AFCON 2019: TANZANIA YAANZA KWA SARE NA LESOTHO!

AFCON2019-LOGOJANA Tanzania imeanza Mechi yake ya Kundi L la kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2019, kwa kutoka Sare 1-1 na Lesotho kwenye Mechi iliyochezwa huko Azam Complex kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.

Kwenye Mechi nyingine ya Kundi L, Wenyeji Cape Verde walitoka 0-0 na Uganda.

Tanzania ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 28 kwa Bao la Nahodha wao Mbwana Samatta na Lesotho kusawazisha Dakika ya 35 kupitia Thepelo Tale.

Katika Mashindano haya yapo Makundi 12 ya Timu 4 kila moja na Mshindi wa kila Kundi atatinga moja kwa moja Fainali wakiungana na Washindi wa Pili wa Makundi Watatu Bora.

++++++++++++++++++++++++++++

MAKUNDI:

A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Madagascar

B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoros

C: Mali, Gabon, Burundi, South Sudan

D: Algeria, Togo, Benin, The Gambia

E: Nigeria, South Africa, Libya, Seychelles

F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya

G: DR Congo, Congo, Zimbabwe, Liberia

H: Ivory Coast, Guinea, Central African Republic, Rwanda

I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania

J: Tunisia, Egypt, Niger, Swaziland

K: Zambia, Mozambique, Guinea-Bissau, Namibia

L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho

**Wenyeji wa Fainali za AFCON 2019, Cameroon, wapo Kundi B lakini wao wanafuzu moja kwa moja kucheza Fainali.

***Washindi wa kila Kundi na Timu za Pili zitakazomaliza Nafasi za Juu Bora 3 zitatinga Fainali

++++++++++++++++++++++++++++

Baada ya Mechi hizi za kwanza, Mechi za Pili za Makundi zitachezwa Machi 2018.

AFCON 2019

Ratiba

**Saa za Bongo

Ijumaa Juni 9      

Sudan 1 Madagascar 3 [KUNDI A]

Libya 5 Seychelles 1 [KUNDI E]

Jumamosi Juni 10     

Malawi 1 Comoros 0 [KUNDI B]

Zambia 0 Mozambique 1 [KUNDI K]

Burundi 3 South Sudan 0 [KUNDI C]

Botswana 0 Mauritania 1 [KUNDI I]

Cameroon 1 Morocco 0 [KUNDI B]

Niger 0 Swaziland 0 [KUNDI J]

Nigeria 9 South Africa 2 [KUNDI E]

Guinea-Bissau 1 Namibia 0 [KUNDI K]

Sierra Leone 2 Kenya 1 [KUNDI F]

Tanzania 1 Lesotho 1 [KUNDI L]

Congo, DR 3 Congo 1 [KUNDI G]

Cape Verde 0 Uganda 0 [KUNDI L]

Burkina Faso 3 Angola 1 [KUNDI I]

Mali 2 Gabon 1 [KUNDI C]

Ivory Coast 2 Guinea 3 [KUNDI H]

Senegal 3 Equatorial Guinea 0 [KUNDI A]

Jumapili Juni 11      

16:00 Zimbabwe v Liberia [KUNDI G]

17:00 Central African Republic v Rwanda [KUNDI H]

18:00 Benin v Gambia [KUNDI D]

18:30 Ghana v Ethiopia [KUNDI F]

Jumatatu Juni 12        

0:00   Algeria v Togo [KUNDI D]

1:00   Tunisia v Egypt [KUNDI J]

TAREHE MUHIMU:

Raundi

Mechdei

Tarehe

MAKUNDI

1

5–13 JunI 2017

2

19–27 Machi 2018

3

3–11 Septemba 2018

4

5

8–16 Oktoba 2018

6

5–13 Novemba 2018

Habari MotoMotoZ