TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI: YANGA YAIFUMUA NGAYA 5 HUKO COMORO!

CAF-CC-17MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, Leo huko Stade De Moroni Mjini Moroni Visiwani Comoro, wamewafumua Mabingwa wa huko 5-1 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI ambayo ndiyo Mashindano makubwa kabisa kwa Klabu Barani Afrika.

Hadi Mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa Bao 2-0.

Bao za Yanga hii Leo zilipigwa na Justin Zullu, 43', Saimon Msuva, 45', Obrey Chirwa, 59', Tambwe, 65',  na Kamusoko, 73'

++++++++++++++++++++++

Fahamu:

Safari hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.

Mshindi wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.

Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

++++++++++++++++++++++

Timu hizi zitarudiana Jijini Dar es Salaam Wikiendi ijayo na Mshindi kutinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda ambazo Jana zilitoka 0-0 huko Zambia.

Mshindi wa Hatua hiyo ataenda Makundi.

KIKOSI CHA YANGA: Deogratius Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Justin Zullu, Saimoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Obrey Chirwa, Haruna Niyonzima

Akiba: Ali Mustafa, Hassani Kessy, Oscar Joshua, Emanuel Martin, Juma Mahadhi, Juma Saidi, Deusi Kaseke

CAF CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Awali

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Februari 10

KCC – Uganda 1 Primeiro 0

JS Saoura 1 Enugu Rangers – Nigeria 1

JumamosiFebruaria 11

Zanaco – Zambia 0 APR - Rwanda 0

Royal Leopards – Swaziland 0 AS Vita – Congo DR 1

Cnaps Sports – Madagascar 2 Township Rollers – Botswana 1

Zimamoto – Zanzibar 2 Ferroviario Beira – Mozambique 1

Tusker – Kenya 1 AS Port Louis -Mauritius 1

Royal Club du Kadiogo – Burkina Faso 3 Diables Noirs - Congo 0

AS Real de Bamako – Mali 0 Rivers United – Nigeria 0

SS Saint-Louisienne – Reunion 2 Bidvest Wits - South Africa 1

FC Johansens - Sierra Leone 1 Fath Union Sport de Rabat - Morocco 1

Côte d'Or – Seychelles 0 Kedus Giorgis - Ethiopia 2    

Lioli Football Club – Lesotho 0 CAPS United FC - Zimbabwe 0  

AS Tanda - Ivory Coast 3 AS-FAN - Niger 0

CF Mounana – Gabon 2 Vitalo FC - Burundi 0   

US Gorée – Senegal 0 Horoya Athlétique Club - Guinea 0                  

Jumapili Februari 12

Ngaya Club – Comoros 1 Young Africans – Tanzania 5

17:00 Coton Sport FC – Cameroon v Atlabara FC - South Sudan     

17:00 Gambia Ports Authority – Gambia v Sewe Sport - Ivory Coast

17:00 All Stars FC – Ghana v Al-Ahli Tripoli - Libya     

17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v UMS de Loum - Cameroon

19:00 Barrack Young Controllers FC – Liberia v Stade Malien de Bamako - Mali   

19:30 Sony de Ela Nguema - Equatorial Guinea v El Merreikh - Sudan       

CAF CHAMPIONZ LIGI: LEO NI NGAYA NA YANGA ESTADIO DE MORONI, COMORO!

=JANA ZIMAMOTO YA ZENJI 2 FERROVIARIO 1!
CAF-CC-17MASHINDANO MAKUBWA ya Klabu Barani Afrika yalianza Jana kwa Klabu za Tanzania huko Amaan Stadium Zanzibar, wakati Zimamoto ilipoichapa Ferroviario Beira ya Mozambique 2-1 na Leo Yanga wako Ugenini huko Comoro kuivaa Ngaya Club.
Leo pia huko Amaan Stadium Zanzibar, KVZ itacheza na Le Messager Ngozi ya Burundi katika Mechi ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Timu nyingine ya Tanzania ambayo ipo kwenye michuano ya Klabu Afrika ni Azam FC ambayo inaanza Raundi ya ya Timu 32 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Mshindi kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Msafara wa Yanga kuelekea Visiwa vya Comoro ulitua Jana huko Moroni ukiwa na Watu 30 wakiwemo Wachezaji 20, Benchi la Ufundi Mtu 8 na Maafisa Wawili wakiongozwa na Katibu Mkuu Charles Boniface Mkwasa.
Lakini Kikosi cha Timu hiyo kitawakosa Straika wa Zimbabwe Donald Ngoma na pia Malimi Busungu ambao ni Wagonjwa.
Wengine ambao hawamo Kikosini ni Mchezaji wa Togo Vincent Boussou, Pat Ngonyani na Kipa Beno Kakolanya huku Vincent Andrew akiachwa kwa kuwa Kifungoni kutokana na kulambwa Kadi za Njano 3 Msimu uliopita kwenye Mashindano ya CAF.
Msimu uliopita Yanga walitolewa Raundi ya Pili ya Mashindano haya na El Ahly ya Egypt kwa Jumla ya Bao 3-2 katika Mechi 2 na kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho walikofika Hatua ya Makundi na kumaliza Nafasi ya 4 kwenye Kundi B.
Ikiwa Yanga wataitoa Ngaya kwenye Raundi hii ya Awali watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda ambazo Jana zilitoka 0-0 huko Zambia.
Endapo Yanga watavuka tena hatua hiyo watatua Hatua ya Makundi.
Nao Zimamoto, wakivuka Raundi ya Awali, watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi wa Mechi ya Barrack Young Controllers ya Liberia na Stade Malien ya Mali.
==================
Safari hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.
Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.
Mshindi wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.
Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.        
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Awali
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Februari 10
KCC – Uganda 1 Primeiro 0
JS Saoura 1 Enugu Rangers – Nigeria 1
JumamosiFebruaria 11
Zanaco – Zambia 0 APR - Rwanda 0
Royal Leopards – Swaziland 0 AS Vita – Congo DR 1
Cnaps Sports – Madagascar 2 Township Rollers – Botswana 1
Zimamoto – Zanzibar 2 Ferroviario Beira – Mozambique 1
Tusker – Kenya 1 AS Port Louis -Mauritius 1
Royal Club du Kadiogo – Burkina Faso 3 Diables Noirs - Congo 0
AS Real de Bamako – Mali 0 Rivers United – Nigeria 0
SS Saint-Louisienne – Reunion 2 Bidvest Wits - South Africa 1
FC Johansens - Sierra Leone 1 Fath Union Sport de Rabat - Morocco 1
Côte d'Or – Seychelles 0 Kedus Giorgis - Ethiopia 2     
Lioli Football Club – Lesotho 0 CAPS United FC - Zimbabwe 0   
AS Tanda - Ivory Coast 3 AS-FAN - Niger 0
CF Mounana – Gabon 2 Vitalo FC - Burundi 0    
US Gorée – Senegal 0 Horoya Athlétique Club - Guinea 0       
Jumapili Februari 12
15:00 Ngaya Club – Comoros v Young Africans - Tanzania    
17:00 Coton Sport FC – Cameroon v Atlabara FC - South Sudan     
17:00 Gambia Ports Authority – Gambia v Sewe Sport - Ivory Coast
17:00 All Stars FC – Ghana v Al-Ahli Tripoli - Libya     
17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v UMS de Loum - Cameroon
19:00 Barrack Young Controllers FC – Liberia v Stade Malien de Bamako - Mali   
19:30 Sony de Ela Nguema - Equatorial Guinea v El Merreikh - Sudan       
 
TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI: ZIMAMOTO YA ZENJI JUMAMOSI NA FERROVIARIO, JUMAPILI YANGA WAPO COMORO!

>>JUMAPILI NI ZENJI, KVZ NA LE MESSAGER NGOZI YA BURUNDI - KOMBE LA SHIRIKISHO!

CAF-CC-17MASHINDANO makubwa ya Klabu Barani Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI, yanaanza hii Leo kwa Raundi ya Awali lakini Klabu za Tanzania zitaingia dimbani Jumamosi na Jumapili.

Hapo Jumamosi, huko Amaan Stadium Zanzibar, Zimamoto itacheza na Ferroviario Beira ya Mozambique na Jumapili, Yanga wako Ugenini huko Comoro kuivaa Ngaya Club.

Jumapili, huko Amaan Stadium Zanzibar, KVZ itacheza na Le Messager Ngozi ya Burundi katika Mechi ya Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.

Timu nyingine ya TTanzania ambayo ipo kwenye michuano ya Klabu Afrika ni Azam FC ambayo inaanza Raundi ya ya Timu 32 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Mshindi kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Ikiwa Yanga watavuka Raundi hii ya Awali watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi kati ya ZANACO ya Zambia na APR ya Rwanda.

Endapo Yanga watavuka tena hatua hiyo watatua Hatua ya Makundi.

Nao Zimamoto, wakivuka Raundi ya Awali, watatinga Raundi ya Kwanza na kucheza na Mshindi wa Mechi ya Barrack Young Controllers ya Liberia na Stade Malien ya Mali.

Safari hii Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo sasa Kiudhamini yatajulikana kama TOTAL CAF CHAMPIONZ LIGI, yamepanuliwa toka Mawili ya Timu 8 na kuwa Timu 16 ambayo yatakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

Haya ni Mashindano ya 53 ya kusaka Klabu Bingwa Afrika lakini ni ya 21 tangu Mfumo wa CAF CHAMPIONZ LIGI uanze.

Mshindi wa Mashindano haya atafuzu kucheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa Mwaka 2017 huko United Arab Emirates na pia kucheza CAF SUPER CUP dhidi ya Mshindi wa CAF Kombe la Shirikisho.

Bingwa Mtetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.        

CAF CHAMPIONZ LIGI

Raundi ya Awali

Ratiba/Matokeo:

**Saa za Bongo

Ijumaa Februari 10

KCC – Uganda 1 Primeiro 0

2100 JS Saoura v Enugu Rangers – Nigeria

JumamosiFebruaria 11

1600 Zanaco – Zambia v APR - Rwanda

1600 Royal Leopards – Swaziland v AS Vita – Congo DR

1630 Cnaps Sports – Madagascar v Township Rollers – Botswana

1630 Zimamoto – Zanzibar v Ferroviario Beira – Mozambique

1700 Tusker – Kenya v AS Port Louis -Mauritius

1700 Royal Club du Kadiogo – Burkina Faso v Diables Noirs - Congo

1700 AS Real de Bamako – Mali v Rivers United – Nigeria

17:00 SS Saint-Louisienne – Reunion v Bidvest Wits - South Africa 

17:00 FC Johansens - Sierra Leone v Fath Union Sport de Rabat - Morocco

17:00 Côte d'Or – Seychelles v Kedus Giorgis - Ethiopia       

17:00 Lioli Football Club – Lesotho v CAPS United FC - Zimbabwe   

17:00 AS Tanda - Ivory Coast v AS-FAN - Niger

17:30 CF Mounana – Gabon v Vitalo FC - Burundi      

20:00 US Gorée – Senegal v Horoya Athlétique Club - Guinea         

Jumapili Februari 12

15:00 Ngaya Club – Comoros v Young Africans - Tanzania    

17:00 Coton Sport FC – Cameroon v Atlabara FC - South Sudan     

17:00 Gambia Ports Authority – Gambia v Sewe Sport - Ivory Coast

17:00 All Stars FC – Ghana v Al-Ahli Tripoli - Libya     

17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v UMS de Loum - Cameroon

19:00 Barrack Young Controllers FC – Liberia v Stade Malien de Bamako - Mali   

19:30 Sony de Ela Nguema - Equatorial Guinea v El Merreikh - Sudan       

AZAM SPORTS FEDERATION CUP – RAUNDI YA 6: RATIBA YATOKA, MABINGWA YANGA NA KILUVYA, AZAM-MTIBWA, SIMBA-LYON!

AZAM-ASFC-CUP>IPO DABI YA MBEYA!

Raundi ya ya Kombe la Shirikisho la Azam 2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), imetolewa na Mechi zake zitaanza Februari 24.

Raundi hii inashirikisha Jumla ya Timu 16 na Washindi wake kutinga Robo Fainali ambayo itafanyika Droo maalum ili kupanga Mechi zake.

Februari 24 zipo Mechi 4 na Raundi hiyo itaendelea na kumalizika Tarehe 7 Machi wakati Mabingwa Watetezi Yanga wakicheza Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Kiluvya.

Mechi za Februari 24 ni kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar huko Azam Complex, Chamazi na nyingine ni Kagera Sugar v Stand United, Mighty Elephant v Ndanda FC na Madini v JKT Ruvu.

Wakati Azam FC wakicheza Nyumbani kwao Februari 24 na Mtibwa Sugar, Simba watacheza pia Nyumbani hapo Machi Mosi na African Lyon.

Katika Raundi hii, Mechi ngumu ni ile Dabi ya Mbeya kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City na zile za Timu za VPL pekee, Mbao FC na Toto Africans na Kagera Sugar na Stand United.

AZAM SPORTS FEDERATION CUP – RAUNDI YA 5

Ratiba:

ASFC-RAUNDI YA 6

VPL: SIMBA WAICHAPA MAJI MAJI, SASA POINTI 1 NYUMA YA VINARA YANGA!

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Matokeo:

Jumamosi Februari 4

Maji Maji FC 0 Simba 3

+++++++++++++++++++++

VPL-DTB-SITSimba Leo huko Uwanja wa Majimaji Mjini Songeawameichapa Maji Maji FC 3-0 katika ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, na kuwakaribia Vinara Yanga wakiwa Pointi 1 nyuma yao.

Hadi Mapumziko Simba walikuwa mbele 1-0 kwa Bao la Dakika ya 19 la Ibrahim Ajib na Kipindi cha Pili kufunga Bao nyingine 2 kupitia Said Ndemla Dakika ya 63 na Laudit Mavugo Dakika ya 88.

Simba sasa wana Pointi 48 kwa Mechi 21 huku Yanga wakiongoza wakiwa na Pointi 49 kwa Mechi 21 pia.

Timu ya 3 ni Kagera Sugar iliyocheza Mechi 21 na wana Pointi 37 wakifuatia Azam FC wenye Pointi 34 kwa Mechi 20.

VPL – Ligi Kuu Vodacom

Ratiba:

Jumatatu Februari 6

Toto Africans v Ruvu Shooting

Mbeya City v JKT Ruvu

Jumanne Februari 7

Azam FC v Ndanda FC

Jumatano Februari 8

Tanzania Prisons v JKT Ruvu