MUSONYE AZILAUMU KENYA, UGANDA, TANZANIA, RWANDA KWA ‘KUIUA’ CECAFA!

CECAFA, Chombo cha Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati, kimezilaumu Nchi 4 kwa matatizo makubwa yanayowakabili yakiwemo kushindwa kuendesha Mashindano ya Chalenji na Kombe la Kagame kwa Miaka Miwili sasa.

CECAFAKatibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, amesema Nchi za Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda ndizo zinazorotesha shughuli zao.

Musonye amedai matatizo yote yamezuka baada ya Uchaguzi wa CECAFA wa 2015 ambapo Rais wa Chama cha Soka cha Sudan, Muatasim Gafe, alipochaguliwa kuwa Mkuu wa CECAFA.

Musonye amedai zipo siasa nyingi miongoni mwa CECAFA ambayo Wanachama wake ni 12 lakini amezilaumu mno Nchi hizo 4.

Musoke amelalamika: “Wakitaka kuiua CECAFA sawa, ni mtoto wao, Chama chao!”

Alifafanua: “Rais wa Sudan alichaguliwa Rais wa CECAFA katika uchaguzi huru na wa haki. Hawa Wanne wakaamua kutomsapoti Rais mpya! CECAFA si Kampuni yangu! Waache waiue!”

+++++++++++

CECAFA - Wanachama:

NCHI

MWAKA KUJIUNGA

CHAMA

Burundi

1998

Fédération de Football du Burundi

Djibouti

1994

Fédération Djiboutienne de Football

Eritrea

1994

Eritrean National Football Federation

Ethiopia

1983

Ethiopian Football Federation

Kenya

1973

Football Kenya Federation

Rwanda

1995

Fédération Rwandaise de Football Association

Somalia

1973

Somali Football Federation

South Sudan

2012

South Sudan Football Association

Sudan

1975

Sudan Football Association

Tanzania

1973

Tanzania Football Federation

Uganda

1973

Federation of Uganda Football Associations

Zanzibar

1973

Zanzibar Football Association

+++++++++++

Musonye alienda mbali mno na kudai kuzorota kwa CECAFA kumesababisha hata Wanachama wake washindwe kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON.

Amedai: “Kuna uongozi mbovu katika Kanda yetu kwa Miaka mingi nah ii imeathiri Soka. Wanachama wa CECAFA hawalipi Ada zao za Mwaka, hawalipi Ada za Viingilio vya Mashindano. Wanataka kucheza bure!”

Habari MotoMotoZ