mechi hiyo Nahodha wa Azam FC, John Bocco, alikabidhiwa Kombe la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein.

Simba waltinga Fainali hii kwa mbwembwe kubwa baada ya kuwabwaga Watani zao Yanga kwa Mikwaju ya Penati 4-2 na Washabiki wao wengi waliamini hilo liliwafanya wastahili Kombe la kini Azam FC, wakiwa chini ya Kocha wa muda, Idd Cheche, walikuwa na stori nyingine kabisa.

Sasa Timu hizi zote zinarejea Bara kucheza VPL, Ligi Kuu Vidacom, ambapo Simba watakuwa dimbani Jumatano huko Jamhuri, Morogoro kuivaa Mtibwa Sugar na Siku hiyo hiyo Azam FC kuwa kwao Chamazi kucheza na Mbeya City.

VIKOSI VILIVYOANZA:

AZAM FC: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Moris, Yakubu Mohammed, Stephan Mpondo, Joseph Mahundi, Salum Abubakar, John Bocco, Yahya Mohammed, Himid Mao.

SIMBA: Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Juma Luizio, Muzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto

­­KOMBE LA MAPINDUZI

Ratiba/Matokeo:

Desemba 30, 2016

Taifa Jang'ombe 1 Jang'ombe Boys 0

Januari 1, 2017

KVZ 0 URA 2

Simba 2 Taifa Jang'ombe 1

Januari 2, 2017

Azam 1 Zimamoto 0

Yanga 6 Jamhuri 0

Januari 3, 2017

Jang'ombe Boys 2 URA 1

KVZ 0 Simba 1

Januari 4, 2017

Zimamoto 0 Yanga 2

Jamhuri 0 Azam 0

Januari 5, 2017

KVZ 1 Jang'ombe Boys 3

Simba 0 URA 0

Januari 6, 2017

Taifa Jang'ombe 3 KVZ 1

Januari 7, 2017

Jamhuri 0 Zimamoto 2

Yanga 0 Azam 4

Januari 8, 2017

Simba 2 Jang'ombe Boys 0

Taifa Jang'ombe 1 URA 0

Januari 10, 2017

Nusu Fainali

Azam FC 1 Taifa Jang’ombe 0

Simba 0 Yanga 0 [Penati 4-2]

Ijumaa, Januari 13, 2017

FAINALI

Azam FC 1 Simba 0